Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Uwepo wa Mungu unadhihirika kwa alama zake na viumbe vyake

Siwezi kudhibitisha vip wakati ata wewe unaona kila mtu ana Mungu wake kichwani , kilichobaki ni kushawishiana tu kila mtu aone wa kwake ni bora kuliko wa mwingne , vitu virahisi unafanya viwe vigumu mkuu.
Kila mtu kuwa na Mungu wake Kuna sababu anuai.

Miongoni mwa sababu hizi ni :

1. Ujinga
2. Matamanio ya nafasi
3. Kuukataa ukweli

Hili kwenye Historia limedhibitiwa na liko wazi.
 
Hili tumeshalifanya zaidi ya mara kumi humu. Ila nyinyi mnao dai hayupo ndio hamuwezi kuthibitisha hilo.

Labda tuanzie hapa, kwako wewe uthibitisho ni nini na ili uthibitisho uwe uthibitisho unatakiwa ukidhi vigezo gani ?
Mungu mwenye upendo wote , anajua maisha ya kila kitu , anaepanga kila kitu kabla hakijatokea , anaechoma watu baada ya yeye kupanga kila kitu , hayupo.

Udhibitisho wa yeye kutokuwepo upo dhahiri bila kuitaji mahubiri, bali ushawishi wa kuwa yupo unahitaji mahubiri yenye vitisho na ahadi nyingi.
 
Tunapaswa kuelwa kuwa Kujadili na kubishana juu ya Imani zetu ni kúpoteza muda, Amini unachoamini lakini usisahau kuushrikisha ubongo wako. Sio Kila kitu kinachohubiliwa kwenye Imani zetu ni sahihi, wakati mwingine inategemeana na nyakati na mazingira tunamoishi. Hizi dini zililetwa na wageni Kwa sababu zao, mojawapo ni kueneza utamaduni wao . Mfano mavazi lugha n.k.Mungu yupo na atendelea kuwepo hata kama sio kutoka Kwa Imani za wazungu au waarabu.
Mthibitishe huyo mungu wako ambae yupo nje ya biblia na korani.
 
Kila mtu kuwa na Mungu wake Kuna sababu anuai.

Miongoni mwa sababu hizi ni :

1. Ujinga
2. Matamanio ya nafasi
3. Kuukataa ukweli

Hili kwenye Historia limedhibitiwa na liko wazi.
Kwamba ukwel wa Mungu ni upi , ivi unafahamu hata wa dini yako pale anapofanya imagination ya Mungu kichwani kwake ni tofauti na wewe na mwingne?
 
Abu Huraira (god be pleased with him) relates that the messenger of God (peace be upon him) said ;God does not look at your bodies and your shapes, He looks at your heart; (Muslim) So hiyo wala hainipi shida endelea kuamini unacho kiamini
Umejuaje kwamba kila mtu anaamini.
 
Mungu yupo kweli... ila sio mungu wa kwenye quran wala biblia, MUNGU yupo ndan yako, wewe ni sehem yake na huna haja yakwenda kumuomba mahali maalum ila popote wkt wowote.. tatz ata hao wanaokubali kuwa mungu yupo bado hawajamjua vzur wao kama wao ila wamekaririshwa.. haitakiwi ukaririshwe unatakiwa umjue, cku ukijijua vzur ww n nini ndiyo siku utakayomjua mungu ni nan
Nikifa anaenda wapi?
 
Isaya 26:3-4

3 Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.

4 Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele.
Hayo ni mahubiri ya imani na si fact
 
Kwanini kumekua na wimbi kubwa sana mnaekosoa uwepo wa Mungu au kudhihaki Mungu sio chochote? Uzuri Mungu sio mwingi wa hasira kama binadamu bali huchukizwa na yule asienenda kwa nyia zilizo nyofu,tuamini ipo siku hakika atajidhihirisha kwenu ili mumfahamu ya kuwa yeye yupo na anawezo wa kufanya lolote, wakati wowote na kwa vile inavyompendeza.
Biblia inasema Mungu ni Mungu wa wivu na hasira na anaadhibu hadi kizazi cha nne. Hiyo kusema sio mwingi wa hasira umelitoa wapi?
 
Wewe mwanao uliemzaa akikukosea huwezi ku
Dunia hii imepitia uongo/utapeli/propaganda kubwa sana na zikapita lakini uongo pekee uliodumu kwa muda mrefu ni huu:

Hebu fikiria; unaambiwa kuna MUNGU muweza wa yote yupo sahihi na hajawahi kukosea

Ameumba dunia kwa ajili yetu na ataiangamiza(jiulize akili za huyo Mungu anaewatakia maafa watu wake)

Alijua ataiangamiza dunia kabla hata hajaiumba lakini aliiumba hivyo hivyo ili aje kuiangamiza(kama vile hajielewi),

Ameumba moto wa jehanamu kwakuwa ametuumba tukosee ili atuchome moto japo alikua na uwezo wakutuumba tusiwe wakosefu ili atuumbie pepo tu tukale bata

Anajua tunacho hitaji lakini lazima tumuombe ili atupe, lakini hata tukimuomba hatupi tunavyotaka sisi maana tayari amekwisha tupangia kila mtu atampa nini, ataishije na atakufaje

Ndio muumba wa kila kitu(magonjwa, bangi, majini,umalaya,ukahaba, ulabu nk) na anaweza kudhibiti chochote lakini anamlaumu msaidizi wake muasi(Shetani) kuleta mambo hayo mabaya duniani (magonjwa nk) kwa watu wake aliyewaumba wakati yeye ndiye aliye mtupa msaidizi wake huyo huku duniani( inaelekea huyu hajiwezi mpaka awe na msaidizi mhuni,amuache tu amchanganyie habari)

Yaani yeye kashindwana naye huko mbinguni kaja kumtupa kwetu sisi viumbe dhaifu tupambane naye na tukishindwa tutachomwa moto milele, lakini anasisitiza anatupenda sana kama mtu anavyopenda na kujali mboni ya jicho lake

Hebu tafakari hili, kawaumba Adam na Hawa na wakati bado wageni duniani akawatupia Nyoka(Shetani) ili awarubuni, na kwa ugeni wao wakarubunika matokeo yake katupa adhabu ya shuruba watu wote hata ambao tulikua hatupo na hata ambao hawajazaliwa chamoto watakiona...... Not fair

Mungu muweza wa yote hayupo WAZI PASI NA SHAKA kwa watu wote kujua huyu ndio MUNGU badala yake Mungu ndio amekua sehemu kubwa ya mgawanyiko wa watu na kusababisha kuwa na imani za MIUNGU zaidi ya milioni dunia nzima

Na kibaya zaidi unatakiwa to blindly believe him, usihoji wala kuwa na shaka juu ya uwepo wake(ni laana na kufuru) vinginevyo moto wa milele unakuhusu

Yaani kuna mtoto wa fundi Kapenta mmoja huko Galilaya eti kafa kwa ajili ya dhambi za watu wote duniani.... Kweli jamani ?

Akaitwa neno. Neno huyo alikua Mungu, mtoto wa Mungu lakini Mungu huyu akajaribiwa na shetani na akapatikana. Shetani aliemuumba mwenyewe.

Mtoto huyu wa fundi kapenta, hakuandika kitabu chochote ila wahuni walio kuwa wanampinga ndio wakaja kuandika vitabu kuhusu dogo huyu na vinaitwa “Bibilia Neno la Mungu takatifu”

Mabilioni ya watu dunia kote wanakesha makanisani wakimlilia na kumuomba awape uponyaji, mali, waume/wake nk

Hebu fikiria huko Arabia kuna maamuma mmoja hajui kusoma wala kuandika alidai anashushiwa maagizo na Mungu kukata vichwa watu wote watakaopinga na kutokutii maagizo yake, “akashushiwa” aya za vitisho na neema kwa watakao tii, yaani ukifa unampigania Mungu unakwenda kupewa mabikra 72 kazi yako ni kuzagamua tu.

Mabilioni ya watu duniani wanasujudu mara 5 kwa siku na kushinda njaa mwezi kila mwaka ili wakale naye bata Peponi

Kwamba maisha yako hapa duniani ni ya mpito tu maisha yako yapo baada ya kufa

Unachotakiwa kufanya ni kumuamini na kufanya aliyoagiza ili ukale bata sana baada ya kufa

Badhi ya sababu za kutoamini uwepo wake hizo hapo mtoa mada. Zipinge tuonekumua

Hoja yako ya kwamba nani kaweza kutengeneza mbingu yake, na kama hakuna, kitu ambacho anakifanya Mungu mtu hakiwezi, kwa kuanzia, ina makosa ya kimantiki.

Logical fallacy. Logical non sequitur.

Ukweli kwamba mtu hajaweza kutengeneza mbingu yake unathibitisha kuwa mtu hajaweza kutengeneza mbingu yake.

Ukweli kwamba mtu hajaweza kutengeneza mbingu yake, hauthibitishi Mungu yupo kweli. Thibitisha kuwa Mungu yupo kweli.

Yani ni hivi, mimi nikishindwa kutengeneza filamu kama ya James Bond 007, hilo halithibitishi kwamba James Bond 007 yupo kweli.

Ukweli kwamba mimi siwezi kutengeneza filamu ya James Bond unathibitisha tu kuwa mimi siwezi kutengeneza filamu ya James Bond. Inawezekana kabisa nikawa siwezi kutengeneza filamu ya James Bond, na James Bond akawa hayupo, ni muhusika wa kufikirika tu wa riwaya na filamu, nje ya riwaya na filamu hizo hayupo.

Vivyo hivyo, inawezekana kabisa mimi nikashindwa kutengeneza mbingu yangu, na Mungu akawa hayupo. Hakuna contradiction wala logical inconsistency hapo.

Mimi kushindwa kufanya chochote hakuthibitishi Mungu yupo, kunathibitisha nimeshindwa kufanya hicho kitu.

Ukiunganisha mawili haya ambayo hayana uhusiano, unaanxa hoja kwa kufanya logical fallacy ya logical non sequitur.

Actually, mtu anaweza kusema kuwa ukweli kwamba hakuna mtu aliyeweza kutengeneza mbingu yake, unathibitisha Mungu hayupo.

Kwa sababu, Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na ujuzi wote, angekuwepo, angeruhusu kila mtu awe na uwezo wa kutengeneza mbingu yake. Mungu huyo si mchoyo wa neema. Angetupa tu neema hiyo ambayo yeye haimgharimu kitu.

Kwa hivyo, ukweli kwamba hakuna mtu aliyeweza kutengeneza mbingu yake, unaonesha Mungu huyo hayupo.

Hoja yako ukiitazama kijuujuu, utaona inaonesha Mungu yupo.

Lakini, ukiichambua kwa kina, utaona inaonesha Mungu hayupo.
Nawewe si ulijua utazaa watoto, watoto wako wakikukosea huwezi kuwaazibu kwa maneno au kwa vitendo?
Wewe hujawahi piga hata mtoto wako?
 
Kwanza jifunze tofauti ya "kusibitika" na "kuthibitika".

Piki, nimeeleza sana tofauti ya habari za imani, jinsi imani ilivyo haki ya kila mtu kuamini anavyotaka, ukweli kwamba imani ni haki ya kikatiba, na kwamba imani ni haki ya utu wa kila mtu, na jinsi imani inavyotetewa na "Universal Declarationnof Human Rights" tangu December 10 1948.

Nimeeleza kwamba imani ni haki ya mtu binafsi, na hata mimi ambaye siamini Mungu, nitatetea haki za wanaoamini kuamini wanavyotaka.

Nimepingana na mtu mwingine asiyeamini dini kama mimi anayetaka kupiga marufuku imani za dini, nikimueleza kuwa haki ya kuamini ni haki ya msingi sana, kila mtu aachiwe aamini anavyotaka.

Siko hapa kujadiki imani ya mtu.

Niko hapa kuangalia ukweli uko wapi.

Imani unaweza kuamini chochote unachotaka, ukweli au uongo.

Kutafuta ukweli kunajikita kwenye upande wa ukweli tu.

Unaelewa tofauti hii?
Na wewe tofautisha kati ya "piki" Na "pili" Umesema mwenyewe kila mtu aachiwe aamini anavyotaka sasa mbona unahoji imani za watu?

Wewe kuna siku tulikuambia ututhibitishie huyo mungu wako unayemuamini? Sisi tunaoamini uwepo wake mbona huwa hatuhoji kile ninyi mnachoamini na kama ni hivyo na sisi tutaomba maandiko ya kile mnachoamini.

Unapohoji imani ya mtu huwezi pata chochote maana imani huwa ni mtu na roho yake, japo inaweza kuzihirika kwa mtu kuonyesha matendo yake.
 
Wewe mwanao uliemzaa akikukosea huwezi ku

Nawewe si ulijua utazaa watoto, watoto wako wakikukosea huwezi kuwaazibu kwa maneno au kwa vitendo?
Wewe hujawahi piga hata mtoto wako?
Mimi si Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote.

Hivyo, mfano wako umenipa kazi kubwa kuliko uwezo wangu kwa mlinganisho na Mungu.

Ningekuwa Mungu huyo, ningeumba ulimwengu ambao watu hawakosei.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na mwenye upendo wote kuumba ulimwengu ambao watu wanaweza kukosea ni contradiction.
 
Na wewe tofautisha kati ya "piki" Na "pili" Umesema mwenyewe kila mtu aachiwe aamini anavyotaka sasa mbona unahoji imani za watu?

Wewe kuna siku tulikuambia ututhibitishie huyo mungu wako unayemuamini? Sisi tunaoamini uwepo wake mbona huwa hatuhoji kile ninyi mnachoamini na kama ni hivyo na sisi tutaomba maandiko ya kile mnachoamini.

Unapohoji imani ya mtu huwezi pata chochote maana imani huwa ni mtu na roho yake, japo inaweza kuzihirika kwa mtu kuonyesha matendo yake.
Mimi sihoji imani ya mtu, imani unaruhusiwa kuamini chochote, cha ukweli au hata uongo.

Mimi najadili ukweli uko wapi, hili ni jambo zaidi ya imani tu. Ukweli unaweza kuwa tofauti na imani.

Unaelewa tofauti hii?
 
Mimi si Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote.

Hivyo, mfano wako umenipa kazi kubwa kuliko uwezo wangu kwa mlinganisho na Mungu.

Ningekuwa Mungu huyo, ningeumba ulimwengu ambao watu hawakosei.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na mwenye upendo wote kuumba ulimwengu ambao watu wanaweza kukosea ni contradiction.
Wewe unaamini Mungu yupi?
 
Mimi sihoji imani ya mtu, imani unaruhusiwa kuamini chochote, cha ukweli au hata uongo.

Mimi najadili ukweli uko wapi, hili ni jambo zaidi ya imani tu. Ukweli unaweza kuwa tofauti na imani.

Unaelewa tofauti hii?
Kubali kwanza unahoji imani ya mtu maana mtu ndio anaeamini uwepo wa Mungu wake?
 
Mtu hakosei bali tamaa yake ndio inampelekea kukosea, binafsi naelewa miili yetu hii ni kama chombo kinachoendeshwa tu ambacho kinapokea nguvu toka pande mbili
1. Shetani
2. Mungu
Ukimuamini mmojawapo matendo yako yataendana na upande huo japo kuna watu wanakuwa vuguvugu kwamba kila upande yupo.
Ndio maana ukitaka kufanya jambo kuna imani mbili huwa zinapingana kimoyomoyo hio ni tosha inazihirisha uwepo wa pande mbili zinazopingana

Ila kwake kila goti litapigwa kuna mda na wakati utamuhitaji na utamtafuta sana naomba Mungu aachilie neema yake ya kumjua zaidi na wala wakati huo hautahoji haya maswali yako.
Mimi si Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote.

Hivyo, mfano wako umenipa kazi kubwa kuliko uwezo wangu kwa mlinganisho na Mungu.

Ningekuwa Mungu huyo, ningeumba ulimwengu ambao watu hawakosei.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na mwenye upendo wote kuumba ulimwengu ambao watu wanaweza kukosea ni contradiction.
 
Mtu hakosei bali tamaa yake ndio inampelekea kukosea, binafsi naelewa miili yetu hii ni kama chombo kinachoendeshwa tu ambacho kinapokea nguvu toka pande mbili
1. Shetani
2. Mungu
Ukimuamini mmojawapo matendo yako yataendana na upande huo japo kuna watu wanakuwa vuguvugu kwamba kila upande yupo.
Ndio maana ukitaka kufanya jambo kuna imani mbili huwa zinapingana kimoyomoyo hio ni tosha inazihirisha uwepo wa pande mbili zinazopingana

Ila kwake kila goti litapigwa kuna mda na wakati utamuhitaji na utamtafuta sana naomba Mungu aachilie neema yake ya kumjua zaidi na wala wakati huo hautahoji haya maswali yako.
Kwa nini Mungu kaumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na Shetani na uovu, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hauwezi kuwa na shetani wala uovu?
 
Kubali kwanza unahoji imani ya mtu maana mtu ndio anaeamini uwepo wa Mungu wake?
Hapana, sihoji imani.

Imani unaruhusiwa kuamini chochote, Allah, Buddha, Jehovah. Unaruhusiwa kuamini hata uongo wowote utakaotaka. Ni haki yako. Huko sitakuingilia.

Ukisema mimi naamini Jehovah kama Mungu wangu, halafu serikali ikaja na kusema tunafuta dini, tunafuta haki ya watu kuamini dini zao, nitaungana nawe kutetea haki yako ya kuamini unavyotaka, nitapingana na serikali.

Hata kama mimi sina dini, natetea haki za watu kuamini wanavyotaka, au kutoamini kabisa.

Hivyo, mimi sihoji imani. Imani ni kitu cha faragha ya mtu binafsi kinachotetewa na katiba na haki za watu.

Ila, ukija hapa JF na kusema, mimi najua ukweli kwamba Jehovah ndiye Mungu, yupo, hiyo ni statement ya fact, ushavuka imani, umetoka nyumbani kwako, umetoka kanisani kwako, umekuja JF public square kusema Mungu yupo kama fact, hiyo si imani tena, hapo tunajadili fact. Hapo ndipo nakubana uthibitishe Mungu yupo kama fact.

Unaelewa tofauti?
 
Back
Top Bottom