Uteuzi wa Nehemia Mchechu: Tunamchekea Rais Samia, lakini hapa ameonyesha udhaifu mkubwa

Uteuzi wa Nehemia Mchechu: Tunamchekea Rais Samia, lakini hapa ameonyesha udhaifu mkubwa

Tuwekee hapa records za utendaji wake ili twende sawa. Alifanya lipi na lipi linaloonekana.

Utajilipaje mshahara wa 20m, housing allowance, gari la office nk kwa shirika linalotegemea mikopo ili liweze kupiga hatua? Una lipi la ajabu katika utendaji?
Alijipangia? Ofisi haina muundo wa scales za mishahara na posho? Ofs haina board inayoamua hayo?

Hakuna ofs ya serikali inayojiendesha kiholela hivyo.Lazima iwe na necessary instruments including hizo zinazoeleza maslahi ya mtumishi wa kwanza hadi wa mwisho.

Kwamba amejipangia seriously haiingii akilini, Bodi ilikuwa wapi?

Anaanzaje tu atoke huko CBA aje ajipe lishahara na marupurupu!!
 
Watu wale wale, miaka nenda rudi utafikiri hii nchi Mchechu, Mafuru, Makamba, Nape nk ndio wasomi pekee na wenye akili pekee.

Huyu mama sijui hata anawaza nini
Yupo kwenye mapambano makali na Maiti.

Na anarusha ngumi kwelikweli.
 
Rais Samia anatengeneza Serikali ya kistaarabu. Anajaribu kuondoa utawala primitive wa Marehemu Magufuli.

Muda si mrefu, mambo yataanza kubadilika taratibu. Marehemu aliua uchumi, aliua demokrasia, aliua ustaarabu, aliua mifumo ya utawala. Kwa kweli uongozi wa marehemu, kama alivyosema yule gavana wa Kenya, ulikuwa ni aibu kwa Watanzania na Afrika nzima.

Tuliombee Taifa letu, ili taifa lisijekupatwa na laana kama ile ya wakati wa utawala wa Marehemu, utawala ulioishia kuteka watu, kupoteza watu, kuua watu, kubambikia kesi watu, kuharibu mahusiano ya kimataifa, kushusha ukuuaji wa utalii toka 15% mpaka 3.6%, kushusha ukiaji wa uwekezaji toka 28% mpaka 4%, kuangusha thamani ya mauzo ya nje ya mazao ya kilimo kwa 50%. Kwa kweli uongozi wa marehemu ulikuwa ni laana kwa Taifa, hasara kwa Watanzania. Tuzidi kumwombea maana hatujui ndani ya roho yake kulikuwa na nini hata mtu akapenda uovu dhidi ya binadamu wenzake kwa kiasi kile.
mtu aliyefanya aibu zote HIZO ikiwa ni pamoja mauaji ya vifaranga visivyo na hatia. Nashauri kumbukizi yake ya mwaka mmoja iwe na slogan ya UKOMBOZI KUTOKA KWENYE AIBU
 
Kumbe mnajua leo kuwa Katiba ni Muhimu?
Ninavyojua hawa wapigaji walikuwa na network, sasa ni kama Magufuli alikuja kukata ile network ila amekuja huyu naona anaunganisha tena network.

Niandike tu kwa kifupi; Katiba Mpya (Rasimu ya Warioba) ndio suluhisho la kudumu.
 
Huyu aliyetoka amefanya nini?
Ebu niambie mbali na Dar kulikojengwa maghorofa ya mchongo kwa matajiri tu, achana na yale yaliyojengwa Magomeni enzi ya Magufuli. Ni mkoa gani mwingine ulionufaika na ujenzi wa majengo ya kisasa? Ni wapi wananchi wa kawaida walinufaika na NHC chini ya uongozi wa Nehemia?
Sitaki kuongelea mamilioni ya fedha aliyokuwa anajilipa, na mashule alojenga, majumba anayomiliki, ambayo kabla ya kuwa meneja hakuwa navyo. Sitaki kuongelea alivyokuwa anamwaga fedha mamillioni. Ilikuwa bahati yake. Sitaki kuwa na wivu nae.
Mie nakumbuka NHC ya zamani ilijenga nyumba Tanzania nzima. Tena wengi waliofaidika ni watu wa chini. Mashirika kama haya nchi nyingine yamekuwa na REAL ESTATES kubwa na kuendezesha miji.

Siyo miaka ya Nehemia na vile vigorofa vya Morocco, basi tukaona amefanya kazi, na kuwa na kipindi. Nimetembelea Ethiopia, shirika la nyumba, limejenga majengo ya ghorofa nchi zima na nimazuri. Na bei nafuu sana nyumba zao. nchi inajengeka utazani Singapore.
NHC haijapata mtu alonavision ya kuwasaidia watanzania. NHC ilitakiwa ibadili madhari ya miji mingi Tanzania, si kuishia Dar es Salaam kujenga vigorofa viwili wanatumia hela nyingi kupoteza muda ati kipindi cha Nyumba! Ha ha ha!

Nehemia, hana tena jipya, kama miaka alotumia, hakufanya cha maana anaporejeshwa sasa atafanya nini? Kikubwa ni madili kujenga maghorofa machache Dar na kuwapa alionao michongo, wamiliki, nao wapangishe kwa matajiri.

Mfano pale mwanza milimani, Dar es Salaam maeneo ya Manzese, Mburahati na kadhalika, haya ni maeneo ambayo NHC ingeingia ubia na wananchi na kujenga majumba au maghorofa ya makazi, kisha wananchi hawa kupangishwa na baadae kuuziwa.

Hata vijijini, NHC ingekuwa na maono kusaidia wananchi wa vijijini kuwajengea makazi bora kwa makubaliano maalum, na kuondoa vijumba vya ajabu na vile vya nyasi. Nampongeza Rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Karume, alikuwa na akili sana huyu, vijijini au shamba kama wanavyoita wa Zanzibar alijenga maghorofa akaweka umeme na maji, mbali na yale maghorofa ya Michenzani, naongelea ya vijijini kama Bambi na kadhalika. Alitaka wananchi wa hali ya nchini wapate makazi safi. Hadi leo hakuna Rais alofanya kazi kama ya Marehemu Karume.

Nehemia hana jipya tena. Hivi nchi yetu haina watu wengine? Hivi hawa ndo tu walio na brain kuliko watanzania wengine? Mie nadhani Nehemia angepewa nafasi nyingine za uteuzi lakini si kumrudisha palepale ambapo kwa kuangalia hakuwa na perfomance nzuri kulinganisha na maono ya NHC.

Ni kiitazama Tanzania naona imesimama, naona hakuna maono yoyote, ipo ili mradi tu iende na tujue kuna Taifa la Tanzania. Siku hizi tunavijana wengi, wanaujuzi katika masuala ya Real estates na niwabunifu. Serikali inawaweka pembeni, inampa mtu aendelee kuwa katika shirika hadi atafikisha miaka 20 ktk shirika, lkn hakuna jipya zaidi ya upigaji na kutumia mamillioni ya fedha kujitangaza.
 
Ni dharau na matusi makubwa kwa wenye akili na uelewa but nafikiri kwa watanzania hii ni kawaida kwao..teuzi zenye lengo la kulinda maslahi ya kikundi kidogo cha watu meanwhile mamia wanateseka..hao wote waliorudishwa hawana extraordinary credentials ambazo watu wengine hawana..walichonacho ni sifa ya wizi na ufisadi ambazo ni sifa kuu ya uteuzi wa utawala huu..but ni tanzania unategemea nini..acha inyeshe.......
 
Ni aibu kwamba nchi ambayo tuliaminishwa kwamba watu fulani ni wezi ni watendaji wabovu sasa wanarudishwa kwenye nafasi zao, utadhani hakuna kilichofanyika.

Yawezekana kweli walionewa, lakini iweje Rais wa nchi awarudishe kwenye nafasi zile zile bila maelezo kwa wananchi? Hii haina maana.

Mchechu alisifika sana kwa ubadhirifu, sasa anarudi NHC kwa nafasi ile ile. Huu ni uongozi au uhuni uliokithiri? Je, haya ndo matokeo ya urafiki na Kikwete au ni sababu gani ya ziada?

Rais Samia na Mzee Kikwete au watu wa Kikwete wana urafiki gani wa ziada? Hawa watu wana sifa zipi ambazo Watanzania wengine hawana? Yaani wananchi hatuna thamani kiasi hiki kwa viongozi wetu!

Mchechu aliondolewa kwa chuki tu za Mwendazake. Kama alikuwa mwizi au fisadi mbona hakufikishwa mahakamani?
 
Ninavyojua hawa wapigaji walikuwa na network, sasa ni kama Magufuli alikuja kukata ile network ila amekuja huyu naona anaunganisha tena network.

Niandike tu kwa kifupi; Katiba Mpya (Rasimu ya Warioba) ndio suluhisho la kudumu.
Jakaya alimtia mchechu marekani huko kuja kuendesha nhc kwa mtazamo mpya,aliwaleta wengi tu hivyo Kama mbarawa,mhongo nk...yule mwenye roho ya kimasikini/mbaya akaleta ghil a zake baada ya kushika hatamu
 
Ila kinachotengenezwa ni kibaya zaidi kuliko kinachotarajiwa.

TISS kaeni chini msaidieni mama.. na muwe na kumbukumbu.

Taifa linapotea hili
 
Tusimlaumu Mama Samia kumteua anayedhani atamsaidia kusukuma gurudumu la maendeleo - ni KATIBA yetu ndiyo inamruhusu kufanya hivyo.
 
Ni aibu kwamba nchi ambayo tuliaminishwa kwamba watu fulani ni wezi ni watendaji wabovu sasa wanarudishwa kwenye nafasi zao, utadhani hakuna kilichofanyika.

Yawezekana kweli walionewa, lakini iweje Rais wa nchi awarudishe kwenye nafasi zile zile bila maelezo kwa wananchi? Hii haina maana.

Mchechu alisifika sana kwa ubadhirifu, sasa anarudi NHC kwa nafasi ile ile. Huu ni uongozi au uhuni uliokithiri? Je, haya ndo matokeo ya urafiki na Kikwete au ni sababu gani ya ziada?

Rais Samia na Mzee Kikwete au watu wa Kikwete wana urafiki gani wa ziada? Hawa watu wana sifa zipi ambazo Watanzania wengine hawana? Yaani wananchi hatuna thamani kiasi hiki kwa viongozi wetu!
Alfanya ubadhirifu gani? Au ni yale yale maneno ya chuki? NHC ilipiga hatua sana kipindo chake. mi naona ana entrepreneurial spirit. Kilichomuondoa NHC kipindi cha jiwe ni mshahara wake tu ambao ulikuwa mkubwa sana. Sikubuki kusikia ubadhirifu alioufanya labda mtu anikumbushe!!!
 
Rais Samia anatengeneza Serikali ya kistaarabu. Anajaribu kuondoa utawala primitive wa Marehemu Magufuli.

Muda si mrefu, mambo yataanza kubadilika taratibu. Marehemu aliua uchumi, aliua demokrasia, aliua ustaarabu, aliua mifumo ya utawala. Kwa kweli uongozi wa marehemu, kama alivyosema yule gavana wa Kenya, ulikuwa ni aibu kwa Watanzania na Afrika nzima.

Tuliombee Taifa letu, ili taifa lisijekupatwa na laana kama ile ya wakati wa utawala wa Marehemu, utawala ulioishia kuteka watu, kupoteza watu, kuua watu, kubambikia kesi watu, kuharibu mahusiano ya kimataifa, kushusha ukuuaji wa utalii toka 15% mpaka 3.6%, kushusha ukiaji wa uwekezaji toka 28% mpaka 4%, kuangusha thamani ya mauzo ya nje ya mazao ya kilimo kwa 50%.

Kwa kweli uongozi wa marehemu ulikuwa ni laana kwa Taifa, hasara kwa Watanzania. Tuzidi kumwombea maana hatujui ndani ya roho yake kulikuwa na nini hata mtu akapenda uovu dhidi ya binadamu wenzake kwa kiasi kile.
Hakuna laana kubwa kwa taifa hili kupata wazazi waliotuletea watoto laana sampuli ya wewe Bams
 
Ni aibu kwamba nchi ambayo tuliaminishwa kwamba watu fulani ni wezi ni watendaji wabovu sasa wanarudishwa kwenye nafasi zao, utadhani hakuna kilichofanyika.

Yawezekana kweli walionewa, lakini iweje Rais wa nchi awarudishe kwenye nafasi zile zile bila maelezo kwa wananchi? Hii haina maana.

Mchechu alisifika sana kwa ubadhirifu, sasa anarudi NHC kwa nafasi ile ile. Huu ni uongozi au uhuni uliokithiri? Je, haya ndo matokeo ya urafiki na Kikwete au ni sababu gani ya ziada?

Rais Samia na Mzee Kikwete au watu wa Kikwete wana urafiki gani wa ziada? Hawa watu wana sifa zipi ambazo Watanzania wengine hawana? Yaani wananchi hatuna thamani kiasi hiki kwa viongozi wetu!
Ubadhirifu zaidi ya kujenga International airport Chato?
 
Chuki binafsi tu Hakuna mtu aliye fanya kazi nzuri kama Mchechu. Alilipaisha shirika . Litazame hali liliyonayo saiv. Tuache watu wafanya kazi haya mambo ya kuruka na vistory visivyo na mashiko zinasababisha kuokota watu wasio na ujuzi wowote.

Nehemia ni Mtu sahihi sana Muda utakupa Majibu mazuri.

Rais anafanya kazi nzuri sana.
 
Back
Top Bottom