Uzi maalum kwa wale wanaopinga uwepo wa Mungu

Uzi maalum kwa wale wanaopinga uwepo wa Mungu

Na utuelezee kivipi neno "akili" yani kitu ambacho hakipo kitumike kuelezea utendaji wa ubongo , inatumikaje ?
Ulisoma nomino dhahania katika lugha ya kiswahili?

Akili ni sawa na njaa, hofu, kiu, hamu,

Ni maneno ambayo hayapo katika uhalisia bali katika dhana ya kufikirika.
 
Kwahiyo shida yako ni kuhusu neno "Mungu" ?
Shida yangu ni ninyi waamini huyo Mungu kudai kwamba huyo Mungu ni nguvu halisi badala ya kukiri kwamba Mungu huyo ni mawazo yenu tu yasiyo na uhalisia wowote ule.
 
hata
Hoja ipi umetoa ya kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu?

Zaidi ya kuhusisha vitu vilivyopo na kutaka kudai vimeumbwa na huyo Mungu?

Thibitisha Mungu yupo yeye kama yeye.

Sio kutumia vitu vilivyopo kutaka kufosi mawazo yako uchwara kusema kwamba ni Mungu ndio kaumba.

Kwa umri nikiwa bado mdogo nimesali sana, pia nimesoma seminari.

Lakini baada ya kukua na kuanza kujifunza na kuchambua hizi dini na imani kwa kina nikagundua kwamba kuna uongo mkubwa sana kwenye mafundisho ya imani na dini kwa ujumla.

Maisha yenyewe ni nguvu iliyopo wala hayahitaji nguvu nyingine ili yaweze kuwepo.
mimi pia nimesoma seminari, kwaiyo hapa ni waseminari wawili tumekutana,

unasema umechambua dini ukaona ni uongo, ila mimi nimezungumzia uwepo wa Mungu na sijazungumzia kabisa dini,

wewe umechambuaje dini na kujua Mungu hayupo ?
 
Unazungumziaje uwepo wa Mungu bila kuthibitisha uwepo wa Mungu huyo?

Huoni kwamba unazungumzia habari za uongo zisizo na uthibitisho wowote ule?
 
ipo tuu kivipi, kwanini unaamini ipo tuu
Kwa sababu kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na muumbaji, Hata muumbaji atahitaji muumbaji wake.

Na Muumbaji wake atahitajika kuwa na Muumbaji wake.

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho jitokeza chenyewe pasipo muumbaji maana kitavuruga muundo mzima wa ulazima awepo muumbaji.

Hivyo kutakuwa na waumbaji wengi endless to infinity.

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na muumbaji wake, Hata huyo Mungu lazima awe na Muumbaji wake.

Na kama sio lazima kila kitu kiwe na muumbaji, Hata dunia haihitaji kuwa na muumbaji.
 
Sasa wewe unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo?

Utafiti upi unathibitisha pasi shaka kwamba Mungu yupo?

Mungu ni nini?
Swali lako halitofautiani na la siafu wanaobishana juu ya uwepo wa binadamu!

Siafu aamini au asiamini kuwa binadamu yupo hakuwezi kumfanya binadamu asiwepo!
 
Nakuuliza tena aliekuletea hio elimu yamu physics ni nani hadi wewe mtu wa nanjilinji leo umeimeza na kuilezea kwa lugha ya kigeni? Jibu usikimbie swali
Elimu nyingi tumeletewa na wazungu.

Zipo elimu zenye uthibitisho zinazo dhihirisha ukweli wa vitu na mambo katika dunia yetu. Zikiwemo Physics, chemistry, Biology n.k

Pia zipo elimu za kutungwa na kusadikika tu zisizo na uthibitisho wowote ule wala uhalisia. Dini zikiwemo.
 
Mtoa mada acha kutumia nguvu nyingi kubishana, MUNGU ni Imani tu Wala sio kitu Cha kuthibitika, unajichosha kumwaminisha na kumponda mwenzio kuwa MUNGU yupo wakati mwenzio ata ww pia hukuwahi kumuona Wala hujui anafananaje Bali unayaishi mafundisho uliyopokea Kwa dini yko hyo na jamii iliyokuwekea hofu ya MUNGU ndani yko,mnabishana bure tu hasa ww unayeamini MUNGU yupo na hujui anafananaje, we SEMA tu mm nna Imani yupo na sio kushikilia kuwa yupo uhakika km ushakaa ukapiga nae stori uyo MUNGU
 
Kwa sababu kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na muumbaji, Hata muumbaji atahitaji muumbaji wake.

Na Muumbaji wake atahitajika kuwa na Muumbaji wake.

Pasiwepo kitu chochote kile kilicho jitokeza chenyewe pasipo muumbaji maana kitavuruga muundo mzima wa ulazima awepo muumbaji.

Hivyo kutakuwa na waumbaji wengi endless to infinity.

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na muumbaji wake, Hata huyo Mungu lazima awe na Muumbaji wake.

Na kama sio lazima kila kitu kiwe na muumbaji, Hata dunia haihitaji kuwa na muumbaji.
hicho ulicho kisema ndo nilichoongelea kwamba akili ina limit na huwezi fikiri nje ya hapo maana akili inajiona imefikiri hadi mwisho

kuna namna nyingine sisi tunaweza kufikiri kitu na ku tatua au kubuni njia fulani,
ila ukimwambia nyani, hawezi hata umuue, hawezi kwasababu kuna sehemu ufikiri wake unaishia

kwaiyo hata hapo ulipoona kwamba cycle zitajirudia to infinity ndo conclusion inayokuja kwenye akili ya kibinadamu kutokana na level ya ufikiri.
 
Elimu nyingi tumeletewa na wazungu.

Zipo elimu zenye uthibitisho zinazo dhihirisha ukweli wa vitu na mambo katika dunia yetu. Zikiwemo Physics, chemistry, Biology n.k

Pia zipo elimu za kutungwa na kusadikika tu zisizo na uthibitisho wowote ule wala uhalisia. Dini zikiwemo.
Sasa mzungu huyo huyo akuambie kuna Mungu na huyo huyo akuambie hakuna Mungu wewe huoni hapo muongo ni mzungu kwaiyo kama unakataa elimu zao zikatae zote
 
Kuna mtu nyuma ya keyboard yake anasema La illahi illallah muhammadur rasulallah
 
Mtoa mada acha kutumia nguvu nyingi kubishana, MUNGU ni Imani tu Wala sio kitu Cha kuthibitika, unajichosha kumwaminisha na kumponda mwenzio kuwa MUNGU yupo wakati mwenzio ata ww pia hukuwahi kumuona Wala hujui anafananaje Bali unayaishi mafundisho uliyopokea Kwa dini yko hyo na jamii iliyokuwekea hofu ya MUNGU ndani yko,mnabishana bure tu hasa ww unayeamini MUNGU yupo na hujui anafananaje, we SEMA tu mm nna Imani yupo na sio kushikilia kuwa yupo uhakika km ushakaa ukapiga nae stori uyo MUNGU
nina uhakika kabisa yupo, wanaosema hayupo kunavitu hawavielewi au wamefungwa akili au wamekaza kichwa

kuna uzi nilikutana nao humu muda fulani umeandikwa

"Atheist wana mtindio wa ubongo"

labda ni kweli, kwasababu kuna namna ata ukijaribi kuwaelezea hawaelewi,
kuna kitu nataka wakipate nawapa ma mfano rahisi ila hamna kitu wanaelewa yaani

ila nikawaza huenda wameelewa ila hawataki kukubalihapa kswala la kisaikolojia) kwasababu wameshakua kwenye upande huo kwa muda
 
Sasa mzungu huyo huyo akuambie kuna Mungu na huyo huyo akuambie hakuna Mungu wewe huoni hapo muongo ni mzungu kwaiyo kama unakataa elimu zao zikatae zote
Huwezi kukataa elimu yenye uthibitisho na inayothibitishika mafundisho yake kwa kuleta uvumbuzi wa shida mbalimbali

Yani ni sawa unataka kuwaambia madaktari wakatae elimu ya kutibu magonjwa kwa vile ni elimu kutoka kwa mzungu.

Au watu wakatae kutumia simu kwa vile ni elimu kutoka mzungu.

Kuna elimu za ukweli na zenye uthibitisho wa matokeo chanya ya mafundisho yake hizo niza kukubaliwa.

Pia kuna elimu za uongo ikiwemo habari za uwepo wa Mungu zisizo na uthibitisho wowote ule zaidi ya hadithi tu, Hizi ni kuzikataa.

Maana hata asilimia kubwa ya wazungu ni Atheists, Hawa amini uwepo wa huyo Mungu.
 
Swali lako halitofautiani na la siafu wanaobishana juu ya uwepo wa binadamu!

Siafu aamini au asiamini kuwa binadamu yupo hakuwezi kumfanya binadamu asiwepo!
😂Sasa mkuu siafu si wanawaona binadamu 😂 ww MUNGU ushawahi kumuona? Kama unaamini MUNGU yupo na hukuamini zumaridi alivosema yeye ni mungu VP je km kwel MUNGU alikuja Kwa njia ya zumaridi 🤔. Swala la MUNGU ni Imani tu kwnz mfano mwanadamu aunde roboti, robot litafata Kila kinachoamrishwa na mwanadamu kamwe haliwez kwenda against na aliyelitengeneza. Ila Kwa MUNGU ni tofauti Yani kaumba watu na kawapa maarifa ambayo hayo hayo maarifa wanatumia kufikiria uwepo wake,bas wasioamin uwepo wa MUNGU hawana makosa mana walipewa maarifa hyo na yeye mwnyw
 
Back
Top Bottom