Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hoja za udini ni hoja dhaifu sana na zinaonyesha kutokuwa na uelewa. Mimi ni Mkristu wa madhehebu ya KATOLIKI ila siamini kama kuna upendeleo kwa Waisalamu kwa kuwa Rais ni Mwislamu. Kimsingi kwa Tanzania ambayo ni secular state, kuamini kuwa Rais anateua maafisa kwa dini zao ni UPUMBAVUWaislam watano (5) na wakristo watatu (3) ngoja amalize kipindi chake cha mpito, hii ni kusudi tu ili kuleta public debates as spinning for public deviations.
umetisha nilitaka kushanga wanakosekaneje
Nilifikiri kwa taifa masikini watu wanaojua biashara na uchumi ndio walipaswa kujaa ubalozini ili wavutie uwekezaji nchini!Ofisi za ubalozi 80% ni Askari, TISS, JWTZ au Polisi.
Ubalozi ni pamoja na USHUSHUSHU kiongozi wangu.
Naomba kujua hapa wa Ijumaa ni wangapi na wale wa Jumapili nao ni wangapi.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mabalozi kama ifuatavyo:
1.Amemteua Meja Jenerali Ramson Godwin Mwaisaka kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo, Meja Jenerali Mwaisaka alikuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji (JWTZ).
2.Amemteua Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Simuli alikuwa Mkuu wa Utumishi Jeshini (JWTZ).
3.Amemteua Bw. Mohamed Awesu kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Awesu alikuwa Konseli Mkuu, Konseli ya Tanzania, Jeddah Saudia Arabia.
4.Amemteua Bw. Gelasius Byakanwa kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Byakanwa alikuwa Afisa Mkuu Ubalozi wa Tanzania, Korea ya Kusini.
5.Amemteua Dkt. Mohamed Juma Abdallah kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Dkt. Abdallah alikuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kaskazini Unguja.
6.Amemteua Bw. Hassan Mwamweta kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mwamweta alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mwandamizi na Mkuu wa Utawala, Ubalozi wa Tanzania, Uturuki.
7.Amemteua Bw. Imani Salum Njalikai kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Njalikai alikuwa Afisa wa Mambo ya Nje Mkuu na Msaidizi wa Waziri Mkuu – Hotuba
8. Amemteua Bw. Khamis Mussa Omar kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huo Bw. Mussa alikuwa Kaimu Mwakilishi wa Kudumu, Ubalozi wa Tanzania Ufaransa.
Uteuzi huu wa Mabalozi umeanza tarehe 10 Mei, 2023 na wataapishwa kwa tarehe itakayopangwa baadae.
View attachment 2630981
Nadhani watapangiwa vituo baadae maana hata kuapishwa ni baadae piaMabalozi wa nchi zipi, au wa nyumba kumi kumi?
unashangaa meja jenerali?Meja Jenerali, IGP unawateua mabalozi. Heri uambiwe toka ulipo kaka nyumbani italipwa mashahara wako mpaka ustaafu. Ubalozi umekuwa sehemu ya kutupa wasiopendeka.
Hapo wala siyo kurina asali bali ni kulamba tu,wanaorina ni sisi walipa kodi na tozo.Hakika mkuu,
Kurina asali mpk unaingia kaburini [emoji4]
Mwanzo mlidai waislamu hawajasoma wanaendekeza elimu ya madrasa sasa japo wachache wamesoma wanatupiwatupiwa kidogo mnaanza kulalamika! Omba wapeleke muswada bungeni iwe 50 kwa 50 basi.4 : 4
hahahahahahahaha aisee nimecheka vibaya mno mpaka nimesweat. Kah!
Akili ndogo always! Kujikomba ili uwemo!Uteuzi unazingatia sifa na vigezo tuu, sio jinsia, dini, Kanda au kabila. Hata ikitokea wateuliwa wote wakiwa dini moja au kabila moja, let it be!.
P
Huyo HR mkuu ndio kipindi chake recruitment ya JWTZ ukiwa na hela unaingia kwa assist. Unamuona wa muhimu sana ila simuoni hivyo, kwanza appointments za kabila fulani zilikuwa nyingi na figisu ziliongezeka ndani.Nataka kuona kaondoa hawa maafisa waandamizi wa ngazi za juu JWTZ wote ‘wagalatia’ toka Bara ataleta akina nani toka wapi!
Kuna kitu nafanyia tafiti teuzi za watakao ziba nafasi zao zitahitimisha tafiti yangu
Kumbuka hawa Major -Generals wawili nafasi zao ni muhimu sana ktk JWTZ.Mmoja ndiyo mkuu wa utumishi JWTZ nafasi nono sana kiutendaji na mwingine mkuu wa kamandi ya jeshi la majini,nafasi ya maana sana.
Wataletwa akina nani kujaza hizi nafasi?
Wanajeshi wanastaafu bado wana nguvu na umri unaruhusu kulingana na utaratibu wa kustaafu ulivyo jeshini, na nchi inatumia gharama nyingi kuwafundisha na kuwafikisha hatua hiyo. Kumpata officer cadet pekee ni procces sasa imagine kumpata Meja Jenerali.Meja Jenerali, IGP unawateua mabalozi. Heri uambiwe toka ulipo kaka nyumbani italipwa mashahara wako mpaka ustaafu. Ubalozi umekuwa sehemu ya kutupa wasiopendeka.
Hapo sasa. Au china, au Russia.Ushushu utaufanya USA kweli? Unaanzaje? Labda Burundi