Bw. Pascal amezindua kitu muhimu hapa,
Tume iko huru ,lakini si shirikishi.
Mimi nionavyo.
1.Sheria iondowe mamlaka ya tume kuwa na kauli ya mwisho juu ya matokeo ya Uraisi. ,yaani tume ikikosea iweze kushitakiwa na matokeo yapingwe mahakamani,bila ya muhusika kupewa nafasi hiyo.
2.Matokeo yote ya uchaguzi kuanzia Uraisi hadi diwani yapingwe Mahakamani.
Na pakiwekwa pingamizi tuu,matokeo ya uchaguzi yasitekelezwe hadi kesi iishe.
3.Polisi,jeshi na vikosi vingine viishie mlangoni katika shughuli ya upigaji kura, kuhesabu na kotoa matokeo. Vyama viachiwe vyenyewe vimalizane na tume bila kuingiliwa na Vyombo vya dole vinavyoonesha upendeleo kwa chama tawala.
4.Wiki moja kabla uchaguzi nchi akabidhiwe jaji mkuu,awe ndio mshika dola, waliobakia wote mpaka raisi wawe ni wagombea wa chama husika tuu wasio na mamlaka ,hadi hapo matokeo yatakapo tangaazwa na kutowekewa pingamizi za kisheria.
Hapo tutajuwa kuwa Plat form imewekwa Level na hakutokuwa na Kutuhumiana. Ili tume iwe huru inapaswa kutowa matokeo hadharani huku wahusika wakiwepo na kuyahakiki kuwa ndivyo yalivyokuwa vituoni na kusomwa na tume.
5.Tume isiwe na haki ya kufuta Uchaguzi katika hali yoyote ile , isipokuwa kwa amri ya Mahakama,na ushauri wa Jeshi la polisi kwa masharti maalumu. Sio kama alivyofanya Jecha kule Zanzibar ya kufuta uchaguzi kwa mapenzi yake tuu pasi na sababu yoyote isipokuwa ni kuibeba CCM iliyokuwa imeshindwa vibaya.