Uteuzi wa Nehemia Mchechu: Tunamchekea Rais Samia, lakini hapa ameonyesha udhaifu mkubwa

Walipo badilisha na kumwondoa Nehemia, si unaona shirika lilikuwa kama halina boss? Kwahiyo utaona mpya hakuwa na jipya

Mchechu na timu yake ya akina maagi waliamsha sana nhc. Africa na hasa tanzania hakuna ambaye sio mwizi, ila uzur wake (nehemia) kazi na tija inaonekana.

i hope sasa nehemia atajifunza na kuwa mzalendo. Kudos mama
Wanajenga nyumba kama Kota za jeshi wanatakiwa wajenge nyumba zitofautiane ramani ili mnunuzi ajichagulie anayopenda kwanini mijumba yao mibaya tofauti na nyumba zinazo jengwa na watu binafsi
 
Watu wale wale, miaka nenda rudi utafikiri hii nchi Mchechu, Mafuru, Makamba, Nape nk ndio wasomi pekee na wenye akili pekee.

Huyu mama sijui hata anawaza nini
Nahodha nae kapewa ubunge wa mezani,pamoja na kuwa waziri kiongozi na kustaafu, nchi hii ina wenyewe na utasikia kawa waziri,akina Mbarawa nao wamo
 
Watu wale wale, miaka nenda rudi utafikiri hii nchi Mchechu, Mafuru, Makamba, Nape nk ndio wasomi pekee na wenye akili pekee.

Huyu mama sijui hata anawaza nini
Nimeimiss sana ile safu ya maswali magumu ya enzi zileeeeeee . . .
Hii kitu isingepita bila wao kuiblast kweli kweli
 
Ni aibu kwamba nchi ambayo tuliaminishwa kwamba watu fulani ni wezi ni watendaji wabovu sasa wanarudishwa kwenye nafasi zao, utadhani hakuna kilichofanyika.

Yawezekana kweli walionewa, lakini iweje Rais wa nchi awarudishe kwenye nafasi zile zile bila maelezo kwa wananchi? Hii haina maana.

Mchechu alisifika sana kwa ubadhirifu, sasa anarudi NHC kwa nafasi ile ile. Huu ni uongozi au uhuni uliokithiri? Je, haya ndo matokeo ya urafiki na Kikwete au ni sababu gani ya ziada?

Rais Samia na Mzee Kikwete au watu wa Kikwete wana urafiki gani wa ziada? Hawa watu wana sifa zipi ambazo Watanzania wengine hawana? Yaani wananchi hatuna thamani kiasi hiki kwa viongozi wetu!
Mchechi ni bilionea.mbadhirifu kuliko Makonda.
Salary yake ni 40 milioni
 
Ni aibu kwamba nchi ambayo tuliaminishwa kwamba watu fulani ni wezi ni watendaji wabovu sasa wanarudishwa kwenye nafasi zao, utadhani hakuna kilichofanyika.

Yawezekana kweli walionewa, lakini iweje Rais wa nchi awarudishe kwenye nafasi zile zile bila maelezo kwa wananchi? Hii haina maana.

Mchechu alisifika sana kwa ubadhirifu, sasa anarudi NHC kwa nafasi ile ile. Huu ni uongozi au uhuni uliokithiri? Je, haya ndo matokeo ya urafiki na Kikwete au ni sababu gani ya ziada?

Rais Samia na Mzee Kikwete au watu wa Kikwete wana urafiki gani wa ziada? Hawa watu wana sifa zipi ambazo Watanzania wengine hawana? Yaani wananchi hatuna thamani kiasi hiki kwa viongozi wetu!
Wewe peke yako ndo uliaminishwa na kudanganyika. Unataka kusema kila alichosema/kufanya magu alkua malaika kwamba Rais aliefuata baada ya yeye lazma afanye ya magu? Hebu tulizans mwache SSH apange safu yake
 
Patazibwa panapovuja! Usiwe na wasiwasi, yupo makini sana usimchukule poa!
 
Wanatuona kuku wa nyama tu. Unakamata unachinja unavyotaka. Madhambi ya Nehemia yalitangazwa hadharani na Rais TBC pembeni akiwapo Makamu wa Rais ambaye ni Rais kwa sasa. Hawa CCM acha tu!!
Alimpeleka mahakama gani kama alikuwa na ushahidi?

Magufuli alikuwa muhuni na mzandiki aliyejaa chuki huku akijificha kwenye kivuli cha ucha Mungu
 
Ebu niambie mbali na Dar kulikojengwa maghorofa ya mchongo kwa matajiri tu, achana na yale yaliyojengwa Magomeni enzi ya Magufuli. Ni mkoa gani mwingine ulionufaika na ujenzi wa majengo ya kisasa? Ni wapi wananchi wa kawaida walinufaika na NHC chini ya uongozi wa Nehemia?
Sitaki kuongelea mamilioni ya fedha aliyokuwa anajilipa, na mashule alojenga, majumba anayomiliki, ambayo kabla ya kuwa meneja hakuwa navyo. Sitaki kuongelea alivyokuwa anamwaga fedha mamillioni. Ilikuwa bahati yake. Sitaki kuwa na wivu nae.
Mie nakumbuka NHC ya zamani ilijenga nyumba Tanzania nzima. Tena wengi waliofaidika ni watu wa chini. Mashirika kama haya nchi nyingine yamekuwa na REAL ESTATES kubwa na kuendezesha miji.

Siyo miaka ya Nehemia na vile vigorofa vya Morocco, basi tukaona amefanya kazi, na kuwa na kipindi. Nimetembelea Ethiopia, shirika la nyumba, limejenga majengo ya ghorofa nchi zima na nimazuri. Na bei nafuu sana nyumba zao. nchi inajengeka utazani Singapore.
NHC haijapata mtu alonavision ya kuwasaidia watanzania. NHC ilitakiwa ibadili madhari ya miji mingi Tanzania, si kuishia Dar es Salaam kujenga vigorofa viwili wanatumia hela nyingi kupoteza muda ati kipindi cha Nyumba! Ha ha ha!

Nehemia, hana tena jipya, kama miaka alotumia, hakufanya cha maana anaporejeshwa sasa atafanya nini? Kikubwa ni madili kujenga maghorofa machache Dar na kuwapa alionao michongo, wamiliki, nao wapangishe kwa matajiri.

Mfano pale mwanza milimani, Dar es Salaam maeneo ya Manzese, Mburahati na kadhalika, haya ni maeneo ambayo NHC ingeingia ubia na wananchi na kujenga majumba au maghorofa ya makazi, kisha wananchi hawa kupangishwa na baadae kuuziwa.

Hata vijijini, NHC ingekuwa na maono kusaidia wananchi wa vijijini kuwajengea makazi bora kwa makubaliano maalum, na kuondoa vijumba vya ajabu na vile vya nyasi. Nampongeza Rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Karume, alikuwa na akili sana huyu, vijijini au shamba kama wanavyoita wa Zanzibar alijenga maghorofa akaweka umeme na maji, mbali na yale maghorofa ya Michenzani, naongelea ya vijijini kama Bambi na kadhalika. Alitaka wananchi wa hali ya nchini wapate makazi safi. Hadi leo hakuna Rais alofanya kazi kama ya Marehemu Karume.

Nehemia hana jipya tena. Hivi nchi yetu haina watu wengine? Hivi hawa ndo tu walio na brain kuliko watanzania wengine? Mie nadhani Nehemia angepewa nafasi nyingine za uteuzi lakini si kumrudisha palepale ambapo kwa kuangalia hakuwa na perfomance nzuri kulinganisha na maono ya NHC.

Ni kiitazama Tanzania naona imesimama, naona hakuna maono yoyote, ipo ili mradi tu iende na tujue kuna Taifa la Tanzania. Siku hizi tunavijana wengi, wanaujuzi katika masuala ya Real estates na niwabunifu. Serikali inawaweka pembeni, inampa mtu aendelee kuwa katika shirika hadi atafikisha miaka 20 ktk shirika, lkn hakuna jipya zaidi ya upigaji na kutumia mamillioni ya fedha kujitangaza.
Umemaliza mawazo yangu mkuu
 
Wabunge wengi ni wa ccm na walipewa ubunge na Magufuli, acha watawabana hawa wezi wanaorejeshwa kwenye mfumo.
Hakuna ushahidi wa wazi ulionesha kuwa Yehemia Mchechu alikuwa mwizi aliondolewa pale NHC kisiasa tu katika Wakurugenzi waliohudumu NHC hakuna mtu aliye fanya mambo makubwa kama Mchechu alifanya reformation kubwa sana katika shirika letu la Nyumba
Hivyo mimi kwangu ni uteuzi mzuri na atamsaidia sana Rais kulifanya shirika liwe bora zaidi
Kiuhalisia lazima shirika liwe na category tatu
Kwanza kuweza kuhudumia wananchi wa chini ambao watakuwa wanufaika kuweza kupata nyumba kwa rahisi

Pili wananchi wenyewe kipato cha kati (Middle Class) ambao hawa wataweza ku afford nyumba za kisasa

Tatu Tabaka la watu wenye uwezo mkumbwa kiuchumi ambayo hawa watakuwa na uwezo wa kupangisha na kununua Apartment za kisasa
 
View attachment 2150611
Hongera kwa kurudishwa nafasi yako , lakini nakushauri sasa nenda katumie nafasi vizuri kampuni zako tunajua ndio zilizokua zinapeewa tender zote hapo NHC jitahidi hiyo keki ule na watanzania wenzako. Sio lazima watu tuseme kila kitu lakini Mwenda zake aliona kitu akakutoa hapo rekebisha hicho kitu na unakijua vizuri, shirika likatoe huduma kwa haki na usawa kwa kulingana maisha halisi ya mtanzania
Mwendazake ndo nani? Huyo muhuni aliyeongozwa na chuki ndo unamsema hapa?
 
Ni aibu kwamba nchi ambayo tuliaminishwa kwamba watu fulani ni wezi ni watendaji wabovu sasa wanarudishwa kwenye nafasi zao, utadhani hakuna kilichofanyika.

Yawezekana kweli walionewa, lakini iweje Rais wa nchi awarudishe kwenye nafasi zile zile bila maelezo kwa wananchi? Hii haina maana.

Mchechu alisifika sana kwa ubadhirifu, sasa anarudi NHC kwa nafasi ile ile. Huu ni uongozi au uhuni uliokithiri? Je, haya ndo matokeo ya urafiki na Kikwete au ni sababu gani ya ziada?

Rais Samia na Mzee Kikwete au watu wa Kikwete wana urafiki gani wa ziada? Hawa watu wana sifa zipi ambazo Watanzania wengine hawana? Yaani wananchi hatuna thamani kiasi hiki kwa viongozi wetu!
Jk is doing his things Chief Hngy is not to blame!
 
Ebu niambie mbali na Dar kulikojengwa maghorofa ya mchongo kwa matajiri tu, achana na yale yaliyojengwa Magomeni enzi ya Magufuli. Ni mkoa gani mwingine ulionufaika na ujenzi wa majengo ya kisasa? Ni wapi wananchi wa kawaida walinufaika na NHC chini ya uongozi wa Nehemia?
Sitaki kuongelea mamilioni ya fedha aliyokuwa anajilipa, na mashule alojenga, majumba anayomiliki, ambayo kabla ya kuwa meneja hakuwa navyo. Sitaki kuongelea alivyokuwa anamwaga fedha mamillioni. Ilikuwa bahati yake. Sitaki kuwa na wivu nae.
Mie nakumbuka NHC ya zamani ilijenga nyumba Tanzania nzima. Tena wengi waliofaidika ni watu wa chini. Mashirika kama haya nchi nyingine yamekuwa na REAL ESTATES kubwa na kuendezesha miji.

Siyo miaka ya Nehemia na vile vigorofa vya Morocco, basi tukaona amefanya kazi, na kuwa na kipindi. Nimetembelea Ethiopia, shirika la nyumba, limejenga majengo ya ghorofa nchi zima na nimazuri. Na bei nafuu sana nyumba zao. nchi inajengeka utazani Singapore.
NHC haijapata mtu alonavision ya kuwasaidia watanzania. NHC ilitakiwa ibadili madhari ya miji mingi Tanzania, si kuishia Dar es Salaam kujenga vigorofa viwili wanatumia hela nyingi kupoteza muda ati kipindi cha Nyumba! Ha ha ha!

Nehemia, hana tena jipya, kama miaka alotumia, hakufanya cha maana anaporejeshwa sasa atafanya nini? Kikubwa ni madili kujenga maghorofa machache Dar na kuwapa alionao michongo, wamiliki, nao wapangishe kwa matajiri.

Mfano pale mwanza milimani, Dar es Salaam maeneo ya Manzese, Mburahati na kadhalika, haya ni maeneo ambayo NHC ingeingia ubia na wananchi na kujenga majumba au maghorofa ya makazi, kisha wananchi hawa kupangishwa na baadae kuuziwa.

Hata vijijini, NHC ingekuwa na maono kusaidia wananchi wa vijijini kuwajengea makazi bora kwa makubaliano maalum, na kuondoa vijumba vya ajabu na vile vya nyasi. Nampongeza Rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Karume, alikuwa na akili sana huyu, vijijini au shamba kama wanavyoita wa Zanzibar alijenga maghorofa akaweka umeme na maji, mbali na yale maghorofa ya Michenzani, naongelea ya vijijini kama Bambi na kadhalika. Alitaka wananchi wa hali ya nchini wapate makazi safi. Hadi leo hakuna Rais alofanya kazi kama ya Marehemu Karume.

Nehemia hana jipya tena. Hivi nchi yetu haina watu wengine? Hivi hawa ndo tu walio na brain kuliko watanzania wengine? Mie nadhani Nehemia angepewa nafasi nyingine za uteuzi lakini si kumrudisha palepale ambapo kwa kuangalia hakuwa na perfomance nzuri kulinganisha na maono ya NHC.

Ni kiitazama Tanzania naona imesimama, naona hakuna maono yoyote, ipo ili mradi tu iende na tujue kuna Taifa la Tanzania. Siku hizi tunavijana wengi, wanaujuzi katika masuala ya Real estates na niwabunifu. Serikali inawaweka pembeni, inampa mtu aendelee kuwa katika shirika hadi atafikisha miaka 20 ktk shirika, lkn hakuna jipya zaidi ya upigaji na kutumia mamillioni ya fedha kujitangaza.
Alijenga Singida, Arusha, Bukoba na Katavi

Alivyoondoka Msechu, waliobaki wamejenga wapi?
 
Walivyoondolewa ulipewa sababu? Uliona wakipelekwa Mahakamani?

Kwa nini useme Rais ana udhaifu?

Kwa taarifa yako Samia haongozwi na chuki
Statement zako 2 za kwanza zinamantiki kubwa sana kuna mengi ya kufikirisha
 
Back
Top Bottom