Uzi maalum kwa wale wanaopinga uwepo wa Mungu

Uzi maalum kwa wale wanaopinga uwepo wa Mungu

nimeshatoa hoja nyingi za kuthibitisha, hazijajibiwa ila zinapingwa kwa maswali yaleyale, na ambayo hayajibu hoja.
Hoja ipi umetoa ya kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu?

Zaidi ya kuhusisha vitu vilivyopo na kutaka kudai vimeumbwa na huyo Mungu?

Thibitisha Mungu yupo yeye kama yeye.

Sio kutumia vitu vilivyopo kutaka kufosi mawazo yako uchwara kusema kwamba ni Mungu ndio kaumba.
napenda pia kujua kitu kimoja kutoka kwako na Kiranga na wengine wasioamini pia,

hujawai kusali, kuswali, au namna yoyote ya ku-contact with higher power
Kwa umri nikiwa bado mdogo nimesali sana, pia nimesoma seminari.

Lakini baada ya kukua na kuanza kujifunza na kuchambua hizi dini na imani kwa kina nikagundua kwamba kuna uongo mkubwa sana kwenye mafundisho ya imani na dini kwa ujumla.
nguvu ambae imefanya maisha yawepo,

au mtazamo wako kuhusu hilo
Maisha yenyewe ni nguvu iliyopo wala hayahitaji nguvu nyingine ili yaweze kuwepo.
 
basi thibitisha kwa kutumia physics kwanini dunia inazunguka jua na haisimami na speed yake ni almost the same kwa mamilioni ya miaka ?

uki refer kwenye laws of motion za Sir Isaac

utasema kitu kinakua kwenye state yake hadi external force iwe aplied ndo itakibadilisha,

je hata hiyo state yake ya kuzunguka ilianzishwaje,
Kuna ulazima gani kwamba state ya Dunia kuzunguka jua ilianzishwa?

Kwa nini unadhani lazima state ya Dunia kuzunguka jua iwe imeanzishwa?

Kwa nini hudhani state ya Dunia kuzunguka jua ipo tu yenyewe?
hata ukieleza mambo ya ma big bang, eleza kilicho nyuma yake

kwakua ni maswala ya physics, thibitisha kwa physics au kwa namna nyingine pia. Thibitisha
 
Lakini ni wewe uliyesema sayansi haina mambo ya kuamini,

Kuhusu hili neno "akili" inamaanisha nini ? Ni neno la kufikirika na limerasimishwa na tunaamini hivyo ( Imani ).
Akili ni neno la kutungwa ambalo hutumiwa kuonyesha ufanyaji kazi wa ubongo wa kiumbe fulani.

Huwezi kuthibitisha uwepo wa Akili, kwa vile akili ni neno la kufikirika na kutungwa tu.
 
Nakiri na nashahadia kuwa hakuna Mungu isipokuwa Allah tu.

Wanaosema mungu hakuna ni nusu Waislam hao, bado kukiri tu kuwa yupo Allah, asiyezaa wala kuzaliwa na hagfananishwi na chochote.
 
Akili ni neno la kutungwa ambalo hutumiwa kuonyesha ufanyaji kazi wa ubongo wa kiumbe fulani.

Huwezi kuthibitisha uwepo wa Akili, kwa vile akili ni neno la kufikirika na kutungwa tu.
Kwahiyo kipi kinakuchanganya kuelewa kuwa neno Mungu ni la kutungwa linaloelezea Higher power iliyofanya kila kilichopo ulimwenguni kuwepo.
 
Ameshakimbia, Kuna maswali yamemzidi uwezo wake alionao.
Akiambiwa anakataa mwanadam anafahamu theluthi ya vitu vya duniani the Almighty God know everything ambavyo binadamu hajui

Wakifunuliwa ufunuo mdogo wanajifanya wajuaji
 
nimeshatoa hoja nyingi za kuthibitisha, hazijajibiwa ila zinapingwa kwa maswali yaleyale, na ambayo hayajibu hoja.

napenda pia kujua kitu kimoja kutoka kwako na Kiranga na wengine wasioamini pia,

hujawai kusali, kuswali, au namna yoyote ya ku-contact with higher power

nguvu ambae imefanya maisha yawepo,

au mtazamo wako kuhusu hilo
Katika kutafuta jibu sahihi, tunaweza kuanza kuyatoa (kuyaondoa) majibu yasiyo sahihi ili kuelekea kwenye jibu sahihi, hata kama hatulijui jibu sahihi bado?

Mfano, Juma ni mwanamme mwenye miaka 30 leo, hamjui mama yake mzazi, anamtafuta.

Je, Juma anaweza kujua kuwa Jeni, binti mwenye umri wa miezi 6 leo, kamwe hawezi kuwa mama mzazi wa kibaiolojia wa Juma, mwanamme mwenye miaka 30 leo?

Tunaweza kukubaliana hilo kwanza, kwamba Juma anaweza kujua kuwa Jeni si mama yake mzazi, hata kabla Juma hajajua mama yake mzazi ni nani?
 
Kuna ulazima gani kwamba state ya Dunia kuzunguka jua ilianzishwa?

Kwa nini unadhani lazima state ya Dunia kuzunguka jua iwe imeanzishwa?

Kwa nini hudhani state ya Dunia kuzunguka jua ipo tu yenyewe?
ipo tuu kivipi, kwanini unaamini ipo tuu
 
Una elewa Physics ni nini?

Au unadhani physics ni kitabu cha kuandikwa kama riwaya zenu za Biblia?
Nakuuliza tena aliekuletea hio elimu ya physics ni nani hadi wewe mtu wa nanjilinji leo umeimeza na kuilezea kwa lugha ya kigeni? Jibu usikimbie swali
 
Akili ni neno la kutungwa ambalo hutumiwa kuonyesha ufanyaji kazi wa ubongo wa kiumbe fulani.

Huwezi kuthibitisha uwepo wa Akili, kwa vile akili ni neno la kufikirika na kutungwa tu.
Na utuelezee kivipi neno "akili" yani kitu ambacho hakipo kitumike kuelezea utendaji wa ubongo , inatumikaje ?
 
Kwahiyo kipi kinakuchanganya kuelewa kuwa neno Mungu ni la kutungwa linaloelezea Higher power iliyofanya kila kilichopo ulimwenguni kuwepo.
Ni ninyi kutokubali kwamba hiyo dhana yenu ya "Mungu" ni neno la kutunga tu na kutaka kufosi ndio uhalisia na ukweli.
 
Katika kutafuta jibu sahihi, tunaweza kuanza kuyatoa (kuyaondoa) majibu yasiyo sahihi ili kuelekea kwenye jibu sahihi, hata kama hatulijui jibu sahihi bado?

Mfano, Juma ni mwanamme mwenye miaka 30 leo, hamjui mama yake mzazi, anamtafuta.

Je, Juma anaweza kujua kuwa Jeni, binti mwenye umri wa miezi 6 leo, kamwe hawezi kuwa mama mzazi wa kibaiolojia wa Juma, mwanamme mwenye miaka 30 leo?

Tunaweza kukubaliana hilo kwanza, kwamba Juma anaweza kujua kuwa Jeni si mama yake mzazi, hata kabla Juma hajajua mama yake mzazi ni nani?
ndio atajua kua sio kwasababu hawezi kumzidi umri mama yake
 
Back
Top Bottom