Uzalendo ni nini?

Uzalendo ni nini?

Kuanzia September 2015, uzalendo ni kumuunga mkono jiwe kwa kila alifanyalo, kutokumkosoa na kukubaliana na takwimu zote zinazotolewa na serikali bila kuhoji
 
Kuna maswali hapa huwa najiuliza napo wasikia wanasias wanadai uzalendo....

Swali linaanza uzalendo ndo nini

unawezaje kujua Huyu ni mzalendo na huyu si mzalendo.

maana nimepitia maelezo ya mwenyekit mmoja wa Chama fulani anadai kuwa vyama viwe vya kizalendo ...sasa nikajiuliza hivyo vyama vya kizalendo Tz ni vip na ambavyo si vya kizalendo ni vip....

Maana kuna wengine wanadai ukiwapinga waliopo madarakani basi siyo mzalendo na usipo wapinga ndo mzalendo...

aise tusaidiane wan JF

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzalendo ni kuwa mshamba na kukata viuno kushangilia CCM na mwenyekiti wake.

tapatalk_1533709787775.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Not quite, wengi wetu tunaipenda serikali yetu lakini hatutambuliki. Siku hizi uzalendo ni kupigania serikali, kutoikosoa kwa namna yoyote ile, kuiunga mkono kwa kila kitu inachofanya na kuishangilia.
usipo ikosoa huku unashuhudia twiga anapanda ndege kwa mfano....au watu wanapiga kama epa vile na sijui kama ile wanayoidai watu 1.5 hivi unakuwa mzalendo ama ndo tafsili ya. nini hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nachojua uzalendo ni kupenda nchi yako lakini sio chama unaweza kua upendi serikali lakini unapenda nchi yako
 
Habari wanajamvi. Kama kuna kitu kinanitatiza sana miaka hii ni matumizi ya neno "UZALENDO". nikiwa shule ya msingi niliwahi fundishwa kuwa mzalendo ni "mtu anaeipenda NCHI yake, na kuwa tayari kuipigania na hata kufa kwa maslahi ya nchi yake". Labda kama walimu wangu walinidanganya maana nachokiona leo ni tofauti na nilichofundishwa. Sikuhizi nasikia hawa wanasiasa wetu wakikusikia unaikosoa serikalo au kuwa na maoni tofauti na wao juu ya mambo fulani watasema WEWE SIO MZALENDO. mfano, lissu,zitto na wengineo walipokua wakikemea mambo mbalimbali kama mauaji n.k .. Baadae pia nikasikia UZALENDO ni ile hali ya kuhama toka upinzani na kuiunga mkono SERIKALI iliyopo madarakani. Mnaojua maana ya uzalendo msaada please. Nataka kuelewa.
 
Nani huyo aliwahi sema hivyo

Zaidi ya hilo Uzalendo no juu ya kile ambacho unadhamiria kukifanya na kujitoa kuitumikia na kuilinda nchi yako,
 
kwa zama hizi za jiwe maana ya neno uzalendo imebadilika.
Kwa sasa uzalendo wa nchi ni kuunga mkono lolote lile linalofanywa na jiwe hata kama
ni libaya.
Mfano Jiwe alivyosema hana mpango na katiba mpya hata kama ipo kwenye ilani kumtetea kwa nguvu zote huo ni uzalendo.
Jiwe alivyosema watu hawaruhusiwi kulalamika kwamba vyuma vimekaza, uzalendo ni kumuunga mkono hadi mwisho ukipinga na kusema vyuma vimekaza wewe unaonekana ni fisadi na sio mzalendo.
Kuwa Mzalendo ni kukubali kwamba uchumi unakuwa hata kama hauna kitu mfukoni ,yaani huku mtaani kuna wazalendo hawana hata nguo wanashindia matishirt ya ccm huku wakiimba uchumi umekuwa, hao ndio wanaonekana wazalendo.
yaani hii nchi imekuwa kweli shithole
 
Uzalendo ni kushiriki kuifanyia mema nchi yako...uwe na chama ama LA ilimradi uitendee jema kila wakati.
Kama kunakikundi kinaiwazia nchi mabaya au kuchochea ubaya utokee ama kupinga mazuri yafanywapo ama kujenga chuki basi hao wamepungukiwa uzalendo.
 
Walimu wako wapo sahihi kwenye definition hizo za Uzalendo,japo kwa mazingira tuliyonayo kwa sasa;
Uzalendo ni hali ya kuunga mkono/kupongeza lolote linalofanywa na kiongozi/viongozi [haswa kutoka chama tawala] taasisi ya serikali na serikali yenyewe,kinyume cha hapa wewe sio mzalendo na utawajibika juu ya kauli/maoni au chapisho la mlengo wa pili uliloliandika...
Sheikh23_Political Analyst
 
Back
Top Bottom