Hoja yako ya kwamba nani kaweza kutengeneza mbingu yake, na kama hakuna, kitu ambacho anakifanya Mungu mtu hakiwezi, kwa kuanzia, ina makosa ya kimantiki.
Logical fallacy. Logical non sequitur.
Ukweli kwamba mtu hajaweza kutengeneza mbingu yake unathibitisha kuwa mtu hajaweza kutengeneza mbingu yake.
Ukweli kwamba mtu hajaweza kutengeneza mbingu yake, hauthibitishi Mungu yupo kweli. Thibitisha kuwa Mungu yupo kweli.
Yani ni hivi, mimi nikishindwa kutengeneza filamu kama ya James Bond 007, hilo halithibitishi kwamba James Bond 007 yupo kweli.
Ukweli kwamba mimi siwezi kutengeneza filamu ya James Bond unathibitisha tu kuwa mimi siwezi kutengeneza filamu ya James Bond. Inawezekana kabisa nikawa siwezi kutengeneza filamu ya James Bond, na James Bond akawa hayupo, ni muhusika wa kufikirika tu wa riwaya na filamu, nje ya riwaya na filamu hizo hayupo.
Vivyo hivyo, inawezekana kabisa mimi nikashindwa kutengeneza mbingu yangu, na Mungu akawa hayupo. Hakuna contradiction wala logical inconsistency hapo.
Mimi kushindwa kufanya chochote hakuthibitishi Mungu yupo, kunathibitisha nimeshindwa kufanya hicho kitu.
Ukiunganisha mawili haya ambayo hayana uhusiano, unaanxa hoja kwa kufanya logical fallacy ya logical non sequitur.
Actually, mtu anaweza kusema kuwa ukweli kwamba hakuna mtu aliyeweza kutengeneza mbingu yake, unathibitisha Mungu hayupo.
Kwa sababu, Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na ujuzi wote, angekuwepo, angeruhusu kila mtu awe na uwezo wa kutengeneza mbingu yake. Mungu huyo si mchoyo wa neema. Angetupa tu neema hiyo ambayo yeye haimgharimu kitu.
Kwa hivyo, ukweli kwamba hakuna mtu aliyeweza kutengeneza mbingu yake, unaonesha Mungu huyo hayupo.
Hoja yako ukiitazama kijuujuu, utaona inaonesha Mungu yupo.
Lakini, ukiichambua kwa kina, utaona inaonesha Mungu hayupo.