5. Kula vitu vyenye sukari mara kwa mara:
Kula kashata, ufuta, ubuyu, visheti, biskuti, pipi, keki, bazoka (Big G, orbit, n.k.) mara kwa mara, hasa vile vyenye sukari huongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa kuoza kwa meno. Mabaki ya vyakula hivi hutumiwa na bakteria (wanaoozesha meno) kutengeneza asidi inayoharibu sehemu ngumu ya nje ya jino na kuacha matundu. Punguza matumizi ya vyakula vyenye sukari, njia mojawapo ikiwa ni kuvitumia vyakula hivyo wakati wa unapokula milo mikuu mitatu