UWATA wamesambaratisha familia yetu

Naomba unipe guidance naweza tumia njia zako
 
Endelea kuwatetea maana hayajakufika
 
We jamaa mtu kama sio mwana-UWATA unaonekana kama shetani mbele yao, sasa upendo gani huo walionao
 
Endelea kuwatetea maana hayajakufika
Dawa,nimeongea kwa nijuavyo ,ninavyo jua wale hawafungishi ndoa,ingawa sina hakika,
Nahisi familia yenu ina shida pahala,na kabda ya ndoa na wasiwasi hamkuwa pamoja,
Kwa sababu hoja kubwa ni ndoa mpya!!?ila je ndoa ilikuwepo kabda?
Ila kuhusu mavazi kwa kweli unawaonea wanavaa vzr mno ,hawana mambo mengi ingawa wanaitana wapendwa na wanaumoja sana
 
Kusali watu 50 mbona ni jambo la kawaida .. TAFES wanasali hata watu 100 TYCS, ASA.. vivyo hivyo.


Kwa habari ya kusali kwa makelele kila mtu ana mtazamo wake kuhusu kelele. Hivyo kwa kusali kwao kwa namna uiitayo kelele haimaanishi ndio ubaya. Au wataka kila mtu kusali utakavyo wewe? Si ndo kutaka kupotosha watu huko ndugu.


Kwa habari ya kunyonya matajiri, fafanua wananyonywaje.

Ushauri watafute hao wanauwata ufanye utafiti maana huwajui kabisa.
 
We jamaa mtu kama sio mwana-UWATA unaonekana kama shetani mbele yao, sasa upendo gani huo walionao
Hebu nifafanulie nami nijue jamaa .. maana nataka kujua wakoje. Kwa namna gani wanakuona shetani. Usizungumze hisia lakini nahitaji useme kweli.
 
Masukila siku hizi inafaulisha?? Chini ya fubile? Japo simjui namsikia tu toka kyela sekondari
 
Sizungumzii kusali
Nazungumzia kuwa huishi nyumba moja watu lukuki!!

Nenda mbeya utawakuta wapo kibao saaaana

Hawa jamaa wanajifanya wanaumoja lakini behind the scenes ni wanyonyaji,
Wakikumata mwenye hela watahakikisha umebaki mtupu, utauza hadi ndoo ili upeleke hilo group liishi

Wanazaliana mno mpaka kero,
Unakuta ndoa ina miaka 10 afu Wana watoto watano na mimba ya sita
 
Dini ni nusu ya uchiziπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ niliacha kwenda makanisani miaka minne sasa kwa sababu ya kuwa na watu wajinga wajinga tu na imani za uongo uongo
 
bado watu wanaamini mambo ya dini hadi leo
 
Hizi ni chuki kuzaa,ni mihamu yako na Kukosa elimu ya uzazi,
 
uwata ndio wale wanaotuhumiwa wamama kutovaa vyupi? wanavaa magauni kama siku ya sikukuu kijijini, wanajitesa sana ila hawafuati njia sahihi ya kumwona Mungu. uwata ni cult.
 
Mimi hapa nilikuwa UWATA japo sasa hivi nakunywa bia. Ulichozungumza mtoa mada napata ukakasi kwa sababu UWATA kama UWATA hawana mamlaka ya kufungisha ndoa bali utafungia kwenye kanisa lako mama.
UWATA wanakutanika faragha kila siku na kufundishana neno la Mungu ili kutimiza andiko lililoandikwa "kutanikeni kila siku maadamu iitwapo leo"
 
U
UKaasi sio?
 
Hebu nifafanulie nami nijue jamaa .. maana nataka kujua wakoje. Kwa namna gani wanakuona shetani. Usizungumze hisia lakini nahitaji useme kweli.
Sio hisia wewe kama sio mpendwa wewe unaambiwa ni wa duniani sasa mi nikajiuliza wenyewe ni wawa wapi uzuri nimekaa nao hata salamu zao za kukumbatiana nazijua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…