Ukiyatazama maji kama mtu alieko Jangwani utaona kama maji ndio kitu cha muhimu kuliko vyote huku duniani.
Ukiyatazama maji kama mtu anaeishi sehemu yenye chemchem na mifereji ya kunyeshea mboga hutajua kama maji ni kitu gani kwenye maisha.
Ukiyatazama maji kama mtu alienusurika kufa kwenye meli iliyoua maelfu ya watu au ile Tsunami utaona maji ni kitu kibaya sana kwenye dunia hii.
Na hivi ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu ya kila siku.
Usiwaambie watu maisha ni magumu au ni mabaya kwasababu ya kile unachopitia au ulichopitia. Usiwaambie watu ndoa ni mbaya kwasababu ya ubaya ulioona kwenye ndoa yako.
Usiwaambie watu jinsia fulani sio waaminifu kwasababu ya huyo uliekuwa nae.
#USIISHIE_NJIANI
Ambiere Kiviere
Sent using
Jamii Forums mobile app