Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Siwezi kudhibitisha vip wakati ata wewe unaona kila mtu ana Mungu wake kichwani , kilichobaki ni kushawishiana tu kila mtu aone wa kwake ni bora kuliko wa mwingne , vitu virahisi unafanya viwe vigumu mkuu.
Kila mtu kuwa na Mungu wake Kuna sababu anuai.

Miongoni mwa sababu hizi ni :

1. Ujinga
2. Matamanio ya nafasi
3. Kuukataa ukweli

Hili kwenye Historia limedhibitiwa na liko wazi.
 
Hili tumeshalifanya zaidi ya mara kumi humu. Ila nyinyi mnao dai hayupo ndio hamuwezi kuthibitisha hilo.

Labda tuanzie hapa, kwako wewe uthibitisho ni nini na ili uthibitisho uwe uthibitisho unatakiwa ukidhi vigezo gani ?
Mungu mwenye upendo wote , anajua maisha ya kila kitu , anaepanga kila kitu kabla hakijatokea , anaechoma watu baada ya yeye kupanga kila kitu , hayupo.

Udhibitisho wa yeye kutokuwepo upo dhahiri bila kuitaji mahubiri, bali ushawishi wa kuwa yupo unahitaji mahubiri yenye vitisho na ahadi nyingi.
 
Mthibitishe huyo mungu wako ambae yupo nje ya biblia na korani.
 
Kila mtu kuwa na Mungu wake Kuna sababu anuai.

Miongoni mwa sababu hizi ni :

1. Ujinga
2. Matamanio ya nafasi
3. Kuukataa ukweli

Hili kwenye Historia limedhibitiwa na liko wazi.
Kwamba ukwel wa Mungu ni upi , ivi unafahamu hata wa dini yako pale anapofanya imagination ya Mungu kichwani kwake ni tofauti na wewe na mwingne?
 
Mthibitishe huyo mungu wako ambae yupo nje ya biblia na korani.
Ata humo ndni ya hivyo vitabu ni jamaa fulani tu mwenye sifa, kiburi ,hasira ,ubaguzi , na mzee wa lawama.
 
Abu Huraira (god be pleased with him) relates that the messenger of God (peace be upon him) said ;God does not look at your bodies and your shapes, He looks at your heart; (Muslim) So hiyo wala hainipi shida endelea kuamini unacho kiamini
Umejuaje kwamba kila mtu anaamini.
 
Nikifa anaenda wapi?
 
Isaya 26:3-4

3 Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.

4 Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele.
Hayo ni mahubiri ya imani na si fact
 
Biblia inasema Mungu ni Mungu wa wivu na hasira na anaadhibu hadi kizazi cha nne. Hiyo kusema sio mwingi wa hasira umelitoa wapi?
 
Wewe mwanao uliemzaa akikukosea huwezi ku

Nawewe si ulijua utazaa watoto, watoto wako wakikukosea huwezi kuwaazibu kwa maneno au kwa vitendo?
Wewe hujawahi piga hata mtoto wako?
 
Na wewe tofautisha kati ya "piki" Na "pili" Umesema mwenyewe kila mtu aachiwe aamini anavyotaka sasa mbona unahoji imani za watu?

Wewe kuna siku tulikuambia ututhibitishie huyo mungu wako unayemuamini? Sisi tunaoamini uwepo wake mbona huwa hatuhoji kile ninyi mnachoamini na kama ni hivyo na sisi tutaomba maandiko ya kile mnachoamini.

Unapohoji imani ya mtu huwezi pata chochote maana imani huwa ni mtu na roho yake, japo inaweza kuzihirika kwa mtu kuonyesha matendo yake.
 
Wewe mwanao uliemzaa akikukosea huwezi ku



Nawewe si ulijua utazaa watoto, watoto wako wakikukosea huwezi kuwaazibu kwa maneno au kwa vitendo?
Wewe hujawahi piga hata mtoto wako?
Mimi si Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote.

Hivyo, mfano wako umenipa kazi kubwa kuliko uwezo wangu kwa mlinganisho na Mungu.

Ningekuwa Mungu huyo, ningeumba ulimwengu ambao watu hawakosei.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na mwenye upendo wote kuumba ulimwengu ambao watu wanaweza kukosea ni contradiction.
 
Mimi sihoji imani ya mtu, imani unaruhusiwa kuamini chochote, cha ukweli au hata uongo.

Mimi najadili ukweli uko wapi, hili ni jambo zaidi ya imani tu. Ukweli unaweza kuwa tofauti na imani.

Unaelewa tofauti hii?
 
Wewe unaamini Mungu yupi?
 
Mimi sihoji imani ya mtu, imani unaruhusiwa kuamini chochote, cha ukweli au hata uongo.

Mimi najadili ukweli uko wapi, hili ni jambo zaidi ya imani tu. Ukweli unaweza kuwa tofauti na imani.

Unaelewa tofauti hii?
Kubali kwanza unahoji imani ya mtu maana mtu ndio anaeamini uwepo wa Mungu wake?
 
Mtu hakosei bali tamaa yake ndio inampelekea kukosea, binafsi naelewa miili yetu hii ni kama chombo kinachoendeshwa tu ambacho kinapokea nguvu toka pande mbili
1. Shetani
2. Mungu
Ukimuamini mmojawapo matendo yako yataendana na upande huo japo kuna watu wanakuwa vuguvugu kwamba kila upande yupo.
Ndio maana ukitaka kufanya jambo kuna imani mbili huwa zinapingana kimoyomoyo hio ni tosha inazihirisha uwepo wa pande mbili zinazopingana

Ila kwake kila goti litapigwa kuna mda na wakati utamuhitaji na utamtafuta sana naomba Mungu aachilie neema yake ya kumjua zaidi na wala wakati huo hautahoji haya maswali yako.
 
Kwa nini Mungu kaumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na Shetani na uovu, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hauwezi kuwa na shetani wala uovu?
 
Kubali kwanza unahoji imani ya mtu maana mtu ndio anaeamini uwepo wa Mungu wake?
Hapana, sihoji imani.

Imani unaruhusiwa kuamini chochote, Allah, Buddha, Jehovah. Unaruhusiwa kuamini hata uongo wowote utakaotaka. Ni haki yako. Huko sitakuingilia.

Ukisema mimi naamini Jehovah kama Mungu wangu, halafu serikali ikaja na kusema tunafuta dini, tunafuta haki ya watu kuamini dini zao, nitaungana nawe kutetea haki yako ya kuamini unavyotaka, nitapingana na serikali.

Hata kama mimi sina dini, natetea haki za watu kuamini wanavyotaka, au kutoamini kabisa.

Hivyo, mimi sihoji imani. Imani ni kitu cha faragha ya mtu binafsi kinachotetewa na katiba na haki za watu.

Ila, ukija hapa JF na kusema, mimi najua ukweli kwamba Jehovah ndiye Mungu, yupo, hiyo ni statement ya fact, ushavuka imani, umetoka nyumbani kwako, umetoka kanisani kwako, umekuja JF public square kusema Mungu yupo kama fact, hiyo si imani tena, hapo tunajadili fact. Hapo ndipo nakubana uthibitishe Mungu yupo kama fact.

Unaelewa tofauti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…