Uwanja wa Uhuru | Vodacom Premier League (VPL), Simba SC dhidi ya Singida United

Uwanja wa Uhuru | Vodacom Premier League (VPL), Simba SC dhidi ya Singida United

Kipindi cha pili kimeaanza Uwanja wa Uhuru,

Mabadiliko kwa Simba, Mkude anakwenda nje, ameingia Shiboub

Kapombe amekwenda nje, ameingia Gadiel Michael
 
Wanachokifanya Simba leo wananikumbusha miaka ya nyuma Mtaani tulisikia kishindo cha gobore, tukakusanyika pale kulikotokea mlio tukamkuta Mzee jirani anatoka na Nyoka mdogo kwenye fimbo anaenda kumtupa.
 
53' Singida wanapiga faulo kulee, golikipa Manula anatokea na kudaka mpira ule

Ametoka John Bocco ameingia Gerson Fraga Viera, upande wa Simba
 
Anakwenda Gadieeeeel, refa anasema mpira ulikuwa umetoka, wanapiga mbele Singida Utd mbele kuleee
 
Aishi Manula yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kumpigwa kiwiko Haruna Moshi wakati mpira wa kona ukipigwa kuelekea Simba

Anaonyeshwa Kadi Nyekundu moja kwa moja, Singida wapo pungufu sasa
 
Shibouuuuub Goooooooooooooooooooaaal

Akiwa eneo la D anapiga shuti na kuiandikia Simba bao la saba, hiii ni kalamu ya mabao

Simba SC 7-0 Singida Utd
 
66' Simba wakitawala mchezo huku Singida wakiwa hawana hata matarajio ya kupata bao, kutokana kutopanga vema mipango yao

Simba SC 7-0 Singida Utd
 
Back
Top Bottom