UTU: Ubalozi wa Marekani wasaidia ujenzi wa vyoo vya kisasa kwenye shule za Iringa na Morogoro

Umeongea Kwa uchungu Hadi nimejikuta chozi likinitoka aisee

Tuna Baadhi ya viongozi ambao ni washenzi Sana, Wapo Kwa ajiri ya faida zao Tu na sio kusaidia jamii

Raisi wetu aongeze kutumbua majiti yasiyojielewa
 
Ni aibu Sana aisee kwa nchi ya uchumi wa Kati kusaidiwa choo. Hali mkurugenzi ananunua v8 la m 470.
Hakuna tusi kubwa Sana duniani kuliko lote Kama mtu kujijengea choo yaani amekudharau Sana yaani amekuona kichwani ni kopo kabisa. Aibu Sana kwa dona kantri inayonunua ndege cash
 
Hivi kuna misaada ambayo si ya kibinadamu? Hata ujenzi wa barabara unalenga kuhudumia binadamu. Sijui ni misaada ipi ambayo si ya kibaindamu?
Ukinunuliwa bunduki na mabomu ni misaada dhidi ya binadamu.
 
Hao ndio MABEBERU!! Bombadiyeee na Drimulaina OYEEEEEEEEEE!!
 
DONOR COUNTRY IN THE RIGHT TRACK!
 
Hii ya lini kwani? Si mlisema mabeberu wamekataa kutoa msaada kwa ajili ya Lissu kushindwa uchaguzi?
Mabeberu yana huruma. Yameona tunafikiria kununua ndege na kuwasahau vijana wetu wanaosoma bure ... wakaamua kusaidia!!
 
Hapo unakuta mkurugenzi ananunua v8 la m 470 cash, aliyeturoga alishakufa.
 
Tundu lisu hajawakatazaa?
 
Miongoni mwa Watu ambao huwa nakubali pale Waafrika tukidhihakiwa Wapumbavu na Wazungu ni Mimi. Karne hii bado pia tunajengewa Vyoo?
 
Haya ni maajabu .tunasaidiwa mpaka vyoo arafu mnawaita mabeberu
 
Mabeberu yana huruma. Yameona tunafikiria kununua ndege na kuwasahau vijana wetu wanaosoma bure. Wakaamua kusaidia!!
Wasaidie pia kujenga ofisi za CHADEMA hata makao makuu tu.
 
Ukinunuliwa bunduki na mabomu ni misaada dhidi ya binadamu.
Kwa nini isiwe misaada, unajilinda dhidi ya maadui. Mfano magaidi wanaosumbua watu huko Msumbiji na Mtwara, dawa yao ni mabomu tu. Huoni huo ni msaada mkubwa sana kuliko hata hiyo choo kwani umeaidia kurudisha amani kwa watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…