Uteuzi wa Nehemia Mchechu: Tunamchekea Rais Samia, lakini hapa ameonyesha udhaifu mkubwa

Uteuzi wa Nehemia Mchechu: Tunamchekea Rais Samia, lakini hapa ameonyesha udhaifu mkubwa

Mimi nakubaliana na wewe, na ndio Hawa wakiambiwa katiba wanaruka. Nafasi Kama hizi hazikupaswa kuwa za uteuzi, ilipaswa kushindaniwa
Kushindaniwa tena kwa uwazi kabisa...
Na hata kama ni lazima uteuzi kuwepo na vetting authority ambayo itawahoji na kujiridhisha!
Anachokifanya Rais wa Tanzania ukii narrow it down to a family level ni sawa kabisa na mfume dume! Mtu mmoja anajua kila kitu na hakoseagi!!
SI KWELI! SI SAWA! SI SAHIHI!!
Tatizo wengi wanafikiria kwa matumbo, masikio na macho!!
So based on use and disuse principle akili kwao si muhimu tena!
 
Walipo badilisha na kumwondoa Nehemia, si unaona shirika lilikuwa kama halina boss? Kwahiyo utaona mpya hakuwa na jipya

Mchechu na timu yake ya akina maagi waliamsha sana nhc. Africa na hasa tanzania hakuna ambaye sio mwizi, ila uzur wake (nehemia) kazi na tija inaonekana.

i hope sasa nehemia atajifunza na kuwa mzalendo. Kudos mama

Andiko hili hapa chini linaonyesha kuwa tume iliundwa na kuongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya NHC mwenyewe wakagundua kuwa kulikuwa na ubadhilifu mkubwa sana wa fedha mpaka wakafikia kuomba serikali iwadhamini kukopa kwenye mabenki ya biashara. Inawezekana wafanyakazi waliokuwa wanafaidi huo ubadhirifu walipoona wamekatiwa miriija yao ndipo wakaingia mgomo baridi.

1647277912780-png.2150411

1647278017485-png.2150415
 
Walipo badilisha na kumwondoa Nehemia, si unaona shirika lilikuwa kama halina boss? Kwahiyo utaona mpya hakuwa na jipya

Mchechu na timu yake ya akina maagi waliamsha sana nhc. Africa na hasa tanzania hakuna ambaye sio mwizi, ila uzur wake (nehemia) kazi na tija inaonekana.

i hope sasa nehemia atajifunza na kuwa mzalendo. Kudos mama
Ebu niambie mbali na Dar kulikojengwa maghorofa ya mchongo kwa matajiri tu, achana na yale yaliyojengwa Magomeni enzi ya Magufuli. Ni mkoa gani mwingine ulionufaika na ujenzi wa majengo ya kisasa? Ni wapi wananchi wa kawaida walinufaika na NHC chini ya uongozi wa Nehemia?

Sitaki kuongelea mamilioni ya fedha aliyokuwa anajilipa, na mashule alojenga, majumba anayomiliki, ambayo kabla ya kuwa meneja hakuwa navyo. Sitaki kuongelea alivyokuwa anamwaga fedha mamillioni. Ilikuwa bahati yake. Sitaki kuwa na wivu nae.
Mie nakumbuka NHC ya zamani ilijenga nyumba Tanzania nzima. Tena wengi waliofaidika ni watu wa chini. Mashirika kama haya nchi nyingine yamekuwa na REAL ESTATES kubwa na kuendezesha miji.

Siyo miaka ya Nehemia na vile vigorofa vya Morocco, basi tukaona amefanya kazi, na kuwa na kipindi. Nimetembelea Ethiopia, shirika la nyumba, limejenga majengo ya ghorofa nchi zima na nimazuri. Na bei nafuu sana nyumba zao. nchi inajengeka utazani Singapore.
NHC haijapata mtu alonavision ya kuwasaidia watanzania. NHC ilitakiwa ibadili madhari ya miji mingi Tanzania, si kuishia Dar es Salaam kujenga vigorofa viwili wanatumia hela nyingi kupoteza muda ati kipindi cha Nyumba! Ha ha ha!

Nehemia, hana tena jipya, kama miaka alotumia, hakufanya cha maana anaporejeshwa sasa atafanya nini? Kikubwa ni madili kujenga maghorofa machache Dar na kuwapa alionao michongo, wamiliki, nao wapangishe kwa matajiri.

Mfano pale mwanza milimani, Dar es Salaam maeneo ya Manzese, Mburahati na kadhalika, haya ni maeneo ambayo NHC ingeingia ubia na wananchi na kujenga majumba au maghorofa ya makazi, kisha wananchi hawa kupangishwa na baadae kuuziwa.

Hata vijijini, NHC ingekuwa na maono kusaidia wananchi wa vijijini kuwajengea makazi bora kwa makubaliano maalum, na kuondoa vijumba vya ajabu na vile vya nyasi. Nampongeza Rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Karume, alikuwa na akili sana huyu, vijijini au shamba kama wanavyoita wa Zanzibar alijenga maghorofa akaweka umeme na maji, mbali na yale maghorofa ya Michenzani, naongelea ya vijijini kama Bambi na kadhalika. Alitaka wananchi wa hali ya nchini wapate makazi safi. Hadi leo hakuna Rais alofanya kazi kama ya Marehemu Karume.

Nehemia hana jipya tena. Hivi nchi yetu haina watu wengine? Hivi hawa ndo tu walio na brain kuliko watanzania wengine? Mie nadhani Nehemia angepewa nafasi nyingine za uteuzi lakini si kumrudisha palepale ambapo kwa kuangalia hakuwa na perfomance nzuri kulinganisha na maono ya NHC.

Ni kiitazama Tanzania naona imesimama, naona hakuna maono yoyote, ipo ili mradi tu iende na tujue kuna Taifa la Tanzania. Siku hizi tunavijana wengi, wanaujuzi katika masuala ya Real estates na niwabunifu. Serikali inawaweka pembeni, inampa mtu aendelee kuwa katika shirika hadi atafikisha miaka 20 ktk shirika, lkn hakuna jipya zaidi ya upigaji na kutumia mamillioni ya fedha kujitangaza.
 
Ni aibu kwamba nchi ambayo tuliaminishwa kwamba watu fulani ni wezi ni watendaji wabovu sasa wanarudishwa kwenye nafasi zao, utadhani hakuna kilichofanyika.

Yawezekana kweli walionewa, lakini iweje Rais wa nchi awarudishe kwenye nafasi zile zile bila maelezo kwa wananchi? Rais Samia ana matatizo kichwani.

Mchechu alisifika sana kwa ubadhirifu, sasa anarudi NHC kwa nafasi ile ile. Huu ni uopngozi au uhuni uliokithiri? Je, haya ndo matokeo ya urafiki na Kikwete au ni sababu gani ya ziada?

Rais Samia na Mzee Kikwete au watu wa Kikwete wana urafiki gani wa ziada? Hawa watu wana sifa zipi ambazo wa-TZ wengine hawana? Yaani wananchi hatuna thamani kiasi hiki kwa viongozi wetu!

Wabunge wengi ni wa ccm na walipewa ubunge na Magufuli, acha watawabana hawa wezi wanaorejeshwa kwenye mfumo.
 
Ukweli Nehemia, Dau na Dr Kimeo walichangamsha sana mashirika ya umma kwa uwekezaji mkubwa. NHC ilikuwa ni kama limekufa, tukaanza kuona miradi mipya kipindi cha Nehemia.

Toka Dr. Dau aondoke mifuko ya hifadhi ya jamii haionekani. Imelundikwa na malalamiko na ukata.

Dr Kimei nae toka aondoke crdb ni kama imesinzia.

images.jpg

Screenshot_20220314-204945.png

images-1.jpg

FB_IMG_1646675202748.jpg
 
Ubaya/uzuri wa nchi hii ni kwamba ukishaingia kwenye system na ukajua kula na wenzako basi mpaka utafiamo; na ulaji huo utaendelea kwako na vizazi vyako vyote. Ndo maana tutaendelea kusikia majina ya akina Makamba na Kikwete hata vizazi 50 vijavyo.

Nchi ya ajabu sana hii. Utafikiri hakuna watu wengine wenye uwezo wa kufanya hizo kazi![emoji706][emoji706][emoji706]
 
Ni aibu kwamba nchi ambayo tuliaminishwa kwamba watu fulani ni wezi ni watendaji wabovu sasa wanarudishwa kwenye nafasi zao, utadhani hakuna kilichofanyika.

Yawezekana kweli walionewa, lakini iweje Rais wa nchi awarudishe kwenye nafasi zile zile bila maelezo kwa wananchi? Rais Samia ana matatizo kichwani.

Mchechu alisifika sana kwa ubadhirifu, sasa anarudi NHC kwa nafasi ile ile. Huu ni uopngozi au uhuni uliokithiri? Je, haya ndo matokeo ya urafiki na Kikwete au ni sababu gani ya ziada?

Rais Samia na Mzee Kikwete au watu wa Kikwete wana urafiki gani wa ziada? Hawa watu wana sifa zipi ambazo wa-TZ wengine hawana? Yaani wananchi hatuna thamani kiasi hiki kwa viongozi wetu!
uliaminishwa wezi una ushaidi ww endelea kupigwa na jua acha wenzako wale mema ya nchi
 
Kwa hiyo serikali sasa itaenda kuweka garantii ili NHC wakope mabilioni ya pesa kwenye mabenki wajenge apartments ambazo watamuuzia mtanzania myonge kwa milioni 200, na kwa kuwa mnyonge hajawahi hata kuota kumiliki hiyo pesa basi hizo apartments zinabaki kuwa makazi ya popo na kupigwa vumbi daily......huyo ndo mama anaupiga mwingi bhana.
 
Mkuu huelewi nini Sasa wakati mchechu anaenda kuwaandalia makazi wamasai wa ngoro ngoro Ili tuuze vizuri ile crater KWA waarabu!!?
So painful, but here comes a day which is nigh, be warned! Sauti iliyonyikani...Mjumne hauwawi, kikombe cha hasira ya Mungu kinajazwa kwa haraka sana
 
Kushindaniwa tena kwa uwazi kabisa...
Na hata kama ni lazima uteuzi kuwepo na vetting authority ambayo itawahoji na kujiridhisha!
Anachokifanya Rais wa Tanzania ukii narrow it down to a family level ni sawa kabisa na mfume dume! Mtu mmoja anajua kila kitu na hakoseagi!!
SI KWELI! SI SAWA! SI SAHIHI!!
Tatizo wengi wanafikiria kwa matumbo, masikio na macho!!
Duuh!
 
Kweli ubinadamu kazi, juzi juzi kuna thread iliandikwa humu mnamtaka Nehemia arudi kwasababu shirika limedorola leo huyu anahoji kwanini ameteuliwa.Hakika Nyerere alisema kweli ukisikiliza kila makelele kiongozi haufikii malengo.
 
Ubaya/uzuri wa nchi hii ni kwamba ukishaingia kwenye system na ukajua kula na wenzako basi mpaka utafiamo; na ulaji huo utaendelea kwako na vizazi vyako vyote. Ndo maana tutaendelea kusikia majina ya akina Makamba na Kikwete hata vizazi 50 vijavyo.

Nchi ya ajabu sana hii. Utafikiri hakuna watu wengine wenye uwezo wa kufanya hizo kazi![emoji706][emoji706][emoji706]
"But they never knew JPM was coming" imebidi nim nukuu Chakwari...Maisha yanaenda kwa speed sana...Dunia hii huwa inazunguka sijui kwanini sijakata tamaa ki vile!
 
Ninavyojua hawa wapigaji walikuwa na network, sasa ni kama Magufuli alikuja kukata ile network ila amekuja huyu naona anaunganisha tena network.

Niandike tu kwa kifupi; Katiba Mpya (Rasimu ya Warioba) ndio suluhisho la kudumu.
Mkuu they know katiba mpya itakuwa mwiba that's why hawataki kuruhusu hiyo kitu iandikwe.

As they ssaying "katiba mpya siyo ajenda yangu au isubiri kwanza"
 
Back
Top Bottom