Uteuzi: Rais Samia amteua Nehemia Mchechu kuwa Msajili Hazina

Uteuzi: Rais Samia amteua Nehemia Mchechu kuwa Msajili Hazina

Hii ya Msechu ni kupanda cheo au demosition?

By the way Kwa nini majina Yale Yale miaka na miaka?
Nashindwa kuelewa hata saa ngapi wanafanya hizo kazi .
Ukikaa kidogo kuweka tako ofisini ushatenguliwa, bado unaaga ushateuliwa, uko safarini kuelekea kituo kipya cha kazi ushapangiwa kazi ingine
 
Naamini Mchechu aliulizwa tumuweke ani badala yako,ila kuendelea kuwa na mirija NHC akamkumbuka jamaa yake . Ni mwendo wa si kulamba asali tu bali kufakamia asali,tena asali ile ya nyuki wadogo wasiong'ata.
Wewe ndo unaweza kua umeongea kitu hapa.wengine wanaropoka hamna wanachojua..mchechu na Hamad ni kulwa na dotto
 
Msajili wa Hazina ni msimamizi wa mashirika yaliyobinafsishwa,yanayosubiri kubinafsishwa,yaliyoshindwa masharti ya ubinafsishàji,yaliyorejeshwa serikalini.
Tegemea mabadiliko katika aina ya mashirika niliyoyataja hapo juu("reforms')
 

Attachments

  • Screenshot_20230225-074807.png
    Screenshot_20230225-074807.png
    107.7 KB · Views: 6
Ni kweli, Zanzibar ni sehemu ya Tanzania ila Tanzania sio sehemu ya Zanzibar.

Mzanzibari ni mtanzania ila sio kila mtanzania ni Mzanzibari.

Mali ya Tanzania ni mali ya Zanzibar ila mali ya Zanzibar sio mali ya Tanzania.

Muungano wa hovyo toka Dunia imeumbwa.
Kinachofanyika hapo ni kutafuta wasio taka muungano toka Pande zote mbili wawe wengi ili watu wajitenge tofauti na hapo mwanzo wengi walikuwa hawataku muungano walikuwa wanatokea Visiwani Tz
 
Safu inazidi kupangwa kwa kuchota uzoefu kutoka sekta binafsi kama alionao Musa Makame sekta ya gesi na mafuta kimataifa

TOKA MAKTABA :
10 June 2022


Waziri January ateaua wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa TPDC
3. Musa Makame — Mshauri Mwelekezi katika sekta ya mafuta na gesi. Aliwahi kuwa Afisa Mwandamizi wa Biashara katika kampuni ya Equinor (zamani Statoil) na kabla ya hapo Makamu wa Rais (Fedha na Utawala) katika kampuni ya Wentworth (zamani Artumas).
Read more : Waziri January Makamba, ateua Wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa TPDC


Toka maktaba :
Bw. Hamad Abdallah Mkurugenzi mtendaji wa GIMCOAFRICA. Uzoefu wake unaweza uuzwaji, upangaji na kodi kwa majengo ya NHC unaweza kupata mabadiliko chanya na pia kukamilisha miradi iliyokwama ya NHC hata ile ya NSSF Dege Beach Kigamboni DSM isigeuke magofu chakavu

Wakadiriaji wa thamani za majengo estate agency upangaji majumba GIMCOAFRICA
psssf

2N0A9938(5)_resized

GIMCOAFRICA LTD is a Property Management and Valuation firm incorporated in Tanzania. has a qualified team of professionals that provide a wide range of commercial, residential agency and consultancy services. With Gimcoafrica you will find a dependable and knowledgeable partner to work with in all your real estate issues.

Venture Consultants Firm incorporated in Tanzania.

The firm is registered and authorized to practice Property Management, Property Development Consultancy, Letting and Marketing,Estate Agency and Valuation in Tanzania by the National Council of Professional Surveyors and the Valuers Registration Board is also registered by the Tanzania Institution of Valuers and Estate Agents (TIVEA) as a Corporate Member
Hao GIMCO ni madalali waliotukuka tu. Wamejenga ghorofa gani au estate gani mpaka MD wao awe na wasifu wa kuwa MD wa NHC?

NHC inakwenda kudorora sasa.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

1. Amemteua Bw. Nehemia Kyando Mchechu, kuwa Msajili wa Hazina. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mchechu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Bw. Mchechu anachukua nafasi ya Bw. Mgonya Benedicto ambaye atapangiwa kazi nyingine.

2. Amemteua Bw. Hamad Abdallah, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Abdallah alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Gimcoafrica Limited na anachukua nafasi ya Bw. Mchechu ambaye ameteuliwa kuwa Msajili wa Hazina.

3. Amemteua Bw. Mussa Mohammed Makame, kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Makame alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na pia ni Mshauri Mwelekezi wa masuala ya mafuta na gesi nchini Tanzania. Bw Makame anachukua nafasi ya Dkt. James Mataragio ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Uteuzi huu ni kuanzia tarehe 24 Februari, 2023.

View attachment 2528416

=====

MAJUKUMU YA OFISI YA MSAJILI WA HAZINA
Kwa mujibu wa Kifungu cha 10 cha Sheria ya Msajili wa Hazina Sura 370 kama ilivyorekebishwa, Ofisi imepewa majukumu yafuatayo: –

1. Kufanya mapitio ya kudumu ama kuhakikisha kunafanyika mapitio ya kudumu ya shughuli na mwenendo wa watu ama Taasisi ambazo Msajili wa Hazina anamiliki mali ama ana maslahi kwa mujibu wa Sheria.

2. Bila kuathiri Kifungu kidogo cha (1) kwa ujumla wake, Msajili wa Hazina anatakiwa:
  • Kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu uanzishaji wa Mashirika ya Umma na kusimamia biashara au mali zilizowekezwa kwenye Mashirika hayo;
  • Kupitia utendaji wa kifedha wa Mashirika kwa lengo la kushauri hatua za kuchukua katika kuunganisha, kuboresha muundo, kufuta au kuboresha utendaji wa Mashirika na Taasisi za Umma;
  • Kuweka malengo ya kifedha na vigezo vingine vya utendaji vitakavyotumiwa na Mashirika na Taasisi za Umma;
  • Kufanya tathmini mara kwa mara ili kupima utendaji wa Bodi au Menejimenti za Mashirika na kutoa mapendekezo kwa Serikali ya hatua za haraka au zilizopo za kuboresha usimamizi wa rasilimali;
  • Kuidhinisha uwekezaji wa hisa unaofanywa na Mashirika ya Umma kwenye Mashirika au Kampuni nyingine;
  • Kuwekeza au kuuza mali za Mashirika ya Umma;
  • Kuhakikisha kuwa kila Shirika la Umma linaingia Mkataba wa Utendaji na Msajili wa Hazina mara moja baada ya kuteuliwa kwa Bodi ya Wakurugenzi;
  • Kufuatilia na kutathmini programu za mafunzo katika Mashirika na Taasisi za Umma;
  • Kuelekeza au kuidhinisha matumizi au marekebisho ya kanuni za fedha ili kuhakikisha usahihi wa taarifa za mapato na matumizi ya Mashirika ya Umma;
  • Kuchambua na kuidhinisha Miundo na Mifumo ya Mishahara, Kanuni za Utumishi na Mpango wa Motisha kwa Mashirika na Taasisi za Umma;
  • Kufuatilia misaada, ruzuku, fedha za mtaji, akiba au malimbikizo ya faida katika Mashirika ya Umma na kwenye uwekezaji mwingine wa Umma;
  • Kupendekeza au kuidhinisha Mipango ya Mwaka ya Mashirika na Taasisi za Umma;
  • Kufuatilia na kutathmini utendaji wa Mashirika na Taasisi za Umma; na
  • Kufanya ufuatiliaji na kuhakikisha gawio, michango na mikopo kutoka katika Mashirika na Taasisi za Umma inalipwa kwa wakati.
Nachukia kwani hakuna watu wengine wenye taluma hiyo hadi miaka na miaka majina kujirudia?
 
Back
Top Bottom