Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya uliofanyika Juni 2021 umeshusha hadhi ya nafasi hiyo

Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya uliofanyika Juni 2021 umeshusha hadhi ya nafasi hiyo

Hakuna aliezaliwa anaelewa chochote. Hiyo ndio nafasi sahihi kabisa ya kuwapima vijana wetu.

Muacheni rais achague watu anaojua watamsaidia. Na wewe ukiwa rais utachagua wako mkuu

Mama aachwe afanye kazi na neema zitapatikana kwa kila mmoja wetu.
 
UTEUZI uko vyema tu.....

MaDC ni wanasiasa pia....Chama tawala ni lazima kiendelee kushika hatamu KIUSHAWISHI.......USHAWISHI WA MAKUNDI TOFAUTI....tukumbuke 2025 tuna uchaguzi pia...mathalani Niki wa Pili si TURUFU kisiasa?!!!!!

#KaziIendelee
Mama ameamua kuchagua watu kutoka katika kada tofauti tofauti, na hili ni jambo la kupongezwa.

Kilichowauma CDM ni kuona waliotoka huko wanaramba vyeo.
 
P mayalla simuoni kwenye teuzi,ila formal miss tz yupo .Maajabu itabaki kusema,ilibaki hiviii ,yaaani hiviiiii kuwa Dc[emoji3][emoji3]
 
Binafsi kwa uteuzi huu,, umeniondolea imani kubwa nilokuwa nayo kwa mteua,,, kwani zaidi 75% ya wateule wake kwenye huu mkeka hawana sifa stahiki za kuwa kwenye hizi ofisi nyeti.
Wewe ndio unazo sifa??

Haya tufanye mama kakosea, teua wewe basi tuone utakavypatia
 
Nakumbuka zamani ma Dc walikuwa ni wastaafu au walikaribia kustaafu kwenye idara za ulinzi.(JWTZ & Police)
Ndio inavotakiwa sio sijui mtu alikua miss,mtu wa mitandaoni huko kupost post,bongo movie anakua mkuu wa wilaya.
Wakati kuna wastaafu, profesa,academicians tunaohitaji mchango wao bado wanaachwa.

Uvccm huko washachanganyikiwa saiv hawajui hataa kinachoendelea
 
Sasa maprofesa wakajazwe kuwa maDC huko wilayani na kufundisha WAWAACHIE akina nani ?!!!

uDC ni nafasi ya KISIASA pia.....siasa ni USHAWISHI.....mathalani unadhani waliofanya vetting ya CHOPA MCHOPANGA hawajitambui?!!!

Usisahau uchaguzi mwingine unakuja 2025 in shaa Allah.....

#ChamaNiLazimaKishikeHatamu
#KaziIendelee
#NchiKwanza
Kumbuka kwamba Mama hakuwa chaguo la CCM bali la Mwendazake. Na hiki kitendo kimewafanya CCM wajitafakari.Hivi sasa lile kundi lililosema Mwanamke ni Mwanamke tu hawezi kuwa Kichwa cha nyumba bali Pambo la nyumba linafurahia kuboronga kwake ili aweze kutoswa na wenye chama muda utakapowadia 2025.
 
Wasanii nao ni watanzania, wapewe nafasi waonyeshe vipaji vyao mbona Jokate ameweza, tuwe wavumilivu tumor mama nafasi afanye kazi

Jokate alishawahi pitia uvvcm uko so maadili ya uongozi anayajua sasa mtu alikua msemaji wa weusi hajawahi kuongoza hata kata leo anapewa ukuu wa wiraya.pathetic
 
Ndio inavotakiwa sio sijui mtu alikua miss,mtu wa mitandaoni huko kupost post,bongo movie anakua mkuu wa wilaya.
Wakati kuna wastaafu, profesa,academicians tunaohitaji mchango wao bado wanaachwa.

Uvccm huko washachanganyikiwa saiv hawajui hataa kinachoendelea
Zama zimebadilika MKUU....

Maisha ya sasa WAZEE WAKO MITANDAONI.....

Unataka vetting ya uDC ifanywe Kama enzi za AZIMIO LA ARUSHA mwaka 1967?!!

#KaziIendelee
#NchiKwanza
 
Yaani mtu upo zako studio unaambiwa umeteuliwa kufanya Kazi hata hujawahi kuiomba wala kuifikiria.
Nadhani DC na RC ni ajira, zitangazwe na wenye nia na sifa waombe.
Haya mambo ya kuteuana kiholela ndio yanatupatia wakina Sabaya wanatesa wananchi.
Sabaya alikuwa na kesi ya jinai mahakamani ya kujifanya afisa wa usalama, akateuliwa DC, alichoenda kukifanya wote tunajua.
 
Jokate alishawahi pitia uvvcm uko so maadili ya uongozi anayajua sasa mtu alikua msemaji wa weusi hajawahi kuongoza hata kata leo anapewa ukuu wa wiraya.pathetic
Msemaji wa WEUSI walio na USHAWISHI kwa vijana.....hasa wa KASKAZINI.....

Msemaji wa WEUSI mwenye shahada zaidi ya MBILI.....

Msemaji wa WEUSI ambaye yuko SMART UPSTAIRS.....

KUSOMA HATUJUI HATA MAANDISHI HATUONI....?!! chama ni lazima kishike hatamu......

#SiempreCCM
#VivaCCM
#KaziIendelee
 
Hapo ndio upinzani wanashangaza sana.

Wanamnanga Nassari kwa kuwa alihama Chadema. Wao walimpokea Lowassa na straight away kumpa nafasi kubwa ya kugombea urais, walimpokea Nyalandu na hivyo hivyo wakampa nafasi ya uongozi.

Wao wanalolitaka ni waliohama CDM wasipokelewe popote. Wakuu acheni hizo
Sidhani kama tatizo ni wao kuhamia upande wa pili. Ni namna wanavyohamia. Hawa vijana walihama huku wakitukana walikotoka wakisahau fadhila kubwa waliopewa na jinsi walivyopiganiwa wakati walipokuwa na matatizo.

Mimi binafsi nawaheshimu wakina Halima kwa kukataa kwao kutumika kuchafua chama ambacho kimewafukuza. Hawa vijana ni mamluki na opportunists. Hawatasita kuwachoma chama kingine kikiingia madarakani.

Amandla...
 
Back
Top Bottom