Naomba niwashauri idara yetu nyeti ya TISS kuhusu jinsi mnavyomfuatilia Kigogo2014 ili kumweka mikononi mwenu kwa sababu ya kutoa siri nzito nzito za Serikali.
Niwaeleze ukweli kwamba, Kigogo2014 hamuwezi kumkamata hata iweje kwa sababu Kigogo siyo mtu mmoja bali ni syndicate kubwa ndani ya syndicate nzito na yenye nguvu kubwa.
Inasemekana zimetumika zaidi ya Bil 1.4 kumsaka Kigogo, mmeshindwa kubaini ukweli na badala yake mnazidi kupoteza pesa za umma kumsaka mtu ambaye hamuwezi kumpata.
Ujio wa Kigogo umesababishwa na uwepo wa utawala mbovu, unaominya haki za Binadamu Uhuru wa Habari, Demokrasia na uharibifu mkubwa wa uchumi.
Badala ya kujikita kwenye kuleta maendeleo, awamu ya Tano imetumia Pesa za umma kununua wapinzani na kuvuruga Demokrasia.
Ajira ya TISS imejikita zaidi kwa vijana wa UVCCM na siyo kwa intelligence experts, sasa watu Kama hao watawezaje kumpata mtu mwenye level ya Mossad na CIA?
Uongozi hauhitaji mabavu bali hekima, unapoamua kuwa mbabe na kwa sababu unawaongoza siyo mbuzi, ni watu wenye akili zao, tarajia kukutana na ma whistle-blowers wengi.
Na mwisho wa siku utashindwa tu, tatizo lenu mnatumika kisiasa sana, yaani mpo kwa ajili ya kuhakikisha CCM inatawala milele na siyo kwa ajili ya ustawi wa nchi.
Awamu hii hii ya Tano inayosifika kwa kukamata wakwepa kodi, kuna kampuni nyingi tu nazijua na nina ushahidi mkubwa kuwa zinakwepa kodi. Ajabu eti serikali makini haijui, ila serikali hiyo hiyo inajua ni lini Mbowe atafanya mkutano wa ndani ili waweze kumdhibiti asichafue amani ya nchi, kichekesho kweli.
Kama Trilioni 1 ilipotea na CAG akatolewa kwa kusema ukweli, basi acha watu wakwepe kodi. TISS wapo bize kuwarekodi kina Steve Nyerere wakiigiza sauti ya Mbowe anamnyanyapaa kimapenzi mbunge wa Chadema (jina linahifadhiwa)
Yaani badala ya kufanya mambo ya msingi kwa Taifa mnatumika na mambo ya hovyo, baada ya Kigogo kuwavua nguo huko Twitter sidhani kama bado mnaendelea tena na hujuma dhidi ya Mbowe.
Fanyeni ishu za maana kwa Taifa, acheni roho ya usaliti kwa Taifa, vinginevyo mtadukuliwa mno.
Long live Kigogo2014.