Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nyoka ni viumbe hai ambao wapo kwenye daraja la reptilian kutokana na uainishaji wa viumbe hai. Viumbe hawa wapo wa jamii nyingi sana, na inakadiriwa kuwa kuna aina takribani elfu tatu ( 3,000) za nyoka duniani. Licha ya kuwepo aina nyingi za nyoka duniani ila ni jumla ya aina 375 tu ya nyoka ndio nyoka wenye sumu ambapo ni sawa na asilimia 12.5%. Ukweli ni kwamba jamii nyingi za nyoka ambazo zinaishi karibu na binaadamu huwa ni nyoka ambao hawana sumu ya kusababisha kifo pale anapo muuma binaadamu.
 
Na huwa ni ngumu sana kwa nyoka kumuuma binaadamu kama nyoka huyo hana hofu ya kuuwawa au kupata mshtuko wa hatari. Hatua ya kwanza kabisa ya nyoka huwa anakimbia pale anapohisi kuwa kuna hatari, ila inaposhindikana na anapohisi hakuna namna ya kukimbia basi nyoka hapo hulazimika kujiandaa kwa ajili ya kuuma.
 
Sasa kutokana na kuwepo kwa aina nyingi za nyoka ni vyema tukachagua aina moja ili tumsome hapa. Na bila kupoteza muda leo tutamsoma nyoka ajulikanae kwa jina la KOBOKO.

Lakini koboko hawa wapo wa aina mbili ambao na koboko mweusi na koboko wa kijani. Sasa hapa nitamzungumzia KOBOKO MWEUSI
 
SIFA NA TABIA ZA KOBOKO MWEUSU

1.Ndiyo nyoka mrefu kuliko nyoka wote miongoni mwa nyoka wenye sumu wapatikanao barani Afrika.

2.Ni nyoka mwenye sumu kali zaidi na anachukuliwa kuwa nyoka wa pili duniani katika nyoka wenye sumu kali. Anapo kuuma ukikosa huduma ya kwanza nza ndani ya dakika ishirini basi unaweza poteza maisha.

3.Koboko mweusi ni nyoka mwenye uwezo wa kukimbia kwa kasi kuliko nyoka wote duniani na ana uwezo wa kukimbia hadi kilometa ishirini kwa saa (20km/saa)
 
4.Ni nyoka mwenye hasira sana na mwenye uwezo wa kuuma ndani ya sekunde chache pale tu anapo hisi kuna hatari.

5.Koboko weusi wana rangi ya kijivu au wakati mwingine rangi ya kahawia nah ii hutokana na mazingira anayoishi ndio huendana na rangi ya mwili ili kumfanya asionekane kwa urahisi zaidi.



6.Anapo kuwa anakimbia au kupata hasira, nyoka huyu ana uwezo wa kuinua moja ya tatu ( 1/3 ) ya mwili wake. Hii inashangaza sana hasa unapo muangalia unaweza ukasema kuna kitu kina mwinua nyoka huyu ila kumbe ni uwezo wake tu.
 
7.Ni nyoka ambao wana weza kuuma mara nyingi zaidi tena ka muda mfu na pale wanapouma basi hutoa kiwango kikubwa sana cha sumu.

Kutokana na uwezo mkubwa wa nyoka huyu kukimbia, tabia zake nyingi sana bado hazijaweza kugundulika. Ila utafifiti bado unaendelea ili kujifunza mengi hasa tabia za nyoka huyu hatari duniani.

MUHIMU KUJUA

Jina koboko mweusi halitokani na rangi ya ngozi yake na wengi huchanganya sana hapa. Nyoka huyu kama nilivo eleza hapo juu hana rangi nyeusi kabisa. Jina koboko mweusi lina tokana na kuwepo kwa rangi nyeusi ndani ya mdomo ambayo huwa tofautisha nyoka hawa na nyoka wengine.

Watu wengi huamini nyoka huyu kuwa ni shetani kutokana na rangi hii iliyopo ndani yam domo wake
 
Back
Top Bottom