We mbona unakisia Mungu yupo wakati hujawah kumuona Wala kumsikia, umejuaje yupo?
Kuhusu uwepo wa MUNGU nina uhakika yupo. Mimi mwenyewe ni kazi ya mikono ya MUNGU na huu ni ushahidi tosha kuwa MUNGU yupo.
MUNGU alituumba kwa mfano wake, maana yake sisi tuna tabia za Kiungu ndani yetu na moja ya tabia ya Kiungu ni kuumba.
Sisi binadamu tunaumba au tunabuni vitu na kuvitengeneza. Mfano meli, magari, robots nk. Hii tabia na uwezo wa kubuni na kutengeneza tumeipata kutoka kwa MUNGU aliyetuumba kwa mfano wa tabia zake.
Chochote kile kilichotengenezwa juu ya dunia ni kazi ya mikono ya mtu fulani. Kila ubunifu uliopo duniani una mmliki wake. Mfano, tukiona robots tunajua mbunifu wake wa kwanza ni George Devol. Huo ni uthibitisho kwamba "robots" zimeumbwa au kutengenezwa na mwanadamu.
Hakuna kitu au kiumbe kilichojitengeneza au kujiumba chenyewe. Mwanadamu aliumbwa na yeye pia anaumba vitu. Mwanadamu aliumbwa na MUNGU. Tumejuaje?
Tumejua kwa sababu BWANA MUNGU kupitia maandiko anatuambia kuwa Yeye ndiye MUUMBA wetu.
Kama vile The Wright brothers walipotengeneza ndege ya kwanza walijitangaza kwa kusema wao ndiyo wenye hati miliki (patent) ya ndege ile waliyoitengeneza.
BWANA MUNGU naye vivyo hivyo kupitia maandiko anajitangaza kuwa YEYE ndiye mwenye hati miliki yetu sisi na viumbe wengine wote ikiwemo dunia na ulimwengu wote (the whole universe).
Hizo kazi za mikono yake ni uthibitisho tosha kuwa MUNGU yupo. Kama vile sisi pia kazi za mikono yetu zinathibitisha uwepo wetu.
Akitokea mtu anapinga kwamba George Devol sio mtu wa kwanza kutengeneza a programmed robot, aje na uthibitisho kutuonesha kuwa George Devol hakutengeneza robot ya kwanza.
Vivyo hivyo mtu anayepinga kuwa BWANA MUNGU hakuumba mwanadamu, mtu aje na uthibitisho unaotuonesha kuwa BWANA MUNGU hakumuumba mwadamu.