UTEUZI: Rais Samia ateua Balozi mmoja na kumhamisha Humphrey Polepole kuwa Balozi nchini Cuba

Hongera Mh. Polepole MUNGU azidi kukupaisha Hadi siku Moja utusaidie kuondoa wahani
 
Endelea kujipa moyo hivyohivyo
 
Mabalozi wanapaswa wawe wanapitia Bungeni kwanza kuchekechwa
 
Wewe hujuhi kitu kaa kimya..
CCM Ina wenyewe lakini SYSTEM INAWENYEWE PIA.

unadhani magufuli kuwa rais ilikuwa NI coincidence tu?
Haya mambo muulize mzee
Mkuchika .
Acheni kuwa overrate hao SYSTEM kilichotokea 2015 ni hofu ya Lowassa na CCM kuwa branded mafisadi so ikabidi tu waweke mgombea mwenye element za kichadema Chadema Ili at least wapinzani wampe kura ila sio kwamba system iliamua Bali ni JK aliona hali mbaya na kwamba CCM ingeanguka licha ya kuiba kura

Kama SYSTEM ilimtaka JPM angekufa kizembe hivo? Taarifa zake zingevuja kiasi hiko? Mpaka kina kigogo sijui mange walipata za jikoni kabisa unadhani sio account za system? Au hao system hawakujua afya ya JPM na kuandaa successor mpaka wamueweke Samia ambaye obviously ni mtu wa JK?

Mkikubali system imemuweka JPM then mnazidi kuonyesha kwa uwazi ilivyo poor kwenye succession management.
 
Endelea kujipa moyo hivyohivyo
Nani anajipa moyo wakati mambo Yako wazi? Nafasi ya uenezi aliyewahi kuwa na ushawishi ni Nape pekee wengine wote hawana mvuto wa kisiasa Hadi Leo so msidanganye eti Polepole anaweza tingisha Rais hiko kitu hakipo Tanzania. Walishindwa kwa JK wakashindwa kwa JPM ndio sembuse Samia?
 
Ama kweli mambo yamebadilika na JPM hayuko tena duniani.

Hadi wewe Kichuguu tunayekufahamu mtetezi wa kila jambo la serikali leo unalalamika!

Inashangaza sana.
Una kichaa wewe kama huo ndio mchango wako kwenye topiki hii. JPM alikuwa habadilisihi badilishi namna hii, ni ama "anatumbua" moja kwa moja au "anakekemea makosa hadharani na kutishia kutumbua". Hakuwa anabadilibadili mara leo hapa mara kesho pale. Hebu eleza ni teuzi ngapi ambazo JPM alikuwa anahamisha hamaisha na kutengua tengua bila taarifa iwapo siyo wale aliokuwa "anatumbua kwa makosa fulani" na ikawa inajulikana fulani "katumbuliwa" kwa kosa fulani.

Mtu anapowekwa katika nafasi fulani, huchukua muda kuielewa nafasi ile na kujenga mikakati ya kukabiliana na changanote zake; kabla hajakamilisha mikakati yake anahamishiwa katika nafasi nyingine ambako ataanza upya; hiyo inapunguza sana ufanisi.
 
Ila alipofanya JPM it was okay kutumbua almost Kila wiki? Hizi double standards haziwezi saidia taifa letu.
 
Kila hatua ina heri

Hongera kwake Humphrey
Ndio wameenda kumzika huko, hahaa Nchimbi yuko wapi now? Wazee nduo wanajua alikuwa mwanasiasa, ila vijana wa sasa hakuna anaye mjua, Polepole ndio mwisho wake sasa
 
Ni mjanjamjanja sana na cuba itaiweza kama alivyoweza Malawi

USSR
Cuba aiweze vipi? Kwa kifupi wamempeleka mbali make inaonekana Malawi alikuwa anakurana na watu wake kupanga mikakati
 
Kabisa na ndio mwisho wake kisiasa sasa
 
Tuna katiba ya kuteua na kutengua tu. Halafu linapokuja suala la kuwashughulikia wala rushwa na mafisadi, katiba hiyo hiyo huwageuza watawala kuwa walalamikaji.
Umeandika hoja ya msingi sana.

Mtawala sasa ameamua kujitafutia kazi rahisi awe anaifanya kila siku, na kwa ujinga wetu tunaijadili kila siku kwa kuitungia vijisababu kwanini huyu kaondolewa hapa kapelekwa pale, utadhani hadhi ya ubalozi inashuka kulingana na taifa analopelekwa balozi husika.
 
Hana mipango yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…