UVCCM yaomba radhi vijana, yaahidi kumpa ushirikiano Rais Samia Suluhu Hassan

UVCCM yaomba radhi vijana, yaahidi kumpa ushirikiano Rais Samia Suluhu Hassan

Waliouliwa na kuumizwa kuharibiwa mali zao waanze kwanza kuwapmba radhi hadharani vinginevyo sisi tupo ma mama tu wao waendelee na mikakati yao ovu.
 
Waliouliwa na kuumizwa kuharibiwa mali zao waanze kwanza kuwapmba radhi hadharani vinginevyo sisi tupo ma mama tu wao waendelee na mikakati yao ovu.
 
Huyu ndio aliyesema safari hii (uchaguzi mkuu 2020) kwamba hawatatumia nguvu nyingi (Kwa Tundu?) ni SINDANO TU ( ya sumu) psiiiiiiiiii!!

Atavuna alichokipanda!
 
Kila zama na kitabu chake bwashee!

Hapo bado David Kafulila aka tumbili anatunga mistari !
Bado wewe na walamba makalio wenzio wa humu mtandaoni hasshasa humu JF
Screenshot_20210329-122110.png
Screenshot_20210329-122949.png
 
Ulipokuwa ukiwatenda wenzio vibaya, haukujua madhara yake? Tumeumia vibaya sana na wengine mliwapoteza! Je, Uko tayari kuwarudisha?
 
Huyu hakushinda nafasi hio ya uenyekiti alishinda kwa maagizo ya mjomba.Msamaha pekee ni ajiuzuru nafasi hio.Walijimilikisha chama toka cha wakulima na wafanyakazi ni kuwa mali binafsi ya familia.Mjomba mwenyekiti,mpwa mwenyekiti,maamuzi ni yao kununua wapinzani, kurejea chaguzi,kuvuruga chaguzi,nk.Ni Kati ya watu walioibip the hague.
Uzuri technology utunza historia
Mjomba alimuandaa ili awe kiongozi wa baadae. Mjomba hakuwa na historia na chama ila alimuandalia mpwa historia .
 
Ulipokuwa ukiwatenda wenzio vibaya, haukujua madhara yake? Tumeumia vibaya sana na wengine mliwapoteza! Je, Uko tayari kuwarudisha?
Waende jela wakae miaka kusubiria ushahidi kukamilika kama walivyowatendea wenzao
 
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umeomba radhi iwapo kuna mahali walitofautiana kimtazamo na makundi mengine na kutaka vijana wengi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika majukumu yake ya kuiongoza nchi.

Kauli hiyo ilitolewa jana Jumapili Machi 28, 2021 na mwenyekiti wa umoja huyo Taifa, Kheri James wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma akibainisha kuwa huu ni wakati wa kusamehe ya nyuma na kufungua ukurasa mpya wenye mambo yatakayokuwa na tija kwa Taifa.

“Inawezekana katika siasa zetu na hekaheka za kutofautiana kimitazamo yapo mambo ambayo huko nyuma yalipelekea umoja wetu ukatetereka, sisi kama umoja wa vijana hatuoni aibu kusema tunaomba radhi kwa hayo kama tuliyatenda na tupo tayari kuyarekebisha ili kutengeneza jukwaa safi kwa rais wetu kuanza upya akiwa na watu walioshikamana ili nchi yetu iweze kwenda mbele.”

“Vijana wa nchi hii ndio watakuwa wanufaika wa kwanza Serikali ikiwa imara na vijana wa nchi hii ndio watakaokuwa wahanga wakubwa nchi ikiwa dhaifu.”

“Kwa hiyo ninasisitiza vijana tunahakikisha maneno na matendo yetu yanafanana na dhamira ya rais wetu ili kumrahisishia kazi yake mpya aliyopewa ya kutuongoza kama mkuu wa nchi ili sisi tuwe ni nguzo ya umoja, mshikamano na maendeleo ya nchi yetu,” amesema James.

Kweli maisha yanaenda kasi sana, Kheri James leo anaongea maneno kama kanyeshewa na mvua.

Kama kweli anamaanisha basi option nyepesi kwake ilikuwa ni kujiuzulu ili amtengenezee mama mazingira mazuri ya kazi yasiyo na makunyanzi. Anasema ‘inawezekana’ hekaheka zao zilipelekea umoja wa vijana kutetereka. Inaonekana hana uhakika au ni mnafiki. Ukweli ni kuwa kauli na ‘maagizo’ yake yamepelekea si mpasuko tu baina ya vijana, bali yameacha wengi kuwa wahanga. Huo msamaha anaouomba uendane na uwajibikaji. Vipi kuhusu walioumizwa wanafidikaje na huo msamaha ambao ni kama ameshajisamehe (kwa maneno yake mepesimepesi... eti hatuoni aibu kuomba radhi). Kirahisirahisi hivyo????[emoji15][emoji15][emoji15]
 
Misamaha mingine huambatana na uwajibikaji na siyo maneno matupu!

Hata kwenye Biblia kuna watu ambao ili msamaha wao ukubaliwe ilibidi wakubali sharti la kwenda kufanya marejesho mara 4 ya kile walichodhurumu watu.

Je madhara ya makosa yao ni makubwa kiasi gani?

Mfano wengine kusababishiwa ulemavu wa kudumu, vifo, wategemezi, kupoteza haki ya kushinda uchaguzi huru wa kuchaguliwa na wanachi n.k.

Yatupasa kutafakari sana.
 
"Sasa hivi hatupigi risasi tunachoma sindano ya sumu " Hii kauli yake naijumbuka mpaka leo.
 
Back
Top Bottom