Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya uliofanyika Juni 2021 umeshusha hadhi ya nafasi hiyo

Subiri nafasi za ukurugenzi, hapo watajazwa makada na wagombea ubunge kura za maoni ccm wa kutisha, rais ajitaidi Sana aboreshe utumishi wa umma, Serikali ingeboresha utumishi wa umma tungepiga hatua kubwa Sana Kama taifa.Rais kwenye ukurugenzi aachane na tabia ya kuchomeka wanasiasa walioshindwa kwenye kura za maoni, badala yake awaombe utumishi wa umma jumps data base yenye watumishi wenye sifa na weledi wamsaidie kazi.Aachane na Mambo ya kuteuliwa mtu kwa vile anajulikana vipi, Hilo halitatusaidia Kama taifa.Kwenye utumishi wa umma wako vijana wengi Sana wenye uweledi wa kufanya kazi, tatizo hawana connections.Kuendelea kutumia mtindo uleule wa kuteuana kwa kujuana hautatupeleka mbele Kama taifa
 
Huyo bongo movie na bongo fleva ni wasomi wazuri sana sasa ulitaka wapewe watu gani professor mwache aendelee kufundisha
 
Mkuu umejibu vyema sana. Maana hawa ni watu wasaliti na hawana msimamo. Kesho watamuhujumu rais kwa maslahi binafsi. Leo hii wanapewa cheo cha kuongoza askari na kusimamia mapato na miradi
 
UTEUZI uko vyema tu.....

MaDC ni wanasiasa pia....Chama tawala ni lazima kiendelee kushika hatamu KIUSHAWISHI.......USHAWISHI WA MAKUNDI TOFAUTI....tukumbuke 2025 tuna uchaguzi pia...mathalani Niki wa Pili si TURUFU kisiasa?!!!!!

#KaziIendelee
Haahaa uchaguzi hata tufanye Mara 10 ccm ndo mshindi, we ulisikia wapi mechi ya Simba na yanga, refa anachaguliwa na yanga
 
Kwa Niki wa pili hapo ndo raisi kachemka kabisa
 
Nassari, lijuakali, mashinji lazima huu itakua uteuzi mbaya...
😀😀😀
 
Inasikitisha sana kuwa na nchi ambayo watu wake wanaamini uongozi ndio keki ya taifa na mtu akipewa cheo ameula
Wametoka kweli mkuu mtu akipewa cheo ujue umaskini ndio basi tena. Kuna mkuu wangu mmoja anaiba balaa anaforge hadi sign za wenzie.
 
Hii trial and error hadi lini? Mtu Watanzania wamemkataa jimboni Kwa kumuona hafai lakini bado anapewa Ukuu wa Wilaya!!!! Baada ya miaka 60 ya uhuru huu upumbavu utaendelea hadi lini!?
Nchi hii bado Sana angalia wabunge bungeni hakuna kitu yani tumetoka kuwa na wabunge Aina ya kina mrema utawala wa mkapa mapka Kuja kuwa na wabunge Aina ya msukuma na utawala wa Magufuli na sasa Samia.

Ukuu wa wilaya tumetoka kuwa na ma-DC aina ya mzee Twalib "ulimwengu" nyakati hizo mpaka Kuja kuwa na ma-DC wapya Aina ya Niki wa pili huu Kama si upumbavu ni nini.

Tanzania bado Sana Sana tu
 
Once a loser ALWAYS A LOSER. Don’t waste your time with LOSERS.
Anaweza kujirekebisha akarudi na kuwa sawa, hata hao unaowaona wanafaa leo huenda huko nyuma waliboronga wakaaminiwa kwa mara nyingine wakajisahihisha...
 
Kinachotengenezwa hapa ni timu itakayohakikisha CCM inashinda chaguzi zijao. Unadhani watu kama Lijualikali, Nassari n.k. watasita kucheza rafu ili kuhakikisha timu yao inashinda? Hawa ndio frontline soldiers maana si watumishi wa umma kama wakurugenzi. Kwa sababu hiyo, huu uteuzi ni mzuri sana.

Amandla...
 
Katiba yetu ndiyo inasababisha yote haya, hata mteuaji hastahili kuwamv apo alipo
 
Pole sana, nilikuhaidi kuwa utanikumbuka! Yapo wapi sasa na bado. Hapa steringi ni JK yangu macho
 
Hajaelemewa, ila hapo ndiyo uwezo wake ulipoishia.
 
Binafsi ili la mweusi sijalihafiki na huo ushawishi sijui umeupima vipi na huko upstairs pia sijajua umepapima vipi.

Huyu Niki ana kazi kubwa ya kutufanya tuamini kuwa mama hakukosea. Anatakiwa atuprove wrong. Ila so far kwangu ni uteuzi wenye mashaka.
 
Wewe nani mpaka useme hivyo cha kushangaza wewe ni mateka wa Mbowe unataka Rais Samia, akufurahishe? Nyie kupinga ndiyo kazi mliotumwa na Mfalme Mbowe, Rais kawambia mpo huru kufanya mikutano yenu nchi nzima au nyie mnafanyie JF.
Umeishiwa hoja. Jina la mbowe limetoka wapi kwenye uzi huu?
 
Kabisa nakuunga mkono umenena mdau yaani hao washauri wanaowanaomshauri mama sijui ni watu wa namna gani,angalia wahamiaji wenye uchu wa madaraka waliotoka upinzani karibia wote kawapa ,hana tofauti na hayati magufuli kuwapa kazi wapinzani mi nikajua amejifunza wakati kuna vijana wako ndani ya ccm wamekitetea chama toka zamani wangepewa ,unawapa vyeo misanii iliyozoea miziki isiyo na maadili kwenye nafasi nyeti na za muhimu ,yaani sijui mama anafeli wapi
 
Wewe acha tu, ndo utasikia akiteuliwa fulani Tz kuwa kiongozi basi utasikia ' aisee kaula', ikiashiria hakuna kuongoza wananchi zaidi ya kwenda kujineemesha.... kazi iendelee.
Wametoka kweli mkuu mtu akipewa cheo ujue umaskini ndio basi tena. Kuna mkuu wangu mmoja anaiba balaa anaforge hadi sign za wenzie.
H
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…