Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

Utumwa wa Tume ya Uchaguzi Tanzania: Wasemavyo Maaskofu wa TEC

Credit kwa majibu mazuri.

Nami itoshe kusema kuwa tatizo kubwa sana liko kwa watendaji kukosa huo uhuru wa kifikra kwa hisia, uoga, njaa na mengine mengi uliyoyataja.

Japo haya yanaweza kupunguzwa iwapo taasisi zitajengwa katika misingi huru inayolenga kutoa huduma zenye ufanisi mkubwa badala ya upendeleo wa kundi fulani.

Good analysis Mama Amon,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paschal Mayala anakosea kusema kuwa Tume ya Uchaguzi ni Huru lakini sheria ya uchaguzi ndio mbaya. Anashindwa kuelewa maana ya uhuru unaoongelewa. Katiba ya nchi na sheria mbaya ni baadhi ya vikwazo vinavyopunguza uhuru wa Tume.

Nini bado namtetea PM kwa misingi ya kuwa tume ya uchaguzi umeundwa kutokana na maelekezo ya sheria...na hata namna ya uendeshaji wake unatokana na misingi hiyo hiyo kisheria...sasa unapoanza kuikosoa tume bila kurudi nyuma na kuangalia ni sheria ipi inayoipa meno unakuwa unakosea....

Jambo la misingi ni kuomba sheria ifanyiwe marekebisho ili iwe vile tunavyotaka...
 
1584639127191.png
 
Sky Éclat . Hawa kina Membe ndiyo wale wale, wakiwa ndani ya system wanashindwa kuidhauri vizuri kiti. Kwa uhusiano aliokuwa nao na JK , alishindwa nini kumshauri waiache nchi ikiwa katika mfumo unaoeleweka na ulio fair kwa kila mwananchi ?!.

Akili zinawakaa sawa wakishakuwa nje ya mfumo, jambo ambalo halisaidii, kwani aliye na kiti anafaidika na ubovu uliopo .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini wao na si pamoja na wewe kama mwananchi mzalendo kwa taifa lake. Jukumu hili muhimu kwa wanao na wajukuu zako, kwanini iwe wao ?!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi najitoa siwezi kufanya kazi na upinzani wa Tanzania uliopo sasa sababu kuna unafiki na uyuda mkubwa sana walitufanyia washabiki na wanachama wake wanaojitambua mwaka 2015.
Naona upinzani huu ni nakala ya CCM.

Kuna watu tunafuata au tunaishi kwa kanuni na misingi flani, ikikiukwa na kupuuzwa tunajitenga na watu walio sababisha hivyo. Ukweli sipendi chama napenda sera na misimamo, napenda mtu mwenye misimamo, sera na itikadi flani.
 
Huo ni mtazamo mmoja, unaweza kuwa sahihi, lakini haumzuii muumini kuwa Mcha Mungu. Nikirudia ile cliché, hakuna binadamu aliyekamilika.

Hata hujajielekeza ktk jibu langu. Ni hivi:

-kumpenda mungu ni kutenda haki

- mtu huyu X anatenda haki

- kwa hiyo mtu huyu X anampenda mungu.

Kwenye nafasi ya X weka jina lako au la mtu baki kv JPM Je, hoja inabaki salama?
 
Mimi najitoa siwezi kufanya kazi na upinzani wa Tanzania uliopo sasa sababu kuna unafiki na uyuda mkubwa sana walitufanyia washabiki na wanachama wake wanaojitambua mwaka 2015.
Naona upinzani huu ni nakala ya CCM.

Kuna watu tunafuata au tunaishi kwa kanuni na misingi flani, ikikiukwa na kupuuzwa tunajitenga na watu walio sababisha hivyo.
Ukweli sipendi chama napenda sera na misimamo, napenda mtu mwenye misimamo, sera na itikadi flani.

Hoja iliyo mezani inahusu electoral managemnt bodies. Jielekeze huko
 
Hoja iliyo mezani inahusu electoral managemnt bodies. Jielekeze huko
Nikijielekeza kwenye mada husika, nadhani sina hoja zaidi ya kusisitiza tume huru na sheria ya uchaguzi safi.
Haya ni kati ya mambo ambayo wakati watu wengi wanashangilia matukio ya kupita nilikuwa nawasihi wapinzani washikie bango hoja hizo kabla ya kufika uchaguzi mwingine kuliko matukio yanayopita muda mfupi na kusahaulika kabisa.

Sisi ni watu wa zima moto, watu kama wewe mlitakiwa mje na michango mingi kama hii wakati ule huenda tungelikuwa tumeshapata tume huru, sheria safi ya uchaguzi na hatimae viongozi safi.

Kwa uzoefu wangu hapa unazima moto tu, labda haya unayopigia leo kelele yatatekelezwa na kusaidia uchaguzi mwingine sio huu wa 2020.
Ukianzishwa mchakato sasa unaweza kuwa na mapungufu mengi sana, na muda utakuwa kisingizio, mwishowe yatajirudia ya katiba mpya.

Viongozi wa dini kwa wakati ule walikuwa na nafasi kubwa sana kusukuma hoja (agenda) ya tume huru na sheria safi ya uchaguzi. Unakumbuka ule waraka wa maaskofu wa KKT ulivyotikisa watawala?
Pale pale wangepigilia misumari zaidi kuhusu hii hoja uliyoleta jukwaani.
Mimi naomba waongeze na mgombea binafsi.
 
Kwa uzoefu wangu hapa unazima moto tu, labda haya unayopigia leo kelele yatatekelezwa na kusaidia uchaguzi mwingine sio huu wa 2020.
Ukianzishwa mchakato sasa unaweza kuwa na mapungufu mengi sana, na muda utakuwa kisingizio, mwishowe yatajirudia ya katiba mpya.

Usikate tamaa haraka. Kuna utaratibu wa kupeleka miswada Bungeni kwa dharula. Mahitaji ni muswada wenye mabadiliko machache ya sheria ya uchaguzi na katiba. Kila kitu kinawezekana palipo na sauti nyingi za kudai mageuzi bila kujiuma uma midomo. Tusonge mbele. Liwezekanalo leo lisingoje kesho.
 
Mama Amon,
"kutenda haki" ni very subjective term, and is open to a wide variety of interpretations. Haki kwa mtu mmoja inweza kuwa kosa au jinai kwa mwingine. Kwahiyo syllogism yako ni batili sababu premise namba moja haisimami kipekee kama ukweli usiopingika.
 
Siyo mtu moja sasa !! Ni aslimia kubwa ya WaTz wanadai haki ya kuwa na chombo huru na si hii inayotishwa na kupewa maelekezo kutoka upande moja wa wagombea.

Na kama ulivyodai, kwao ni haki na huru kwa vile wanaweza kuichezea. Lakini kwa watu wengine si huru na haki. Kubwa inatakiwa chombo kinachokubalika kwa washindani wote. Ukumbuke tume hii iliundwa wakati wa mfumo wa chama kimoja kushika hatamu. Hivyo kuwa na mapungufu mengi kwa hali ya sasa. Leo ni vyama vingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi najitoa siwezi kufanya kazi na upinzani wa Tanzania uliopo sasa sababu kuna unafiki na uyuda mkubwa sana walitufanyia washabiki na wanachama wake wanaojitambua mwaka 2015.
Naona upinzani huu ni nakala ya CCM.

Kuna watu tunafuata au tunaishi kwa kanuni na misingi flani, ikikiukwa na kupuuzwa tunajitenga na watu walio sababisha hivyo.
Ukweli sipendi chama napenda sera na misimamo, napenda mtu mwenye misimamo, sera na itikadi flani.
Kujitoa napo ni unafki kama ulivyodai . Huwezi kutaka mambo mazuri kwa kukaa pembeni. Na makosa ya wadau wa miaka hiyo unayoisema, yalitakiwa kuwa funzo na hivyo kuja na kitu bora zaidi. Na kama hutasahau , miaka unayoitaja unashuhudia kuwa WaTz wapo tayari labda wa kuwaunganisha ndiyo hawapo.

Mwisho kuwa na sheria nzuri na tume huru si faida ya mtu moja wa leo. Bali ni kwa ajili ya watoto na wajukuu zetu. Tukijiwazia sisi tu, bila kuliwazia taifa hili siku za usoni, basi hatutafanikiwa kwa sababu za ubinafsi wa kuangalia nani anafaidika na mfumo mbovu uliopo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja niikopi hawachelewi kuifuta! hili bandiko limekaa poa sana. kuna watu wana kaa chini wanatenga siku kuandaa makala huku wengine tunaandika tukiwa kwenye daladala yaan fasta fasta tukitegemea kueleweka. Barikiwa sana mwandishi na mtafsiri wa ujumbe huu.
 
Back
Top Bottom