Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya uliofanyika Juni 2021 umeshusha hadhi ya nafasi hiyo

Kamanda mbona mama amewachefua mapema?
 
Mwacheni Rais aunde timu anayotaka....Amepata ushauri kwa watu anaowaamini na hiyo inatosha. Walioteuliwa wote ni watanzania na wana fursa sawa.
Hata wakikosea kwa kukosa experience, wataonywa na wakati mwingine watajifunza kwa makosa ya wenzao....Kupitia uteuzi huu inaonyesha mama anawasikiliza subordinates na washauri wake na anafanya power delegation ya kutosha. Wasimuangushe, wapige kazi.

Tuendelee kumtakia kila jema Rais wetu. Hana ubaguzi,ni msikivu na mshirikishi. Mengine atabadilisha polepole
 
Wewe nani mpaka useme hivyo cha kushangaza wewe ni mateka wa Mbowe unataka Rais Samia, akufurahishe? Nyie kupinga ndiyo kazi mliotumwa na Mfalme Mbowe, Rais kawambia mpo huru kufanya mikutano yenu nchi nzima au nyie mnafanyie JF.
Kufikiria kwamba watu wote wanaweza kuwa na mawazo yanayofanana ni upumbavu uliotukuka.

Wewe kama umeamua kusalimisha akili zako kwa m/kiti wenu basi ni wewe, usitegemee wote wawe hivyo.

Hizi teuzi sisi wengine tunaona hazina maana katika dunia ya sasa eti bado tuwe tunabambikiwa watawala na mtu moja badala ya sisi wenyewe kuwachagua ili tuwe na fursa ya kuweza kuwawajibisha wakati wowote tukiona inafaa kufanya hivyo.

Mfano, mimi niko Mara ninaletewa mtu kutoka Mbeya au Mtwara kuja kuniongoza na nikiona hanifai siwezi kumuondoa hadi eti impendezee aliye mteua!! Huu ni utawala wa kiimla tumechoka nao na ndio maana tunahitaji katiba mpya.
 
Bora hivi vyeo vifutwe kabisa
 
Tanzania oooooooooh nchi yangu weeeeeeeeeeeee ghafla bin vuu watu washamgeuka mama.narudia tena kila rais anateua watu ambao atakuwa comfortable kufanya nao kazi tusimlazimishe kuchanganya betri na magunzi tochi haitawaka
 
Wasanii nao ni watanzania, wapewe nafasi waonyeshe vipaji vyao mbona Jokate ameweza, tuwe wavumilivu tumor mama nafasi afanye kazi
Joketi kaweza kipi .Watu wa kisarawe wengi wao ni wakulima Bora kama angewasaidia kupata masoko ya mazao yao hapo tungeona kaweza.Eti mnadai kajenga shule .sasa kama ni shule mbona zimejengwa nchi nzima.nachokiona kwake anabebwa na midia tu ,Hana ubunifu wowote.
 
Sasa Kama vigezo wanavyo kwa Nini wasiteuliwe na ukiangalia hao wasanii Elimu zao nikuanzia ngazi ya shahada(degree) na huyo Niki tena Ana degree mbili sizani Kama kakosea acha vijana tuneemeke na huu uongozi acheni kutukunjia Sana [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu wa Wilaya ni cheo Cha kisiasa tu na Cha kikoloni, kazi wanayo wakurugenzi na ma Dad...
Ni sawa lakini ndo wachukuliwe watu from nowhere? Haya ni maajabu ya aina yake.
 
Ifike mahali tuwe na vigezo vya vyeo vyote hata kama ni vya kuteuliwa, tunazidi kurudi nyuma kila mtawala anayeingia wamuige the late Mkapa ambaye hakupenda uteuzi. Tuwe na proffesionalism kwenye teuzi au watu waombe. Vyuo alivyofungua Mwalimu Nyerere kwa ajili ya viongozi tumeviacha tunategemea unyenyekezi na kusifia viongozi ili uteuliwe
 
Wacha hizo, Ronald Reagan alikuwa mcheza filamu, akawa gavana wa Calfornia USA badae akawa Rais Arnold Shwarzneger alikuwa mcheza body builder, akaenda kucheza sinema, akawa gavana wa Calfornia jimbo ambalo kama lingekuwa nchi, lingekuwa the 6th richest nation duniani, na rekodi yake ilikuwa nzuri sana! Rais wa Ukraine ni mcheza komedy kama Mpoki lakini nchi iko stable licha ya ubabe wa Urusi! Jokate amefanya vizuri Kisarawe! Mbona watumishi wa umma, wasomi wazoefu kama Hapi, Kasesera, Chalamila, Odunga nk hovyo kabisa! Kaka Uongozi ni karama, dont judge a book by its cover! Kwa mfano mimi simuoni Nikki wa pili akishindwa uDC hata kidogo pamoja na usanii wake! Be +ve kaka wacha tuwape stage wanaweza kutusogeza mahali, usivunjike moyo sana kwa sababu Sabaya kaharibu!
 
Kwa hili nakuunga mkono. Naona ameteua team ya kampeni yake 2025 badala ya madc
 
Msukuma asihukumiwe kisa ni darasa la saba, ana brains nyingi sana jamaa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…