Uzi maalum kwa wale wanaopinga uwepo wa Mungu

Hakuna kitu kinachoshikilia uhai wangu, izo ni Imani zako tu.. usikwepeshe thibitisha kuwa Mungu yupo
Sijaamini chochote hapo ni logic ile ile unayosema.. kama hakuna kinachoshikilia uhai wako means wewe sio kiumbe hai?


Kuhusu kuthibisha nimethibisha kama unashindwa kuona uthibitisho ambao ni wewe mwenyewe utawezaje kuona hayo mengine?
 
bado unazunguka bila kutoa sababu,
inawezekanaje Dunia iwepo tuu...
Kwa sababu dunia haijaumbwa.

Dunia ipo tu, kwa sababu haijaumbwa.

Usicho elewa ni nini?
Theists tuna sababu tukisema Mungu alikwepo tu hajaumbwa na Ataendelea kuwepo tuu.
Na wewe toa sababu.

Onyesha ni wakati gani huyo Mungu aliumba Dunia?

Uni prove wrong kwamba dunia ilikuwepo tu.

Na unionyeshe kwa uthibitisho Mungu huyo alivyoumba dunia na kwamba dunia haikuwepo tu bali iliumbwa.
Atheists mna sababu ipi ya ku-support kwamba kitu kina weza kuwepo tuu bila sababu, je hii ni hali ya kawaida ?,
Uli elewa niliyokwambia mwanzo,

Sababu ni hii..👇

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe kimeumbwa Hata Muumbaji wa kila kitu lazima awe ameumbwa.

Na kama si lazima kila kitu kilichopo kiwe kimeumbwa, Hata Dunia haihitaji iwe imeumbwa.

Usicho elewa ni nini?

Au unakaza fuvu tu!!
hata kama unasema dunia ilikwepo tuu
je hiyo ni hali ya kawaida kwamba kitu kiwepo tuu ?
Kwa nini unadhani si hali ya kawaida?

Kwani ni lazima isiwe hali ya kawaida?

Kwa nini hudhani ni hali ya kawaida?
kama sio kitu cha kawaida unakiekezeaje simply kwa kusema ni simple Logic na hamna extraordinary power beyond everything beyond human understanding ?
Hiyo extraordinary power ndio Dunia yenyewe.

Labda wewe umeamua kuita na kuipachika hiyo Extraordinary power jina Mungu.
 
Kasome kwanza ndo uje tujadiliane, maana naona we umeisoma biblia tu, vingne hujataka kuvisoma
Tuseme mimi sijaelewa na naona kabisa wewe ndugu yangu kisomo kimepanda.. nisaidie ili na mimi ambae sijui nielewe ili nisije nikawa napotea kwa ujinga
 
Tuseme mimi sijaelewa na naona kabisa wewe ndugu yangu kisomo kimepanda.. nisaidie ili na mimi ambae sijui nielewe ili nisije nikawa napotea kwa ujinga
Bahari zimeundwa kutokana milipuko ya volcanic, iliyosababisha maji kutokea chini ya Ardhi kuja juu, maana uko chini ya Ardhi huwa Kuna maji
 
Tuseme mimi sijaelewa na naona kabisa wewe ndugu yangu kisomo kimepanda.. nisaidie ili na mimi ambae sijui nielewe ili nisije nikawa napotea kwa ujinga
Miti imeevolve kutoka kwenye mimea ya ferns na mosses ilikuwa baharani mwanzo, lakin movement ya maji ya bahari ikaisambaza mpka nchi kavu, iyo ni miaka 370 million iliyopita.
Miti ni viumbe hai, ambavyo pia vime evolve
 
Tuletee huo uthibitisho na sisi tuuone
 
Bahari zimeundwa kutokana milipuko ya volcanic, iliyosababisha maji kutokea chini ya Ardhi kuja juu, maana uko chini ya Ardhi huwa Kuna maji
ni kweli kuna maji chini na juu pia kuna maji.. lakini yanachanzo.. hivyo vina chanzo.. havitokei tu
 
Miti imeevolve kutoka kwenye mimea ya ferns na mosses ilikuwa baharani mwanzo, lakin movement ya maji ya bahari ikaisambaza mpka nchi kavu, iyo ni miaka 370 million iliyopita.
Miti ni viumbe hai, ambavyo pia vime evolve
Sasa hayo unayosema miaka million kadha sote wawili hatukuwepo tumejifunza baada ya kuzaliwa.. na kila mtu anathibisha kwa namna yake kwamba ni kweli ama si kweli..


Ni nini hasa kimekufanya usiamini uwepo wa Mungu angali wakati hayo yanatokea hukuwepo ila ulifundishwa ukayakubali..
 
Matendo ya Mitume 17:24.,25.,26.,27.,28.,29.


24. Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;

25. wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.

26. Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;

27. ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu.

28. Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.

29. Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu.



Mind you hapo Paulo alikuwa ameenda kwa wagiriki wenye shule zao mababa wa kisomo wakawa wameandika kwa Mungu asiyejulikana..
 
Ifanyike ba

Tangu nianze kuona hoja zako jambo ambalo nimebaini ni tatizo kwako, ni ukomo wako wa kufikiri,

Ukomo wako wa kufikiria ndio unaokupa mateso chief
 
Ndo nikakuuliza Mungu yeye ameumbwa na nani?
Ukishasema MUNGU inatosha kukueleza kwamba ni mwanzo na mwisho..



Yohana 1:1.,2.,3.,4.
1. Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.


2. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

3. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
 
Kwa sababu hakuna aliyethibitisha uwepo wa Mungu.
Ila kisayansi, inawezekana ukajua umri wa kitu Fulani kwa vipimo, na njia maalumu kama CARBON 14. so vitu vyote ivi vimethibitishwa kisayansi
 
Ifanyike ba


Tangu nianze kuona hoja zako jambo ambalo nimebaini ni tatizo kwako, ni ukomo wako wa kufikiri,

Ukomo wako wa kufikiria ndio unaokupa mateso chief
Nafikiria nje ya box chief, siwez amini vtu ambavyo havipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…