Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya uliofanyika Juni 2021 umeshusha hadhi ya nafasi hiyo

Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya uliofanyika Juni 2021 umeshusha hadhi ya nafasi hiyo

Inasikitisha sana kuwa na nchi ambayo watu wake wanaamini uongozi ndio keki ya taifa na mtu akipewa cheo ameula

Ni kweli mkuu kuwa haki hiyo ya mtu kupewa cheo kuwa ni ulaji inasikitisha, lakini ndio uhalisia. Wafuatilie karibia wote waliopata hivyo vyeo, maisha yao yataboreka. Kumbuka kwa kupitia hiyo nafasi ya uDC, mtu atakuwa anapata 5m+@month, je ni nani kati ya hao walioteuliwa uDC walikuwa uwezo wa kupata 5m+@month?

Mbali ya huo mshahara, kuna mambo yao mengi yataenda kirahisi kama matibabu, atakuwa na gari la kuzungukia 24/7, connection za biashara za hapa na pale, rushwa nk. Na mwisho japo sio kwa umuhimu, anaweza kuwa mporaji kama alivyokuwa Makonda, Sabaya, Gambo nk na akapata ukwasi wa haraka. Usisahau atapata heshima ya kunyenyekewa, kitu ambacho wanasiasa hupenda sana.
 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ally Hassan Mwinyi Aliwahi kusema kuwa TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZI Akimaanisha Kila Anayejifunza KUNYOA Anajifunzia TANZANIA na ni baada ya Timu yetu ya TAIFA kufungwa na Kila Timu.Jana Tumesikia Wakuu wa Wilaya Wameteuliwa ,Wateuliwa husika ni Vijana na Walio wengi ni Wa Mitaani hawana Rekodi ya UTENDAJI au UONGOZI wowote.Una Mteuaje Mtu Asiye na Uzoefu au Hata ELIMU ya UONGOZI na Anaenda KUONGOZA na KUSIMAMIA Maendeleo Ya Wilaya yenye Wananchi zaidi ya Maelfu? Mkuu wa WILAYA ni Mwenyekiti wa KAMATI ya Ulinzi na USALAMA Mjukumu ambayo inahitaji Hekima na Busara .Leo Wanateuliwa WASANII kwenda Kuyasimamia Kweli TANZANIA ni KICHWA cha MWENDAWAZIM Nendeni WATEULIWA mkajifunze KUNYOA
 
Ulichoumia ni wale wafuasi wenu wa zamani kupewa vyeo hamna lingine.
Kwani wameanza leo kupewa vyeo? Wenye sababu ya kuumia ni wafia chama ambao wanaangalia nafasi zinachukuliwa na mamluki ambao juzi tu walikuwa wanawatukana. Mnajikaza tu lakini mnaumia.

Amandla...
 
Inasikitisha sana Tanzania sijui inaelekea wapi. DC ni nafasi nyeti ya kuunganisha watendaji na jamii inayowazunguka. Kusimamia mambo ya ulinzi na usalama. Hii ni nafasi ya waandamizi kutoka katika utumishi au chama, wakiwa wamejaa utu uzima na busara za kumwagika. Leo unaenda kuokoteza wasanii na watu mitandaoni.

Naona Tanzania inapoteza uelekeo kabisa. Hawa jamaa wanatupa kazi sana kuirudisha Tanzania kwenye reli.

Mimi sijawahi kushuhudia uteuzi wa hovyo kama huu toka nizaliwe
Uteuzi wa hovyo sanaaa
 
Binafsi huu uteuzi ni kichekesho na kituko kikubwa sana,umeonesha wazi kwamba wateuaji hawapo makini na wana uwezo mdogo Sana(very substandard).
🚮
 
Inasikitisha sana Tanzania sijui inaelekea wapi. DC ni nafasi nyeti ya kuunganisha watendaji na jamii inayowazunguka. Kusimamia mambo ya ulinzi na usalama. Hii ni nafasi ya waandamizi kutoka katika utumishi au chama, wakiwa wamejaa utu uzima na busara za kumwagika. Leo unaenda kuokoteza wasanii na watu mitandaoni.

Naona Tanzania inapoteza uelekeo kabisa. Hawa jamaa wanatupa kazi sana kuirudisha Tanzania kwenye reli.

Mimi sijawahi kushuhudia uteuzi wa hovyo kama huu toka nizaliwe
mkuu ,mama amewapa nafasi vijana nao washike nafasi za uongozi katika nchi yao,sijaona alipokosea, kwani we ulitaka awateue wote kutoka UVCCM au
 
Inasikitisha sana Tanzania sijui inaelekea wapi. DC ni nafasi nyeti ya kuunganisha watendaji na jamii inayowazunguka. Kusimamia mambo ya ulinzi na usalama. Hii ni nafasi ya waandamizi kutoka katika utumishi au chama, wakiwa wamejaa utu uzima na busara za kumwagika. Leo unaenda kuokoteza wasanii na watu mitandaoni.

Naona Tanzania inapoteza uelekeo kabisa. Hawa jamaa wanatupa kazi sana kuirudisha Tanzania kwenye reli.

Mimi sijawahi kushuhudia uteuzi wa hovyo kama huu toka nizaliwe

ndo kwaaanza sindano inaandaliwa, si mliwacheka sasa endeeleni kuanzisha uzi za kutosha wakiwa wanapokea mishahara ya kutosha
 
Msepende kumtaja taja Mungu kwenye fikra zenu yaani Mungu yupo kuwafuhisha nyie?
Wewe umepata mshtuko na roho imekuuma mno baada ya kuona kina Nassari wamepewa vyeo hamna jingine.

Uko sahihi, ila mstuko wa roho kwa mtu kupata uDC? Labda angekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa.
 
Wewe nani mpaka useme hivyo cha kushangaza wewe ni mateka wa Mbowe unataka Rais Samia, akufurahishe? Nyie kupinga ndiyo kazi mliotumwa na Mfalme Mbowe, Rais kawambia mpo huru kufanya mikutano yenu nchi nzima au nyie mnafanyie JF.
Wewe mateka ya Mwendazake bado una ndoto za Mwendazake làbda atarudi
 
Nafasi wapewe lakini sio ukuu wa wilaya. Wanaelewa nini kwenye utumishi na ulinzi na usalama.
Hakuna aliezaliwa anaelewa chochote. Hiyo ndio nafasi sahihi kabisa ya kuwapima vijana wetu.

Muacheni rais achague watu anaojua watamsaidia. Na wewe ukiwa rais utachagua wako mkuu

Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.
 
ndo kwaaanza sindano inaandaliwa, si mliwacheka sasa endeeleni kuanzisha uzi za kutosha wakiwa wanapokea mishahara ya kutosha

Kwahiyo heshima kwao ni hiyo mishahara na sio utendaji! Nimecheka kwa nguvu. Sitaki kuamini kuwa waamepewa hivyo vyeo ili wasichekwe kwa kupata mishahara ya kutosha. Hii inadhihirisha cheo cha uDC maana yake ni kupata mshahara wa kutosha ili usichekwe.
 
Wewe nani mpaka useme hivyo cha kushangaza wewe ni mateka wa Mbowe unataka Rais Samia, akufurahishe? Nyie kupinga ndiyo kazi mliotumwa na Mfalme Mbowe, Rais kawambia mpo huru kufanya mikutano yenu nchi nzima au nyie mnafanyie JF.
Hapo ndio upinzani wanashangaza sana.

Wanamnanga Nassari kwa kuwa alihama Chadema. Wao walimpokea Lowassa na straight away kumpa nafasi kubwa ya kugombea urais, walimpokea Nyalandu na hivyo hivyo wakampa nafasi ya uongozi.

Wao wanalolitaka ni waliohama CDM wasipokelewe popote. Wakuu acheni hizo
 
nikweli mana mlituletea magufuli asiyejua lolote kuhusu usalama akazingua kwelikweli ...vyombo vipi vitawasaidia
 
Back
Top Bottom