Uwanja wa Mkapa ni eneo gani mtu akikaa anaona mechi vizuri kuliko maeneo mengine?

Uwanja wa Mkapa ni eneo gani mtu akikaa anaona mechi vizuri kuliko maeneo mengine?

Sisi watu wa nje ya Dar es salaam hatujui majukwaa ya uwanja wa Mkapa yalivyopangiliwa, hivyo kuuliza si ushamba😃

Ni eneo gani ukiwa kwa Mkapa ndiyo unaweza kuona mechi vizuri zaidi kuliko maeneo mengine ya uwanja huo wa Mkapa?
Huo uwanja wenyewe nimekuja kuuona kwa macho tena kwa nje mwaka Jana mwezi wa 10, 🤣 kumbe umepakana na uwanja wa uhuru ambao nauskiaga tu.
 
Ni kweli mashabiki wanakuwa mbali na pitch hata ukikaa kule mbali kwenye mzunguko sometimes unakuwa na uoni hafifu, Azam sasa hivi washaanza kuweka viti na pameanza kupendeza lakini kwa Mkapa kuna mashabiki wanaangalia mechi zaidi ya umbali wa mita 100
Kwa umbali huo sidhani kama naweza vutiwa kwenda uwanjani. Labda kwa ajili ya socialization na sio burudani
 
Kwa umbali huo sidhani kama naweza vutiwa kwenda uwanjani. Labda kwa ajili ya socialization na sio burudani
Kabisa. Heri kuangalia kwenye TV na replay tunapata😆😀😃
 
Pale kinachoonekana kuna upendeleo kwa kujuana,kuna waheshimiwa hawakati ticket au hata wakikata ni za mzunguko ila wanaenda kukaa kule,maana idadi ya seats zinajulikana na kama watu wamekata zikaisha haiwezekani kuongeza sasa inakwaje watu wanazidi kuliko viti?
Huo nao ni ujinga mwingine. Mtu wamepromote tickets since day 1. Mimi shabiki nimekata mapema kabisa siku 7 kabla ya mechi halafu siku ya mechi nakuta kuna kifutu kakaa na hajalipia VVIP. hii haipendezi
 
Ila utaratibu wa kuingia uwanjani ni mbovu wauangalie na wale jamaa wamachinga sijui wawekewe utaratibu maalumu.

Muda wote kazi ya kukunja miguu kuwapisha.

Mi nawaambieni pale airport pasingekuwa na ulinzi mngeuziea maji ya kunywa na sambusa dirishani nawangekuwa wanaikimbilza ndege hafi inapaa..
 
Kwa uwanja wa Taifa,labda ukae kwenye viti vya benchi la fundi na wachezaji wa akiba.
Au ndiyo maana watu wengi siku hizi badala ya kwenda kwa Mkapa wanabaki vibanda umiza na majumbani mwao kuangalia mechi?
 
Sisi watu wa nje ya Dar es salaam hatujui majukwaa ya uwanja wa Mkapa yalivyopangiliwa, hivyo kuuliza si ushamba😃

Ni eneo gani ukiwa kwa Mkapa ndiyo unaweza kuona mechi vizuri zaidi kuliko maeneo mengine ya uwanja huo wa Mkapa?
Nyuma ya mabenchi ya ufundi ila kaa juu kidogo.
 
Sehemu yeyote utakayokaa utaona vizuri eneo lile litakalokuwa na uwiano mzuri na macho yako..!

Mfano Aliyekaa karibu na goli La mashariki ataona vema matukio ya hapo golini kumshinda aliyekaa VVIP
Kumbe mwelekeo wa pitch ni kutoka mashariki kwenda magharibi na si kusini kwenda kaskazini....

Sikujua hili maana bado sijafika huo uwanja kwa ndani
 
Kuna raha sana kuangalia mpira live pale kwa mkapa. Kama umezoea kuangalia kwa tv af uingie uwanjani unaweza dhani wachezaji hawako serious kumbe wako serious.

Af uwe na earphones uwe unasikiliza matangazo kwenye radio🔥🔥
Mkuu kwani inakuwaje kuwaje..
 
Wengi jiji la Dar huwachanganya sana uelekeo wa pande za dunia.

Nadhani huyo kaskazini ndiyo anaona kuwa ndiyo mashariki yake.
Yaani dar ukiwa ubungo kaskazini kwingine,ukienda mabibo ndanindani kaskazini kwingine kabisa,ukienda yombo ndiyo utachoka,na jua tu huwa lina muelekeo wa ajabu ajabu siyo kama mkoani
 
Back
Top Bottom