Uzi maalum kwa wale wanaopinga uwepo wa Mungu

Kwaiyo siku huyo aliekuletea elimu ya science akianza kuikataa na akakufundisha nawewe utamkubali?
 
Kabla sijaenda kuonesha ni kwa nini naamini Mungu yupo ushaelewa maana ya neno IMAN na misingi ya imani?
Misingi hiyo ya imani imejengwa katika uongo kwa sababu vitu vyote vya kuona, kusikia na kutenda vinafanyika na viungo vya binadamu.

Macho huona, masikio husikia, ubongo huamua na kisha mwili kwa ujumla hutenda.

Hivyo definition yako ya imani ni definition UCHWARA.

Definition yako ni ya MCHONGO.
 
Kwaiyo tuseme neno IMANI halipo au lisitumike mfano tusiseme "naamini mtoa mada amepata muongozo"

Hilo neno IMANI lisiwepo maana halina msingi wowote au halina faida
 
we jamaa mbona unarudia swali ni kua huelewi au ni nini, ksoma bandiko upya,

"soma kwa hatua"
Nilisha kufafanulia kwamba akili ya binadamu haipo limited.

Hiyo limit unayo idai ipo ni uongo kwa sababu binadamu hufanya tafiti, uchunguzi na udadisi wa kuvumbua vitu asivyo vijua

Hivyo binadamu kutokujua kitu fulani si kwamba akili yake ipo limited bali ni kwamba bado utafiti na uchunguzi wa kujua kitu hicho hajaufanya hadi kufikia kupata jibu.
 
mambo mangapi yanafanyiwa utafiti na hamna jibu ?
 
Kwaiyo tuseme neno IMANI halipo au lisitumike mfano tusiseme "naamini mtoa mada amepata muongozo"

Hilo neno IMANI lisiwepo maana halina msingi wowote au halina faida
Nilikwambia kwamba, Imani ni kutokuwa na uhakika.

Ndio maana unasema "Naamini mtoa mada amepata muongozo" kwamba huna uhakika kwa asilimia mia kwamba mtoa mada amepata muongozo ila una amini tu, kwamba mtoa mada atakuwa amepata muongozo.

Ungekuwa na uhakika kwa asilimia mia kwamba mtoa mada amepata muongozo, Ungesema
"Najua mtoa mada amepata muongozo"

Na uhakika utakuwa nao kwa vile tayari unajua kwa uhakika zaidi.

Na si kwa imani tena.
 
mambo mangapi yanafanyiwa utafiti na hamna jibu ?
Mambo hayo kukosa majibu si hitimisho(conclusion) ya kusema kwamba majibu hayapo kamwe.

Tafiti nyingi zilishindwa sana mpaka pale majaribio mengi zaidi na zaidi yalipo endelea kufanyika ndipo majibu yakapatikana.

Mfano, waliojaribu kwenda mwezini walirusha vyomba vingi sana angani bila mafanikio lakini mwishowe walifanikiwa kufika mwezini kwa kuendelea kufanya tafiti zaidi na zaidi.

Hivyo jambo fulani kukosa jibu si hitimisho la moja kwa moja kwamba jambo hilo halina jibu na halitakaa lipate jibu.
 
This logical fallacy is called non sequitur.

Kitu cha kwanza inachotakiwa kufanya ni kuthibitisha Mungu yupo.

Kabla ya kusema Mungu kaumba hiki au Mungu kaleta hiki, thibitisha Mungu yupo kwanza.
 
je kuhusu uwepo wa Mungu mbona wewe umeshaweka conclusion kwamba hayupo,

wakati sanansi yenyewe haina majibu na hai conclude kua hayupo
 
This logical fallacy is called non sequitur.

Kitu cha kwanza inachotakiwa kufanya ni kuthibitisha Mungu yupo.

Kabla ya kusema Mungu kaumba hiki au Mungu kaleta hiki, thibitisha Mungu yupo kwanza.
mfano umekuta nyumba imejengwa, lakini hujawakuta mafundi hapo au umekuta tu vifaa vyao wenyewe hawapo

hauta tumia uwepo wa vifaa walivyoacha au jengo walilojenga, kuthibitisha kua mafundi wapo arround ?
 
je kuhusu uwepo wa Mungu mbona wewe umeshaweka conclusion kwamba hayupo,
Kwa sababu mimi sidai kwamba Mungu yupo.

Mnaodai Mungu yupo ni ninyi na inabidi mthibitishe madai yenu.
wakati sanansi yenyewe haina majibu na hai conclude kua hayupo
Sayansi haisemi Mungu yupo.

Sayansi ina kanusha madai yenu ninyi mnaosema Mungu yupo halafu hamna uthibitisho.

Sayansi inasema Mungu hayupo kwa vile hakuna uthibitisho wowote ule wa uwepo wa Mungu huyo.

Hivyo ukiweza kuthibitisha Mungu yupo utai prove wrong sayansi kwa kusema Mungu hayupo.

Na sayansi ita conclude Mungu yupo kutokana na uthibitisho wako.

Lakini cha ajabu ni kwamba mpaka sasa mmeshindwa kuithibitishia sayansi kwamba Mungu yupo.

Ila mnafosi imani zenu uchwara ziwe ukweli bila kuleta uthibitisho.
 
wewe mwenyewe umetoka kusema kwamba sayansi ikishindwa ku prove kitu saivi sio kwamba hakipo, inawezekawa ikafanikiwa kuprove baadae,

kwa mantiki hiyo, uta conclude vipi Mungu hayupo kwasababu Sayansi imeshindwa ku prove Yupo ?
 
mfano umekuta nyumba imejengwa, lakini hujawakuta mafundi hapo au umekuta tu vifaa vyao wenyewe hawapo

hauta tumia uwepo wa vifaa walivyoacha au jengo walilojenga, kuthibitisha kua mafundi wapo arround ?
Ukiuchukua mfano huu, ukasema kwamba kilicho complex hakiwezi kuwapo bila kuumbwa, kimantiki, unaweza kukubali kuwa nyumba haiwezi kuwepo bila kujengwa na mtu.

Na unaweza hata kukubali kuwa mtu hawezi kuwepo bila kuumbwa na Mungu.

Na mantiki hiyo hiyo itakutaka ukubali kwamba Mungu hawezi kuwapo bila kuumbwa na yeye, na aliyemuumba naye kaumbwa, hivyo hivyo, bila mwisho.

Katika ulimwengu huo, hakuna Mungu.

Umeitoa hoja yako kama uthibitisho kuwa Mungu ni lazima awepo.

Lakini, ukiiangalia kwa undani hiyo hoja, kiukweli inaonesha Mungu hayupo na hawezi kuwepo.
 
Kwa ufupi wanakataa uwepo wa Mungu ambao wanauwezo mdogo sana wa kufikiri,hwafikirii katika uhalisia zaidi ya nadharia za walio watangulia.
 
wewe mwenyewe umetoka kusema kwamba sayansi ikishindwa ku prove kitu saivi sio kwamba hakipo, inawezekawa ikafanikiwa kuprove baadae,

kwa mantiki hiyo, uta conclude vipi Mungu hayupo kwasababu Sayansi imeshindwa ku prove Yupo ?
Kwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, pingamizi si kwamba hajathibitishwa tu.

Pingamizi ni kwamba hoja ya kuwepo kwake ina internal contradiction.

Ni kama useme kuwa katika Euclidean geometry, pembetatu ina nyuzi 180 na duara lina nyuzi 360, halafu kuna pembetatu ambalo hapohapo ni duara.

Obviously pembetatu ambayo hapohapo ni duara haiwezekani kuwapo, kuwapo kwake kunashindikana kwa sababu sifa ya pembetatu, nyuzi 180, inapingana na sifa ya duara, nyuzi 360.

Unaelewa hilo jambo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…