No offence, agreed.
Ingawa mtoa mada hajabainisha facts za kutosha ila nitajaribu kumuongoza kwa namna ninayoijua kwa kumpa open ended suggestions.
Bilashaka alivitoa pesa nusu waliandikishiana (express term), if not, hata barua aliyoiandika wakamjibu kwa kutaka kumpa makubaliano mapya ni kielelezo tosha pia kwamba walishapokea pesa kutoka kwa mteja wao (implied term).
In law, there is a doctrine of estoppel, kwamba baada ya makubaliano kufanyika (expressly or impliedly), hakuna upande unaruhusiwa kurudi nyuma na kutengeneza makubaliano mapya isipokuwa kwa maridhiano ya pande zote mbili.
Aanze kwa kuandika demand notice and intention to sue, which is mandatory before commencing a civil suit, asiandike mwenyewe aende akaandikiwe kitaalamu na Wakili, awape labda siku 14 au zaidi kwa namna atakavyoona inafaa, wakishindwa kutekeleza kama walivyokubaliana ndiyo afungue kesi Mahakamani.
Kwa nature ya kesi ilivyo, atashinda. Lkn kwa uzoefu wangu, Makampuni mengi yakiandikiwa demand notice huwa yanamuita mteja kwenye meza ya mazungumzo.
I humbly submit. Ushauri nilioutoa hapa bure ningekuwa ofisini ningepata 10K ila hii ni sadaka yangu kwenu wana JF. Siku yenu na ikawe njema wakuu.