UVCCM yaomba radhi vijana, yaahidi kumpa ushirikiano Rais Samia Suluhu Hassan

UVCCM yaomba radhi vijana, yaahidi kumpa ushirikiano Rais Samia Suluhu Hassan

Libya

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2016
Posts
790
Reaction score
1,968
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umeomba radhi iwapo kuna mahali walitofautiana kimtazamo na makundi mengine na kutaka vijana wengi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika majukumu yake ya kuiongoza nchi.

Kauli hiyo ilitolewa jana Jumapili Machi 28, 2021 na mwenyekiti wa umoja huyo Taifa, Kheri James wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma akibainisha kuwa huu ni wakati wa kusamehe ya nyuma na kufungua ukurasa mpya wenye mambo yatakayokuwa na tija kwa Taifa.

“Inawezekana katika siasa zetu na hekaheka za kutofautiana kimitazamo yapo mambo ambayo huko nyuma yalipelekea umoja wetu ukatetereka, sisi kama umoja wa vijana hatuoni aibu kusema tunaomba radhi kwa hayo kama tuliyatenda na tupo tayari kuyarekebisha ili kutengeneza jukwaa safi kwa rais wetu kuanza upya akiwa na watu walioshikamana ili nchi yetu iweze kwenda mbele.”

“Vijana wa nchi hii ndio watakuwa wanufaika wa kwanza Serikali ikiwa imara na vijana wa nchi hii ndio watakaokuwa wahanga wakubwa nchi ikiwa dhaifu.”

“Kwa hiyo ninasisitiza vijana tunahakikisha maneno na matendo yetu yanafanana na dhamira ya rais wetu ili kumrahisishia kazi yake mpya aliyopewa ya kutuongoza kama mkuu wa nchi ili sisi tuwe ni nguzo ya umoja, mshikamano na maendeleo ya nchi yetu,” amesema James.

Kweli maisha yanaenda kasi sana, Kheri James leo anaongea maneno kama kanyeshewa na mvua.

 
Huyu KIJANA na wenzake kauli zao na utendaji wao wa kisifasifa umeumiza watu wengi sana na kuongeza idadi ya waliokichukia CCM. Aidha wengi walijiunga nao huku mioyoni wana mambo yao wakimuomba Mungu awasamehe waishi vile wapendavyo hawa. Binafsi sikupendezwa na ubabe na kauli zao. Hapa anawataja act waishi anajua kabisa CHADEMA ndicho Chama chemie VIJANA wengi tena huenda kushinda CCM ambacho kimekusanya VIJANA wenye tamaa na matarajio ya uongozi tu tena wa Mtindo wowote ule. Ushiriki wenu kuathiri chaguzi kibabe unawanyima kibari mbeleni ZA Mungu wenu. Jitahidi kubadilika sana
 
Back
Top Bottom