Uteuzi: Rais Samia amteua Humphrey Polepole kuwa Balozi Malawi, Mchechu arudishwa NHC

Polepole kamuenzi JPM,kabaki na ulimi mmoja mpaka sasa,na hatimaye kaula.
Mkuu, hapo jamaa kazimwa aachane na wahuni, kama ni suala la ulaji hata ubunge ulikuwa na pesa tu
 
Polepole kamuenzi JPM,kabaki na ulimi mmoja mpaka sasa,na hatimaye kaula.
Kwa akili yako wewe unaona kaula? Bora ungeishia kusoma tu bila kukomenti chochote. Ona sasa unavyoonekana mpumbavu kwa vitu vya kujitakia.
 
tatizo ukikataa unaonekana huna maslahi na nchi bali ni tumbo lako binafsi, kwani hata huko Malawi unawakilisha maslahi ya Taifa lako
 
Hivi inakuwaje mstaafu anarudishwa kazini?

Huku ndio kupeana mashavu sasa. Huku watoto wa maskini waliojikongoja kusoma wanaambiwa waende veta au wajiajiri..

Recycling bad, old, broken, tired people, with nothing new to offer. Uwezo mdogo wa kuchagua watu sahihi kuongoza na kusimamia Taasisi, idara na wizara nyeti kwa maslahi ya Tanzania unaligharimu na utaligharimu sana hili taifa.
 
Hata mimi naona atose uteuzi kwani watu wangapi wanaishi bila kutegemea uteuzi! Kama atakubali kwisha habari yake! Maana aliyemteua hana nia njema na yeye! Atajilisha upepo tu hata kama ataenda huko!
Wapambe njaa 😬😬
 
Juzi waliidhinisha mkopo wa kibiashara tsh 164 billioni with government guarantee NHC wamalizie miradi yao iliyokwamia kati washapewa first payment tsh 40 billion.

NHC ilikopa zaidi ya tsh 1 trillion zama za J.K miradi ambayo aikulipa. Kwakuwa mkopo ulikuwa na government guarantee sasa hivi deni linalipwa na walipa kodi.

Nehemia alipotaka tena government guarantee kwa miradi ambayo keshaikopea ilihali madeni ya awali serikali inamlipia for poor investment decision and poor management of costs za miradi ndio JPM alipoona upuuzi na kumtimua.

Mama shida, hiyo kazi sio size yake ni wazi nani anaongoza nchi kwa sasa. Inaonekana anawaza kuendelea baada 2025 come whatever na kufanya ivyo inabidi amfurahishe mwafulani akiamini anaweza mudu mikiki ya 2025.

Kumalizia miradi sio shida but does it have to be the same people who caused the problems in the first place.
 
Mbona Malawi karibu ni bora angepelekwa Ukraine huko kungemfaa zaidi
 
Nehemia Mchechu NHC tena? Ni sababu zipi zilipelekea kutumbuliwa? Hazikuwa genuine?Hivi hakuna watanzania wengine?
Kizazi cha mchwa kilianza kurudi mapema tu baada ya mama kushika usukani.
 
Akikataa Uteuzi wa Rais kesho kutwa yule Muandishi wa Barua ya Mnyika ya kuteua Kina Halima Mdee na ya kujiuzulu Ndugai anaingia Jikoni na huwa hakosei mapishi
Nimecheka sana hii coment
 
Kashika kidevu
 
Nauliza tu sio kwa ubaya.
Hivi Polepole Ana mke na watoto?
Maana kila Mara namuona anapika au amehifadhi KY.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…