UVCCM haya yanayoendelea siyo sifa ni ukosefu wa nidhamu ndani ya chama. kiongozi wa UVCCM Taifa jitafakari

UVCCM haya yanayoendelea siyo sifa ni ukosefu wa nidhamu ndani ya chama. kiongozi wa UVCCM Taifa jitafakari

Mchengerwa ndiye aliyeanzisha. Akiwa kama Waziri wa Afya na Mbunge wa Rufiji, alisema hadharani kuwa rushwa imekithiri ndani ya UVCCM - viongozi na baadhi ya vijana hawafanyi kazi bila kuhongwa.

Kauli hiyo iliwaka moto kwenye mitandao na matawi ya UVCCM mikoani.

UVCCM wakamjibu:

1. Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohamed Kawaida - Oktoba 18: Akasema Mchengerwa kama mwanachama mtiifu afuate taratibu za CCM. Kama kuna tuhuma za rushwa, kuna vyombo na vikao vya ndani vya chama vya kuzishughulikia, sio kueneza hadharani ambazo zinaweza kuwa za kweli au si za kweli. Akasema kauli kama hizo zinawakatisha tamaa vijana wanaojitolea.

2. UVCCM Mikoa - Dar na Pwani: Mwenyekiti wa CCM Dar, Nasra Mohamed, akatoa onyo kali kwa kiongozi (akimaanisha Mchengerwa) anayetishia vijana wa UVCCM - "Tutakushughulikia na hatutakuogopa. Unataka upendwe na kila mtu? Kwani wewe umekuwa fedha?"

Na UVCCM Dodoma na Pwani wakasema Mchengerwa amewazingua, wanampenda kama shemeji yao (mume wa mtangazaji wa Planet Bongo) lakini kauli yake imewahusisha wote vibaya.

Kwa kifupi:

Mchengerwa anasema: UVCCM mna rushwa, mnataka pesa ndio mfanye kazi.

UVCCM wanasema: Kama kweli kuna rushwa lete ushahidi vikaoini, usituchafue hadharani, na wewe mwenyewe kipindi cha TAMISEMI ulijaza ndugu zako kwenye UDED na UDC.

Nani ni mkosefu wa nidhamu hapo?😂
Njia iliyotumika kujibu hoja Imekosa nidhamu
 
Chadema ni Chama pekee kinachoendeshwa kwa rushwa.
Wanachangisha watu bila kutoa mapato na matumizi, hii ni rushwa
We bwege nini?
Tunaongelea swala la rushwa NDANI ya CCM
Wewe unarukia Chadema.
Mchengerwa aituhumu UVCCM , sasa hapo Chadema wapi na wapi?
Ndio maana huwa nasema IQ ya makada wa leo ni tope kabisa.
 
Bado tunasubiri Nchengerwa achokonolewe tena atoboe siri nyingine kwamba ndio wanaowateka watu na kujifanya watu wasiojulikana kumbe wanajulikana mbali na rushwa hawa ndio wanaoongoza kwa kuteka watu, oya sijui watamfanyaje mimi naangalia kwa kutumia darubin yangu huku mbali
Mchengerwa kapiga kwenye mshono, na ndio maana unasikia vilio, hao madogo huwa wanajiona wao ndio wao
 
We bwege nini?
Tunaongelea swala la rushwa NDANI ya CCM
Wewe unarukia Chadema.
Mchengerwa aituhumu UVCCM , sasa hapo Chadema wapi na wapi?
Ndio maana huwa nasema IQ ya makada wa leo ni tope kabisa.
Chadema ndo rushwa ilikozaliwa. Eti chadema Hivi Ile Donation ya hanang mliwasilisha kwa wahanga
 
Back
Top Bottom