Mkuu tusichanganye mambo mawili hapa, mchezaji analipwa kutokana na kiwango alichonacho kwa wakati huo au kutokana na mkataba wake unavyosema??.
Haya ni mambo mawili yanayotegemeana huwezi kuyatenganisha
Mchezaji kulipwa pesa kwasababu ya Mkataba haimaanishi hana nafasi ya kuongezewa mshahara kulingana na improvements ya ubora aliyokuwa nayo.
Na ndio maana Yanga waliona ipo haja ya kuboresha zaidi mashahara wa Feisali ili kumfanya aendelee kubakia
Mkataba ni malidhiano yenye kuleta tija pande zote mbiki, ukishasaini mkataba wa maslahi yako means umelidhia kuwa hicho umekikubali kinakufaa!!.
Hili nakubaliana na wewe lakini bado linamaelezo yake
Mfano siku ya kusaini mkataba mpya mchezaji anaweza akaja na mapendekezo yake ya kuongezewa mshahara kulingana na kiwango chake
Lakini Club sio lazima ikubaliane naye na hivyo atalazimika kusaini mkatana mpya hata kama haukidhi mahitaji yake kwasababu hana option zaidi.
Sasa mchezaji huyu siku amepata shavu kutoka Club nyingine kwanini Club ambayo haikuwa tayari kumuongezea mshahara, safari hii iwe tayari kutimiza matakwa yake??
Suala la mchezaji kutaka kupewa maslahi mengine ni haki yake Kama mfanyakazi lakini hauna uwezo wa kuvunja mkataba ambao una terms kibao, yaani unaweza kupewa tu ofa na timu fulani ukaaamua kuvunja mkataba na boss wako bila kurudi mezani?.
Mkuu swala la kuvunja mkataba lina vipengele vingi na sio lazima uvifate vyote
Moja ya kipengele ambacho nimeona Feisali amekitumia ni ile sheria inayomtaka arudishe pesa ya usajili pamoja na mshahara wa miezi 3 kitu
Kama ni kosa kisheria ngoja tutaona hili swala mwisho wake utakuwaje
Kwahiyo Mzamiru adai maaslah mapya saizi kwakuwa yupo kwenye top performance?. Kama mikataba ingevunjwa kwa stahili hii basi ingekuwa kichekesho .
Mzamiru anaweza akadai mshahara kwasababu sio dhambi ni swala la makubaliano tu na Simba kama haimlipi vizuri basi siku imetokea offa kutoka Club nyingine sitegemei kuona Simba inamuita tena mezani kufanya mazungumzo kumpa kile alichokiomba