Uteuzi: Rais Samia amteua Humphrey Polepole kuwa Balozi Malawi, Mchechu arudishwa NHC

Uteuzi: Rais Samia amteua Humphrey Polepole kuwa Balozi Malawi, Mchechu arudishwa NHC

Ameteuliwa leo na kuapishwa ni kesho..yani hajapewa hata nafasi ya kujitafakari kuhusu uteuzi....na pia ameteuliwa kuwa balozi na hapo hapo vuai nahodha ameteuliwa kuchukua nafasi ya pole pole...amepewa options ngumu sana hapo polepole..lazima akubali tu hio teuzi maana mbadala wake ameshateuliwa tayari

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna haja ya kukataa, kama anaamini katika Mungu basi atulie aende...Siku asiyoitegemea atalipwa mara saba yake
 
Rais Samia Suluhu amemteua Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Sambamba na hilo Rais Samia Suluhu amemteua Shamsi Vuai Nahodha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia Rais Samia Suluhu amemteua Waziri Kindamba kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Kindamba alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL na anachukua nafasi ya Mhandisi Marwa Rubirya ambaye amestaafu kwa umri.

Polepole na Kindamba wanatarajiwa kuapishwa kesho Jumanne tarehe 15 Machi 2022 Ikulu ya Chamwino Dodoma saa 04:00 Asubuhi.

Katika hatua nyingine Rais Samia Suluhu amemteua Nehemia Mchechu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Mchechu ambaye amewahi kuhudumu kwenye wadhifa huo, anachukua nafasi ya Dkt. Maulid Banyani ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Pia amemteua Balozi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (Mstaafu) Ernest Jumbe Mangu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Bandari (Tanzania Port Authority)

View attachment 2150380


Kama nilivyoshauri! Polepole atafutiwe ubalozi wa Malawi akapigie kelele zake huko! 😂. Hii itamsaidia vilevile maana siasa sio kazi lakini ubalozi ni kazi.
 
Nehemia Mchechu NHC tena? Ni sababu zipi zilipelekea kutumbuliwa? Hazikuwa genuine?Hivi hakuna watanzania wengine?
Huyoo ndoo aliyesimamia ule ujenZi wa gorofa lile refu kule Dubai Kama hujui unajui kikwete ndoo alimkuta kule karudi eneo lake. Ashukuru Safari yamama farume zakiarabu
 

POLEPOLE KUWA BALOZI MALAWI…usiende.​

Ukienda unafanyiwa kile alichofanyiwa Dr Emmanuel Nchimbi kupelekwa Brazil kuwa Balozi sasa anachunga mbuzi kule Goba Dar.​

Ataitwa kwenye chama kwa utovu wa nidhamu
 

POLEPOLE KUWA BALOZI MALAWI… kuteuliwa tarehe 14.3.2022 kuapishwa tarehe 15.3.2022 ?​

Kwanini ni dharura hivyo? Msechu wa NHC alifukuzwa na JPM na Samia leo anapewa nafasi ile ile na Samia?​

Mwenye kufahamu Samia anakutupeleka anielewesha tafadhali, mimi ninaona kama tunapotea njia.​

We kuwa mpole uongozwee
Tu

Ova
 

POLEPOLE KUWA BALOZI MALAWI…usiende.​

Ukienda unafanyiwa kile alichofanyiwa Dr Emmanuel Nchimbi kupelekwa Brazil kuwa Balozi sasa anachunga mbuzi kule Goba Dar.​

shida ni kwamba huwezi kataa..si kwamba unataka ila sababu system inakua inataka iwe hivyo. na yeye anaijua system inaweza kumfanya nini asipochukua hio option..
 
Kutoka mshahara milioni 12, posho laki tatu kwa kikao, mafuta Lita 1000, ziara za kukagua miradi nchi nzima.....politically finished
Ubalozi mshahara shillingi ngapi?
 
Nehemia Mchechu NHC tena? Ni sababu zipi zilipelekea kutumbuliwa? Hazikuwa genuine?Hivi hakuna watanzania wengine?
Hujui kuwa alikuwa ameteuliwa kwenye nafasi hiyo na Kikwete?

Kesho huko NHC kutafanyika bonge la Party maaana Mchechu ni Kipenzi cha Wafanyakazi kwa jinsi anavyojali maslahi yao .
Banyani nae alikuwa jembe sana pia

Labda maslahi hayo ni yale yaliyo nje ya sheria, ila maslahi ya kawaida kama mishahara na stahiki zake naona ni mambo ya kawaida bila kujali nmkurugenzi ni nani. Sasa kama alikuwa anaruhuru watu kujipatia maslahi kwa urefu wa kamba zao, basi watafurahi tena.

Kibali Cha kukopa bil 300 kwenye commercial banks, ili kumalizia ili kumalizia Morocco square

Sababu iliyomfukuzisha wakati huo ni hiyo hiyo, baada ya uchunguzi ulioongozwa na mwenyekiti ya bodi ilionekana ufujaji mkubwa ulikuwa umefanyika.

1647277912780.png

1647278017485.png
 
Back
Top Bottom