Uwezo wetu wa akili ni mdogo mno, teknolojia yetu inaenda kama konokono, binadamu anachekwa kila kona

Time is relative not absolute..(Both literally and metaphorically speaking)
Siku moja kwako isiyo na maana kwako Kuna nzi amezaliwa kabalehe kaoa mpaka kafa.
Na wewe Toka uzaliwe mpaka Sasa una mvi Kuna nyangumi bado yupo tumboni Kwa mama ake hajazaliwa.

Kwahyo miaka iliyotumika kutoka iPhone 4 mpaka 12 unaona binadamu tupo slow Sana.
Hata aliens waliotumia mwezi kufanya hivo unaweza kuwaita slow kwasababu wameshindwa kutumia wiki Tu.
Na waliotumia wiki bado Ni slow kwasababu wameshindwa ndani ya masaa.

Kwahyo unaposema binadamu ni wajinga kwasababu WaPo slow inabidi useme ukilingamisha Na Nani.


Again. Time is relative.
 
Binadamu tukubali intelligence yetu imedumaa kwa kumtumikia ibilisi, kama tuliumbwa kwa mfano wa Mungu ina maana tunao uwezo wa ki Mungu ndani yetu. Kwa akili alizokuwa nazo binadamu alikuwa na uwezo wa kutatua changamoto yoyote ndani ya sekunde na ku predict changamoto za mbele na kuzitatua kabla hata hazijatokea.......leo hii magonjwa kama HIV yanakaa zaidi ya miaka 20 bila suluhu yoyote, kwenye korona ni kubahatisha bahatisha tu.......tumrudie Muumba tusijifanye wajanja.
 
Umeanza hadith Za ngano sasa
 
Unasema tecnolojia yetu ni ndogo, je, ni ndogo kujilinganisha na viumbe vipi?

Ni viumbe gani waliowazidi wanadamu kwa tecnolojia? Ng'ombe, mbuzi, kuku, vipepeo, kambale au viumbe gani waliotuzidi?
 
Ndungu yangu kuna MUNGU aliyeumba mbingu na nchi na ndiye anatawala vyote na hata akili zetu anazitawala. Maarifa yote anayo yeye na ni kweli sisi tuko very limited kwa mambo mengi sana. Nikifikiria tu magonjwa kama ukimwi, cancer na mengineo tunashindwa kugundua kweli madawa. Tunarudi palepale kwamba kuna aliyejuu na hatuwezi kumtoroka na siku akisema leo ndiyo mwisho wako huna la kufanya.
 
Sababu havikuwepo kabla kwenye magari mengine
 
ndo ujishughulishe ili ugundue, na ulete mawazo ya kujenga mfano; ukiunga kile na hiki unapata injini ya ndege, ukichanganya hiki na kile unajikuta uko sayari ya mars, ili yashughulikiwe na kuendelezwa, sio kulalamika tuuu for nothing.
 
Unasema teknolojia yetu ni ndogo, je, ni ndogo kujilinganisha na viumbe vipi?

Ni viumbe gani waliowazidi wanadamu kwa teknolojia? Ng'ombe, mbuzi, kuku, vipepeo, kambale au viumbe gani waliotuzidi?
Thanks bro, nilikua karibu ku comment ulichosema

Hoja yake nzima ina fail hapo, Kasi ya teknolojia ya binadamu ni ndogo ulikilinganisha na nini?

Hakuna comparison yoyote,
Huwezi kulinganisha na kasi ya πŸ‘½ alien, hatuna ushahidi kuhusu Alien wala Technologies zao

Pia major changes kwenye teknolojia zina tegemea kwa kiasi kikubwa Break through discoveries vitu ambavyo ni rare sana kwenye science

Once in a generation brains kama kina Newton, Einstein, Darwin, Hawking ni wachache sana

Pia hata kwa hizi vumbuzi zinazoendelea kiasi kikubwa cha akili kimetumika,kipe credit
Appreciate brains nyuma yake sio una take for granted tu

Tuna depend kwenye brains za wachache sana
 
Hapana, mimi siwezi kukubali najijua.
 
Tatizo kazi tuliyopewa na Mungu pia hatufanyi, Kushukuru, Kuabudu na Kutukuza ni kazi kubwa tuliyopewa wakati wa uvumbuzi Sasa wengi tunawasifu waliovumbua badala ya Mungu na wakati mwingine tunaomba tu bila Kushukuru tulivyopewa mfano mtu Kesha pata chakula badala ya Kushukuru anaanza kuomba tena hata kwenye tekinolojia hivyo hivyo badala ya kutumia na kushukuru Mungu mtu anaanza kuomba tena alichonacho.
 
Ndy kwanza 2021 may be mwaka wa 5050 kudadeki sintakuwa nimeshakufa
 
Basi ndo mje na solution au ndo akili zimeishia kutambua kama tupo nyuma na zimeshindwa kupata solution
 

Vijana mnaotoka chuo bana...
Nimesoma uzi wote unakosoa as if wewe una teknolojia yoyote hata hapo mtaani kwenu. Hebu jifunze ku appreciate kwanza maana hata kifaa unachotumia humu JF ni dhahili hayo ni matokea ya teknolojia unayoikosoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…