Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

Asante sana Mama Amon kwa Makala iliyo sheheni maarifa. Ungenukuu tarehe ya waraka ingenoga zaidi.

Paschal,
Katika hili hongera kaka, umeutendea haki uzi.
 
Bw. Pascal amezindua kitu muhimu hapa,
Tume iko huru ,lakini si shirikishi.
Mimi nionavyo.

1.Sheria iondowe mamlaka ya tume kuwa na kauli ya mwisho juu ya matokeo ya Uraisi. ,yaani tume ikikosea iweze kushitakiwa na matokeo yapingwe mahakamani,bila ya muhusika kupewa nafasi hiyo.

2.Matokeo yote ya uchaguzi kuanzia Uraisi hadi diwani yapingwe Mahakamani.
Na pakiwekwa pingamizi tuu,matokeo ya uchaguzi yasitekelezwe hadi kesi iishe.

3.Polisi,jeshi na vikosi vingine viishie mlangoni katika shughuli ya upigaji kura, kuhesabu na kotoa matokeo. Vyama viachiwe vyenyewe vimalizane na tume bila kuingiliwa na Vyombo vya dole vinavyoonesha upendeleo kwa chama tawala.

4.Wiki moja kabla uchaguzi nchi akabidhiwe jaji mkuu,awe ndio mshika dola, waliobakia wote mpaka raisi wawe ni wagombea wa chama husika tuu wasio na mamlaka ,hadi hapo matokeo yatakapo tangaazwa na kutowekewa pingamizi za kisheria.

Hapo tutajuwa kuwa Plat form imewekwa Level na hakutokuwa na Kutuhumiana. Ili tume iwe huru inapaswa kutowa matokeo hadharani huku wahusika wakiwepo na kuyahakiki kuwa ndivyo yalivyokuwa vituoni na kusomwa na tume.

5.Tume isiwe na haki ya kufuta Uchaguzi katika hali yoyote ile , isipokuwa kwa amri ya Mahakama,na ushauri wa Jeshi la polisi kwa masharti maalumu. Sio kama alivyofanya Jecha kule Zanzibar ya kufuta uchaguzi kwa mapenzi yake tuu pasi na sababu yoyote isipokuwa ni kuibeba CCM iliyokuwa imeshindwa vibaya.
 
Pascal Mayalla,
Pascal nimekuelewa mno. Kwa sasa tume ni huru. Lakini ni uhuru wenye hiari ya kuonekana au kutokuonekana. Tatizo kubwa ni uhuru huo kutokuonekana.

Ili uhuru wa tume uonekane yafanyike mambo ya msingi yatakawezesha hilo. Mambo haya pamoja na mengine ni huo ujumuishi (inclusiveness) na uwazi (transparency) kwenye utendaji.
 
Kitaturu,
I fully concur with your argument which is absolutely undisputable.

However, I tend to perceive that you either misunderstood or misinterpreted Mr. Paschal's argument by simply allowing your focus merely on the word "milele" which I believe was rightly used by Paschal in a sense that he is a person who regularly uses some difficult words to stir up the discussion and/or raise people's heads to be mindful of their life-timeline in a manner that avoids taking too long to make decisions which are already due or even late.

I think Paschal intends to urge people to refrain from unthoughtful living and act timeously and appropriately with a responsible social attitude that implies setting defined objectives that are achievable within timelimits. Part of our objectives should include national leadership that must not be permitted loopholes to dictate their leadership styles and assured continuity of tenures whereas the entire mass remain weakened without ability to make their voting count for who should lead and who shouldn't.

I think the u-milele in this case may imply torelated long periods for unfitting leadership while we remain starring at them as they determine the national destiny of their own choice.

We ought to be angered by our inaction rather that words like milele and others.
 
Nami pia nashauri msusie uchaguzi. Ila ujiulize, mliposusia ule wa Serikali za Mitaa mlipata impact gani?

Impact iliyopo ndio hilo joto la kudai tume huru na wananchi wote kuelewa nini tunamaanisha. Ingekuwa tumeshiriki leo hii tungedai hiyo tume huru tusingeeleweka.
 
Mlikuwa wapi tangu 2015?

Tume huru ilianza kudaiwa toka mfumo wa vyama ulipoanza hapa nchini, sio madai ya wiki iliyopita. Unaposema tulikuwa wapi hiyo 2015, naona hiyo 2015 ndio ulianza kujua siasa baada ya hizi siasa chafu kuanza hapa nchini.
 
Tume huru ilianza kudaiwa toka mfumo wa vyama ulipoanza hapa nchini, sio madai ya wiki iliyopita. Unaposema tulikuwa wapi hiyo 2015, naona hiyo 2015 ndio ulianza kujua siasa baada ya hizi siasa chafu kuanza hapa nchini.
All the best. Mkiipata nitawapongeza.
 
Mama Amon,
Ninapomaliza kusoma uzi huu natafakari sana. Uchambuzi thabiti usio na chembe ya shaka au uchama. Nilipoona tena jina la Mama Amon nikatafakari akina dada/mama majasiri wangu, Halima Mdee, Fatma Karume, Maria Sarungi, Jesca Kishoa, Esther Bulaya na wengineo.

nikihesabu waungaji juhudi katika kundi la wanawake kulinganisha na vidume naona wazi kuwa ukombazi wa Tz uko kwenye mstakabali wa wanawake.
Mama Amon you are one of my heroes!
 
Historia itajiandika vibaya sana kwa wajukuu vilembwe na vilembwekeze vyetu...kuwa kulikuwa na tume isiyokuwa huru kusimamia uchaguzi .. yaani sawa na kumweka jambazi benki kulinda fedha na mali za wanachama/wateja...

yaani ikiwa katika mgongano huu wa kimaslahi tume ikikosa confidence in itself inakuwa kama jambazi sasa kulinda fedha... Hili likitokea katiba haipo tena, inavunjwa na kila mtu wa tume na waliyemfanya kushinda na hakushinda wanasema amina... sijui hata ikiwa inaleta maana dhahiri lakini naomba kuwakilisha.
 
Mkuu Tindo hoja ya Pascal kuwa mda uliobaki Ni mdogo Haina mashiko,hivi kupeleka mbele uchaguzi let say kwa miezi mitatu ili kupata time mpya na inayokubalika haiwezekani?hivi ikitokea Rais akafa siku tatu kabla ya Uchaguzi Mkuu ambae pia Ni mgombea,mda wa uchaguzi hautasogezwa mbele?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo sentensi ya mwisho ndiyo umeongea la maana. Na litokee!!
 
Back
Top Bottom