Sijapendezwa na midahalo inayoendelea mitandaoni nadhani sasa inavuka mipaka, kama vijana (UVCCM) yapaswa mjitafakari kuona haya mnayoyafanya yanaafya au lah! Kuweni na heshima kwa viongozi ndani ya chama, hayo ya kujibizana mitandaoni si desturi ya CHAMA CHA MAPINDUZI.
Niwaombe UVCCM wote, acheni tabia ya ku exaggerate mambo, tumieni njia ya heshima na busara kwenye kutatua changamoto zenu acheni kujibu hoja kwa kukurupuka. Pia mwenyekiti wa UVCCM Taifa wewe ndiye mwenye uwezo wa kutuliza haya yanayoendelea kwa wenzako.
My take:
Mpaka sasa sijaona kosa la Mh. Mchengerwa, Mh aliongea kama MLEZI pia kwa kuzingatia observation zake, jukumu la UVCCM ilikuwa ni kuyapokea na kuyafanyia KAZI badala ya kujibizana mitandaoni, ni ukweli usiopingika watu wanatanguliza masilahi zaidi badala ya kazi, ni jukumu la UVCCM Taifa kuwakanya watu wako waachane na hii tabia ya kujibizana mitandaoni na Viongozi wakubwa huu ni ukosefu wa nidhamu.