Uwezo wa vifaa vya kijeshi vya Mmarekani kutazamwa upya?

Uwezo wa vifaa vya kijeshi vya Mmarekani kutazamwa upya?

Nimeanza kwa kusema Iran siyo taifa la kubezwa Mmarekani, mwenyewe analifahamu! Hivyo hawezi kwenda akashambulia kiholela kwani anajua huyu siyo mtu wa mchezo na pia anajua Mashariki ya Kati patabana kwa Marekani.

Fikiria Syiria kumembana Iraq kumebana, Pakistan juzi ndiyo kafanya mazungumzo kulikuwa kumebana kinoma na kule ndiko chimbuko la ugaidi. Afghanstan kumebana hadi akawatoa wanajeshi wake baada yakuona wanauawa akawa anatoa misaada ya kijeshi kwa NATO na safari hii nato imesema haitaki kujihusisha na ujinga uliofanywa na marekani!

Fikiria Angel Mikhael anaenda kukutana Putin kuna mipango mingi sana Marekani hawezi kuthubutu hata hivyo kwa sasa Trump atakuwa katika vikao na washauri w anchi katika maswala ya kivita, pia kumbuka ukipiga Iran ni kuwa umewasha Israel hivyo yote haya yanaangaliwa kwa mapana.

Hivyo kwangu naona ni propaganda za kisiasa Trump akitafuta kuungwa mkono na washirika wake ili aanze chokochoko.
 
Trump anawachezea akili watu wapotezee issue ya kumuondoa madarakani.
Nimewaza kama mtoto .... ha haa haa.
 
Nenda ka swaki subiri Trump aamke avae na wigi lake ndio uulize hayo maswali
 
Tuombe Mungu aepushie mbali vita na migogoro itakayokatisha maisha ya watu na kutengeneza yatima, wajane, wagane, vilema na watu wasio na makazi.
 
Narudia hapa hakuna kitu!Marekani hawezi kuthubutu kutuma madege kuishambulia tulieni!
 
Tulieni jamani Trump aamke

mtarudi na vilio hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
wamarekani wenyewe wamegawanyika katika hiki kisanga ila Iran wana umoja ambao haujawahi kutokea hapo kabla, wameunganishwa na choko choko za Trump.... kila nikitazama naona Trump ana mengi ya kupoteza kuliko Iran
 
Na huyo US mwambie ashambulie Iran kutokea nchini kwake kama ataweza...
Kwani mashambulizi hayo yamefanyika kwenye base za jeshi la US ndani ya ardhi ya Marekani au kwenye base za jeshi la US ndani ya ardhi ya Iraq?

Nijuavyo mimi anga la Marekani liko protected zaidi ukilinganisha na anga la Iraq. Hao Iran wako kama ni wakali waambie washambulie ardhi ya Marekani yenyewe waone kama wataweza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marekani inaonekana hana defence nzuri kwenye kambi zake... Iran katupa makombora 15 na 11 yamehit target.. sasa hapo unaona kuna defence yoyote au ni propaganda za kutuaminisha kwamba jamaa hapigiki..

Hata hizo za eurooe zinapigwa tu.
Huko hawawezi..

Halafu mkuu sio kila kambi hapo Iraq iko sawa na nyingine, kuna kambi za 'Logistic', kuna kambi ni karakana, kuna kambi za ugavi wa zana..mifumo ya ulinzi inatofautiana. lengo la US hapo Iraq kabla halikua kuishambulia Iran,
 
Ni Russia tu ndio anangaliwa kama taifa pekee la kuzuia vita isitokee, kwa sababu: Russia ana urafiki mkubwa na Iran na akiwaomba Iran waache wanaweka kumsikiliza pia Russia anaweza kutumia uwezo wake Wa kijeshi kuisaidia Iran kitu ambacho si Ulaya wala Marekani wanatamani kitokee.

Pia, Russia anaweza asiingie kabisa kuisaidia Irani kwa kufanya kwa kufanya hivyo inamaanisha kumfanya Trump ashindwe na Trump ni MTU anayelinda maslahi ya Moscow pale Washington DC.

Ninachoona Russia atakubaliana na Marekani kwa siri kuridhia kuchapwa kwa huyo muajemi kwa makubaliano maslahi yake pale mashariki ya kati yadumu. na kwa hakika muajemi atapigwa bila msaada Wa anaoamini wangemsaidia
 
Uchambuzi huu una mapungufu makubwa Russia na Iran uwezi kuwatenganisha kwa sababu ya DC nakataa Iran na Russia ni maswaiba hawezi kumletea mwenzake usnitch wa hivyo.
 
Hivi unajua maana ya kambi?

Back
Top Bottom