Ebu niambie mbali na Dar kulikojengwa maghorofa ya mchongo kwa matajiri tu, achana na yale yaliyojengwa Magomeni enzi ya Magufuli. Ni mkoa gani mwingine ulionufaika na ujenzi wa majengo ya kisasa? Ni wapi wananchi wa kawaida walinufaika na NHC chini ya uongozi wa Nehemia?
Sitaki kuongelea mamilioni ya fedha aliyokuwa anajilipa, na mashule alojenga, majumba anayomiliki, ambayo kabla ya kuwa meneja hakuwa navyo. Sitaki kuongelea alivyokuwa anamwaga fedha mamillioni. Ilikuwa bahati yake. Sitaki kuwa na wivu nae.
Mie nakumbuka NHC ya zamani ilijenga nyumba Tanzania nzima. Tena wengi waliofaidika ni watu wa chini. Mashirika kama haya nchi nyingine yamekuwa na REAL ESTATES kubwa na kuendezesha miji.
Siyo miaka ya Nehemia na vile vigorofa vya Morocco, basi tukaona amefanya kazi, na kuwa na kipindi. Nimetembelea Ethiopia, shirika la nyumba, limejenga majengo ya ghorofa nchi zima na nimazuri. Na bei nafuu sana nyumba zao. nchi inajengeka utazani Singapore.
NHC haijapata mtu alonavision ya kuwasaidia watanzania. NHC ilitakiwa ibadili madhari ya miji mingi Tanzania, si kuishia Dar es Salaam kujenga vigorofa viwili wanatumia hela nyingi kupoteza muda ati kipindi cha Nyumba! Ha ha ha!
Nehemia, hana tena jipya, kama miaka alotumia, hakufanya cha maana anaporejeshwa sasa atafanya nini? Kikubwa ni madili kujenga maghorofa machache Dar na kuwapa alionao michongo, wamiliki, nao wapangishe kwa matajiri.
Mfano pale mwanza milimani, Dar es Salaam maeneo ya Manzese, Mburahati na kadhalika, haya ni maeneo ambayo NHC ingeingia ubia na wananchi na kujenga majumba au maghorofa ya makazi, kisha wananchi hawa kupangishwa na baadae kuuziwa.
Hata vijijini, NHC ingekuwa na maono kusaidia wananchi wa vijijini kuwajengea makazi bora kwa makubaliano maalum, na kuondoa vijumba vya ajabu na vile vya nyasi. Nampongeza Rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Karume, alikuwa na akili sana huyu, vijijini au shamba kama wanavyoita wa Zanzibar alijenga maghorofa akaweka umeme na maji, mbali na yale maghorofa ya Michenzani, naongelea ya vijijini kama Bambi na kadhalika. Alitaka wananchi wa hali ya nchini wapate makazi safi. Hadi leo hakuna Rais alofanya kazi kama ya Marehemu Karume.
Nehemia hana jipya tena. Hivi nchi yetu haina watu wengine? Hivi hawa ndo tu walio na brain kuliko watanzania wengine? Mie nadhani Nehemia angepewa nafasi nyingine za uteuzi lakini si kumrudisha palepale ambapo kwa kuangalia hakuwa na perfomance nzuri kulinganisha na maono ya NHC.
Ni kiitazama Tanzania naona imesimama, naona hakuna maono yoyote, ipo ili mradi tu iende na tujue kuna Taifa la Tanzania. Siku hizi tunavijana wengi, wanaujuzi katika masuala ya Real estates na niwabunifu. Serikali inawaweka pembeni, inampa mtu aendelee kuwa katika shirika hadi atafikisha miaka 20 ktk shirika, lkn hakuna jipya zaidi ya upigaji na kutumia mamillioni ya fedha kujitangaza.