Uteuzi: Rais Samia amteua Humphrey Polepole kuwa Balozi Malawi, Mchechu arudishwa NHC

Uteuzi: Rais Samia amteua Humphrey Polepole kuwa Balozi Malawi, Mchechu arudishwa NHC

Rais Samia Suluhu amemteua Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Sambamba na hilo Rais Samia Suluhu amemteua Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia Rais Samia Suluhu amemteua Waziri Kindamba kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Kindamba alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL na anachukua nafasi ya Mhandisi Marwa Rubirya ambaye amestaafu kwa umri.

Polepole na Kindamba wanatarajiwa kuapishwa kesho Jumanne tarehe 15 Machi 2022 Ikulu ya Chamwino Dodoma saa 04:00 Asubuhi.

Katika hatua nyingine Rais Samia Suluhu amemteua Nehemia Mchechu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Mchechu ambaye amewahi kuhudumu kwenye wadhifa huo, anachukua nafasi ya Dkt. Maulid Banyani ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Pia amemteua Balozi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (Mstaafu) Ernest Jumbe Mangu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari (Tanzania Port Authority)

View attachment 2150380


Yale Yale ya Nchimbi = na hii ya Polepole.
 
Back
Top Bottom