Zote Bado ni nadharia tu. labda tulitupwa kutoka edeni, ambako hatukuzoea shuruba za kujitaftia, kila kitu kilikuwepo.
Nadharia nyingine ukisoma kitabu cha the Book of Enoch, hao wazungu wametokana na muingiliano kati ya watchers/ annunaki/ fallen angels na watu weusi, ndio wakapatikana wao, so hizo teknolojia na maendeleo wanayopiga wanapewa usaidizi na hao watchers, ili waje waitawale tena Dunia, ukisoma kitabu cha The book of enock, baada ya maasi kuzidi kulikosababishwa na wanefili( vizazi vya watchers) , hao fallen angles walipewa adhabu ya kufungiwa chini ya Dunia,/kuzimu, na vizazi vyao /( wanefili) vikaangamizwa kwenye gharika ya nuhu
Kuna tafiti wanafanya wazungu wakisaidiwa na hao watchers mfano ile ya CERN ilioko uswizi ili waweze kufungua uko chini walikofungiwa hao watchers waje Duniani kutawala tena.
Hizo zote ni nadharia, ambazo hazijathibitishwa.
Kuna nadharia nyingi sana kuhusu mtu mweusi au human race in general. Lakini jambo moja ambao wote tunakubali, ni kuwa mtu mweusi ni phenomena ya ajabu! Aidha kuna laana, na kama huamini laana kuna kibaya kiitokea katika Evolution yetu!
Hebu angalia kwa mfano kwenye Berlin Conference 1884, mataifa madogo mno kama Belgium, German, Uingereza , France nk kukaa mezani na kuigawana Africa kama keki! Africa inameza kabisa nchi zote hizo! Hizo tawala kubwa za Kiafrika zilikuwa wapi? Kwa kifupi lazima ukubali zilikuwa gizani kabisa.
Na mpaka leo ukitaka kujua asili ya watu wa Africa au makabila, lazima urudi kwenye vitabu walivyoandika wazungu! Mababu walibakia kwenye oral traditions ambazo zilikuwa confined kwenye makabila yao tu.
Tulikuwa na dini na miungu yetu, lakini yote haya yalimwezwa kwa ujio wa Mzungu au Mwarabu, na lakusikitisha HATUWEZI KABISA KURUDI HUKO!
Hata hao wanaopiga kelele leo kwamba turudi kwenye tamaduni zetu au mila na desturi zetu hujui wanasema nini hasa! Na sijui wanajua tamaduni zetu ni nini!
We are confused as a race! Hatujui tufanye nini! Hatakujifunza tu! Tumeisha kuwa twisted kiakili. Wenye PHD na mbumbumbu wote sawa! Mzungu mmoja aliwahi kusema Mwafrika anahitaji Degree ya kwanza tu ili ku survive! Elimu zaidi ya hapo ni kupoteza muda wake! Haina msaada wa kubadili maisha yake! Au mwelekeo wake! Na labda ni kweli, hatuongezi kitu chochote katika teknoloji, philosophy etc.
Hivyo inawekana kabisa kuna ulimwengu mwingine kabisa ( mystic)
mebeba ukweli kuhusu Mwafrika! Na kuna jamaa mmoja alisema Mwafrika angelipata ufahamu wa elimu kama wa mzungu angekua mbaya kuliko mzungu!
Anyway labda siku moja kama huko nyuma tulikua great, upepo utatugeukia na kuwa juu tena!