Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuusafisha mfumo wa damu

Matibabu ya uvimbe wa tezi ya shingo yanapaswa kuanza kwa kuusafisha mfumo wote wa damu na kuanzisha matumizi ya mlo unaostahili pamoja na utulivu na mapumziko ya kutosha.
 
Mgonjwa anaweza kubadili taratibu mlo wake na kuanza kutumia mlo ulio na virutubisho kamili. Katika utaratibu huu anapaswa kula matunda yaliyo katika hali ya upya wake (fresh), yasiyo na muda mrefu tangu yachumwe.
 
Matunda hayo yanapaswa kuwa matufaa (Apples), Machungwa, zabibu, mapeasi, na madalanzi, jamii za karanga zilizo mbichi na glasi ya maziwa yasiyochekechwa kuondolewa mafuta vitumike asubuhi. Chakula cha mchana kinapaswa kuwa mboga za majani zilizochemshwa au kupikwa bila kuiva,
 
chapati zilizopikwa kwa ngano ya atta isiyokobolewa na glasi ya maziwa mazito yasiyochekechwa mafuta. Supu ya mboga za majani, saladi za mboga mbichi za majani kama vile nyanya, karoti, letusi, kabeji, celery na tanipu. Mbegu za Alfalfa,
 
jibini ngumu iliyotengezwa kienyeji na jamii zote za karanga zikiwa katika ubichi zitumike wakati wa usiku. Glasi ya juisi ya matunda au maziwa inywewe kabla ya kwenda kulala usiku. Vinywaji kama chai, kahawa, unga uliokobolewa na vyote vinavyotengezwa kwa ngano
 
Mengine ya Kuzingatia:

Madini ya Joto (Iodine)

Vyakula vilivyo na madini joto kwa wingi vinapaswa kutumika bila kipimo kwa muda wote kwani humsaidia mgonjwa kupona haraka. Vyakula hivi ni pamoja na mboga za majani kama vile Kabeji, vitunguu swaumu, asparagus, oats, karoti, vitunguu na nyanya, strawberries, na mchele usiolowekwa.
 
Back
Top Bottom