Uteuzi wa Nehemia Mchechu: Tunamchekea Rais Samia, lakini hapa ameonyesha udhaifu mkubwa

Uteuzi wa Nehemia Mchechu: Tunamchekea Rais Samia, lakini hapa ameonyesha udhaifu mkubwa

Watu wale wale, miaka nenda rudi utafikiri hii nchi Mchechu, Mafuru, Makamba, Nape nk ndio wasomi pekee na wenye akili pekee.

Huyu mama sijui hata anawaza nini
Inabidi fulsa ziwe kwa wote wajameni nimewahi sema hili suala wakati flani watu wakaja juu!

Wasomi wa maana nchi hii wako wengi inakuwaje leo hii wanaopewa nafasi wawe wale wale wa 2015 kurudi nyuma huko?
 
Mliaminishwa..

Neno sahihi kabisa. Haikuwa hivyo ila zilikuwa ni chuki kali zilizojaa husda majungu na visasi.

Tulieni hivyohivyo Mama aiponye nchi.

Mama songa mbele. Tuko nyuma yako.
Aiponye wapi kaka??? Kwani hii nchi wasomi ni hao hao tu????
 
Ni aibu kwamba nchi ambayo tuliaminishwa kwamba watu fulani ni wezi ni watendaji wabovu sasa wanarudishwa kwenye nafasi zao, utadhani hakuna kilichofanyika...
Kikwete kahusikaje hapo? Kwa hilo tu tayari nakuona we tahira unasukumwa na husda juu ya mzee kikwete
 
Ninavyojua hawa wapigaji walikuwa na network, sasa ni kama Magufuli alikuja kukata ile network ila amekuja huyu naona anaunganisha tena network.

Niandike tu kwa kifupi; Katiba Mpya (Rasimu ya Warioba) ndio suluhisho la kudumu.
Ile katiba nayo zuga, ujinga mtupu
 
Kilichomtoa msechu ni mshahara mkubwa 35m per month, hii magu akikubaliki, mbona alisema!

Pia vikampuni vyake vilivyofanya kazi nhc. Ila kazi ilikuwa inaonekana, sasa mama amemrudisha aendelee ni program zake!
 
Yawezekana kweli walionewa, lakini iweje Rais wa nchi awarudishe kwenye nafasi zile zile bila maelezo kwa wananchi? Hii haina maana.
Hapa kuna udhaifu mkubwa ndani ya utendaji wa serikali ya ccm, huyu aliondolewa kwani alikuwa na kampuni zake zilizokuwa zinafanya kazi na NHC hivyo kuleta mgongano wa kimaslahi! something wrong ktk 'kada' za uteuzi.
 
Tukubaliane Nehemia anaweza! Ana uwezo mkubwa wa kuwaza nje ya kibox akaja na solutions.
Kipindi kile labda hakuwa kwenye boat ya mtawala
Tuwekee hapa records za utendaji wake ili twende sawa. Alifanya lipi na lipi linaloonekana.

Utajilipaje mshahara wa 20m, housing allowance, gari la office nk kwa shirika linalotegemea mikopo ili liweze kupiga hatua? Una lipi la ajabu katika utendaji?
 
Rais Samia anatengeneza Serikali ya kistaarabu. Anajaribu kuondoa utawala primitive wa Marehemu Magufuli.

Muda si mrefu, mambo yataanza kubadilika taratibu. Marehemu aliua uchumi, aliua demokrasia, aliua ustaarabu, aliua mifumo ya utawala. Kwa kweli uongozi wa marehemu, kama alivyosema yule gavana wa Kenya, ulikuwa ni aibu kwa Watanzania na Afrika nzima.

Tuliombee Taifa letu, ili taifa lisijekupatwa na laana kama ile ya wakati wa utawala wa Marehemu, utawala ulioishia kuteka watu, kupoteza watu, kuua watu, kubambikia kesi watu, kuharibu mahusiano ya kimataifa, kushusha ukuuaji wa utalii toka 15% mpaka 3.6%, kushusha ukiaji wa uwekezaji toka 28% mpaka 4%, kuangusha thamani ya mauzo ya nje ya mazao ya kilimo kwa 50%.

Kwa kweli uongozi wa marehemu ulikuwa ni laana kwa Taifa, hasara kwa Watanzania. Tuzidi kumwombea maana hatujui ndani ya roho yake kulikuwa na nini hata mtu akapenda uovu dhidi ya binadamu wenzake kwa kiasi kile.
 
Ni aibu kwamba nchi ambayo tuliaminishwa kwamba watu fulani ni wezi ni watendaji wabovu sasa wanarudishwa kwenye nafasi zao, utadhani hakuna kilichofanyika...
Naona dr maulidi banyani anaiacha salary ya tshs 13,000,000/= kwa mwezi na anarudi ardhi university kwenye lectures za tsh 3,400,000/= kwa mwezi.Dah maisha ya siasa ni kama gwaride.

Ukisikia nyuma geuka hapo ndo pale wa mwisho anaenda kuwa wa kwanza.Shubamiiiiiitiiiiiiiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom