#COVID19 UVCCM: CCM imchukulie hatua Askofu Gwajima kwa kuhamasisha Watanzania kukataa chanjo ya Uviko-19
"Askofu Gwajima anahamasisha Wananchi wasiende kuchanjwa, ni utovu wa nidhamu kwa Serikali na kwa CCM, sisi Vijana wa CCM tunalaani vikali kauli zile na tunakiomba Chama Viongozi wa namna hiyo wachukuliwe hatua kali" :- Kenani Kihongosi, Katibu Mkuu UVCCM
Gwajima ana 'watu',mtaaibika bure.
 
Dodoma. Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM) umekitaka chama chao kumchukulia hatua Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima kwa kitendo chake cha kuhamasisha watanzania wakatae chanjo ya Uviko-19.

Katibu Mkuu wa UVCCM, Kenani Kihongosi ameyasema hayo leo Jumanne Julai 28 2021 mara baada kumalizika kwa kikao cha sektarieti ya UVCCM.

Amesema mbunge huyo ametoa maneno ya kichochezi na kwamba yanakwenda kuwagawa wananchi kwa sababu Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa msimamo kwa wananchi wapate chanjo.

“Sisi umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi kauli zile tunazipinga na kuzilaani kwa sababu utaratibu wa CCM kama mbunge ana jambo lake anapeleka kwenye party cocus (kamati ya wabunge wa chama),”amesema.

Amesema utaratibu alioutumia mbunge huyo wakwenda kutoa maneno hayo kwa umma, kwamba mtu atakayediriki kuwaambia watu wachanjwe atakufa ni utovu wa kinidhamu.

“Lazima atambue yeye sio Mungu anayetoa uhai ni Mungu. Tunakiomba chama chetu viongozi wa namna hiyo aachukuliwe hatua kali za kinidhamu na ajieleze kwanini anaongea maneno ya namna hiyo,”amesema

Source: Mwananchi
Dawa imeshaanza kuwaingia eeh! Zijibuni hoja alizoleta kama mnayo majibu!
UVCCM Gwajima anapigania usalama wenu ninyi msijitambua wadanganyika!
 
Ana watu gani?

Labda Mataga Kama wewe mnaoenda kanisani kwake kumsikiliza mkiwa na akili timamu au akilizenu huwa mnaziacha nyumbani?
Usikurupuke kujibu,siku nyingine utaabika. Itoshe tu kukuambia mimi siyo mataga. Tuheshimiane.
 
Hujui ulisemalo, kama Bashite tu aliweza kumlaza ndani sembuse serikali nzima ikiamua? 2015 aliwekwa ndani na Kikwete akazimia mahabusu! Mnapenda sana kuwaoverrate matapeli
Jambo usilolijua kwako ni sawa na usiku wa giza nene.
 
Aisee yaani mtu kaongea kanisani like a pastor na sio mwanasiasa wamuadhibu kwa lipi

And by the way hata wafanyeje chanjo mma
Ametoa tuhuma nzito kwa Serikali nzima kuwa wamevuta mshiko toka kwa mabeberu.
 
Ana watu gani?
Hawa wanaomsikiliza hapa...


Lugha ngumu sana hii, afadhali yule dhalimu wa fenti fod...bila shaka hata huko kuzimu ananena kwa lugha!
 
MH.GWAJIMA NA TUHUMA NZITO MNO......

Ukimsikiliza vyema katika ile CLIP yake kuna sehemu amerudia mara mbili kumtaja Hayati JPM...."kuwa ni kwanini Sasa chanjo ije baada ya JPM kuaga dunia....alipoaga dunia tu,chanjo zimekuja".....

Kauli hii ni ya hovyo kupindukia.....

Anataka AMCHAFUE RAIS SSH kwa "kumdogosha na kumfanya mwepesi kiuongozi" kwa kuwa HAYATI JPM ameacha LEGACY ya misimamo ISIYOYUMBA.....

MANENO HAYA NI MANENO MABOVU MNO KUTOLEWA NA MBUNGE TU DHIDI YA AMIRI JESHI WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA

#GwajimaAfukuzweCCM
#KaziIendelee
#TujiandaeKuchanjwa
#JMTMilele
Usalama wa raia kwanza! Hiyo chanjo hata hatuielewielewi!
Namuunga mkono Gwajima ktk hili 🤝!
 
UVCCM KUPITIA KATIBU MKUU UMOJA WA VIJANA WA CCM KENANI KIHONGOSI AWAONYA WANAOPOTOSHA K
IMG_20210726_081129_676.jpg
UHUSU CHANJO YA CORONA.


MwanaCCM

Kutokana na kauli mbalimbali zilizotolewa hivi karibuni na baadhi ya Viongozi na watu mbalimbali kuhusu Chanjo ya Uviko 19 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Ndugu Kenani Laban Kihongosi amezungumza na waandishi wa habari.

Katibu Mkuu amempongeza Mhe Rais kwa kazi kubwa anayoifanya bila kuchoka katika kuwahudumia Wananchi na kulinda Amani ya Nchi yetu, pia amewahakikishia Wananchi kuwa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wapo pamoja na Mhe Rais kuhakikisha adhma ya serikali ya Awamu ya sita (6) inatimia katika kuwaletea Watanzania Maendeleo.

Kwa upande wa wanaopotosha kuhusu Chanjo ya Uviko 19 Ndug Katibu amesema ""Kuna jambo pia naomba niliseme Juzi Kuna viongozi wameongea kuhusu Chanjo, Mbunge wa Kawe Gwajima ameongea maneno yasiyofaa kuhusu Chanjo ya Corona na Chanjo imeshaletwa, Sasa anapotokea Kiongozi wa mhimili mwingine anaenda kuwahubiria Waumini na kuwatisha watu kuwa wanaosapoti watakufa sasa Tumweleze kuwa anaetoa Uhai ni Mungu na anaechukua Uhai ni Mungu"

Pia Katibu Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi amesema wanalaani kauli hizo na wanaomba Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya Mbunge huyo.

Kwa upande mwingine Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Kenani Laban Kihongosi amesisitiza Watanzania kwenda kuchanjwa Kwa hiari yao na kuendelea kufanya mazoezi ili Taifa letu kupata watu wenye Nguvu na afya njema Kwa Maendeleo ya Taifa letu.

Mwisho amesisitiza Watanzania kumheshimu Mhe Rais kwa mamlaka aliyonayo na kuwakumbusha Watanzania wote kuwa Maendeleo yanayopiganiwa ni kwa Ajili ya Watanzania wote hivyo wanaopinga Maendeleo yanayofanywa waache mara Moja.

#UvccmMoto
#ChamaImara
#SerikaliMadhubuti
#KaziIendeleee
 
Back
Top Bottom