Uwezekano wa Rais aliye madarakani kuwa shahidi mahakamani ukoje kisheria?

Uwezekano wa Rais aliye madarakani kuwa shahidi mahakamani ukoje kisheria?

Mimi sio mwanasheria ila kwa mtazamo wangu kwakuwa Raisi anakinga ya kutokushtakiwa hvyo ata asipoenda sioni chochote atakachofanywa hvyo ni vile vile naungana na maoni ya wanaosema kwenda ni hiyar yake
Hiari Gani wakati yeye ndio analalamika anataka kupinduliwa.
 
Akikataa kwenda mahakamani nini kitatokea?
Na Lissu anataka aonyeshwe Dunia kuwa mahakama zetu ni dhaifu kama zinashindwa kufikishwa mashahidi mahakamani watahukumu vip hii kesi.

Kama Rais anadharau mahakama itadhirisha udhaifu wa mahakama zetu
 
Lazima aende ili kudhibitisha yeye kama Rais alikuwa na taarifa za kupinduliwa. Asipoenda mahakama itakwama.
Hawezi kutuma ushahidi wa kurekodiwa au wa maandishi kama wanavyofanya marais wa Marekani wakiitwa mahakamani?
 
Hawezi kutuma ushahidi wa kurekodiwa au wa maandishi kama wanavyofanya marais wa Marekani wakiitwa mahakamani?
Hawezi, maana lazima afanyiwe examination in chief na cross examination. Kwa kifupi lazima awepo.
 
Huyo mhaini ameshachanganyikiwa! Hv anafikiri Rais wa JMT ni km yule malaya wake Rose Mayemba? Huyo mwehu mvua zinamsubiri asitafute pa kushika na bado asubiri ripoti ya tume ya uchunguzi ataunganishwa na wenzake kina Heche, na wale malaya waliokimbia nchi
Punguza matusi. Wewe Kila mtu unamtukana Malaya hata kama hujui. Jadili hoja bila matusi
 
Ana kinga ya kutoshitakiwa,
Je anayo kinga ya kutokuwa shahidi mahakamani??
Anapelekewa wito na mahakama. Kukubali au kukataa ni hiyari yake. Akimaliza muda wake wa uongozi hapo ndio anaweza kushurutishwa kufika mahakamani kama raia wengine. Kuna kesi fulani Mkapa akiwa rais mstaafu alishawahi kuwa shaidi
 
Sasa mtuhumiwa akisema ushahidi wake wa utetezi hauwezi kukamilika bila rais kuwepo kesi itaamuliwaje ?
Kama mtuhumiwa akisema hivyo Kesi itakuwa ngumu, yatatumika mabavu
 
Back
Top Bottom