Utoto wa Fei Toto utawasumbua wachezaji wa Kizanzibari

Acha upumbavu.... Unahusisha mambo ya kipuuzi na mpira. Yanga bado tutatafuta vipaji Zanzibar. Kwani kwa Morrison ilikuaje? Si ndo alitudhalilisha zaidi? Sasa hivi anachezea team gani? Na yupo wapi?
 
Yanga ilipojitela ni pale tu ilipoweka kipengele cha Fieitoto kuilipa Yanga milioni 100 na mishahara ya miezi 3 endapo atataka kuvunja Mkataba,mengine yote haya ni maongezi ya kunogesha kijiwe cha JF tu
Hapo ndipo uongozi wa Yanga ulipochemka, na ni wazi mambo ya kimkataba uongozi hauna mwana sheria mahiri na pia kuna watu wana uwezo wa kufikiri ndani ya uongozi wa Yanga. Bora wasingeandika kabisa kipengele cha kuvunja mkataba bali wasubiri mkataba unataka kuvunjwa wanakaa mezani anapewa thamani ya pesa ya kuuvunja mkataba. Sio kuandika vile kama walivyofanya wao, basi bora hata wangeandika ela nyingi kwanza bilioni wao wameandika milioni mia. Wamechemka sana kwakweli
 
TOA MWIKO AKILI IJAE VIZURI,unawasimanga wazanzibar kwa mgongo wa FEI,acha ushamba
 
Hata kama angalikuwa analipwa sh moja, taratibu za uondokaji zizingatiwe. Nani anakumbuka kisa cha Makelele na Real Madrid? Fei kuondoka Yanga sio tatizo, shida inaanzia pale anapowaacha waajiri wake waliokuwa wamemweka kwenye programu yao kwa dharura, ni kama shambulizi la kushitukiza na hivyo kuvuruga mpango wa timu. Alipaswa kutoa tahadhari kwa uongozi kuwa msimu uliomalizika na hali ikiendelea kuwa hivi atalazimika kuondoka.

Fei sio mfano mzuri kwa vizazi vijavyo vya soka.
 
Kama hakuwa na jeuru ya kwenda popote maanake hakuwa na ubora/ kiwango cha kumpeleka popote au unataka kusema alikuwa ajitambui?
Sio kweli

Kwani katika hicho kipindi uliona perfomance yake ikiwa low?

Una maanisha saizi Mayele hana ubora kwasababu hakuna timu ambayo imeonesha nia kumtaka?
 
Amejikita kwenye mada iliyopo mezani.Wewe anzisha hiyo mada ya kuhoji kwa nini CEO ameresign atakuja kuchangia pia
 
Ukiona mtu yeyote ambaye anakwenda na jina la utotoni au la kishamba hadi ukubwani ujue Kuna tatizo
 
Sio kweli

Kwani katika hicho kipindi uliona perfomance yake ikiwa low?

Una maanisha saizi Mayele hana ubora kwasababu hakuna timu ambayo imeonesha nia kumtaka?
Una uhakika Mayele hakuna timu inayohitaji huduma yake mpaka sass? Kuna performance halafu kuna performance za kushawishi timu zingine zikugombanie. Embu niambie wakati Yanga wana muongezea Feitoto mkataba je wewe ulisikia timu zipi zilikuwa zina mgombania Feisal?
 
Mkuu kwani juzi wakati mnasaini mkataba mpya kwanini hamkufikiria kipengele hicho kama mliona kuna kero inaweza kujitokeza endapo mtataka kuongeza maslahi katikati ya mkataba?

Kama maslahi hayarekebishwi katikati ya mkataba mbona punde tu baada ya kuonesha nia ya kuondoka mlikuwa tayari kumpa hitaji lake ili kumfanya aendelee kubaki bila kujali ni katikati ya mkataba??
 
Vitu vingine tusijadili kama hatujui mifumo ya uongozi wa hizi Club zetu

Ebu jiweke katika nafasi ya Feisali afu jaribu kufikiria unaomba kuongezewa mkataba mpya wenye maslahi bora.

Wakati huo hakuna timu yeyote iliyoonesha nia ya kukuhitaji (means hauna plan B nje ya Yanga)

Kiasi ulicho demand kuongezewa vipi kama mkishindwa kufika muafaka na uongozi je utaenda wapi?

Ni ngumu sana hilo wazo la kuomba kupewa mkataba wenye maslahi kuwezekana
 
Hakika
 
Mayele ni tetesi tu tena kwenye vyanzo vile vile ambavyo msimu uliopita vilianzisha tetesi kama hizo mpaka Senzo akaweka kiapo kuwa akiondoka Mayele nayeye ataondoka

Kipindi Yanga wanamuongezea mkataba Feisali ni kweli hakukuwa na tetesi za Club zingine kumhitaji

Lakini katika hicho kipindi unataka kutuaminisha kuwa alikuwa under perfomance?
 
Ndo maana ameachwa akatafute maslahi anapoona inafaa yeye
 
Unaelewa kweli nachoongelea? Kuna performance na kuna performance ya kushwawishi timu zingine zihitaji huduma ya mchezaji husika. Feisal kutohusishwa na tetesi yeyote maanake hakuna club iliyokuwa inamuhitaji. Nakumbuka ishu ya Feisal ilianzia humu humu JF kuna mtu alianzisha uzi wa kigogo wa Azam amng'oe Feisal pale Yanga. Kiufupi Feisal kashawishiwa na kaweza kushawishika badala ya mapungufu ya kimkataba dhidi ya Azam. Feisal alisaini mkataba na Azam kwa kukubali kiwango cha masilahi wala hakushikiwa bunduki ili asaini.
Kuna mtu alianzisha hili chokochoko humu jukwaani

 
Asante kwa kunisahihisha.Back to my point,kwa muktadha huo sioni kwanini Fei ashutumiwe kwa kuondoka katikati ya kipindi cha mkataba wake.Umetoa angalizo zuri sana ambapo wengi wa Mashabiki wa Yanga hawataki kuliona la udhaifu wa Viongozi wa Yanga walioundaa huo mkataba.
 
Wabongo tuna ujuaji wakijinga Sana!! Kwahiyo mkataba wake ulisema baada ya kiwango kuwa juu adai maboresho ya maslahi??. Vipi Kama kiwango kingekuwa kibovu je angedai kushushiwa mshahara??. Tuacheni upuuzi huu, Kama alitaka kuondoka angefuata taratibu za kimpira.
 
Ukiona mtu yeyote ambaye anakwenda na jina la utotoni au la kishamba hadi ukubwani ujue Kuna tatizo
Nyinyi ndiyo mnajiona wajanja kwa kuwaita watoto wenu "Junior au Beyonce" majina ambayo siyo ya 'kishamba'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…