Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nyama ya kuku ina kiasi kingi cha vitamini – Niacin na Vitamini B6 -Vitamini hizi mbili husaidia sana mwili kufanya kazi zake vizuri na kutengeneza nguvu ya kutosha. Niacin husaidia mwili kudhibiti kiasi cha sukari na huhitajika na mwili ili kubadilisha mafuta, protini na wanga kuwa nishati (nguvu) . Vitamini B6 husaidia mwili kubadilisha wanga na kuwa nishati (nguvu)
 
Nyama ya kuku ina kiasi kidogo cha mafuta (Hususan ikipikwa na mafuta kidogo tu na kutolewa ngozi ya nje) – Hii husaidia kupunguza matatizo yatokanayo na mafuta mengi mwilini na kuweza kutumika hata na watu wenye mafuta mengi mwilini na magonjwa yatokanayo na tatizo hilo
 
USHAURI

Punguza ulaji wa nyama nyekundu kama vile nyama ya ng’ombe, mbuzi, kondoo na badala yake kula nyama ya kuku. Kula zaidi kuku wa kienyeji na wapike au wachome ili wasiwe na mafuta mengi. Kwa kuku wa kisasa hakikisha hauvunji na kutafuna mifupa yao maana mabaki mengi ya dawa huachwa huko, utakuwa unakula na dawa zilizotumika kuwakuzia na kuwatibia.
 
Pimia vyakula unavyopika ndani ya sinki na rudisha kila kitu mahali pake baada ya kukitumia ili vitu visilundikane kwenye meza au sinki. Jitahidi kufanya maandalizi yanayotakiwa kabla ya kuwasha jiko.
Aisee. Itabidi nifuate ushauri huu. Siku nikipika yaani mazagazaga kibao mpaka kichwa kinaniuma...
 
Yaah Ahsante ila mim napenda samaki zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…