Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

BZ34ELBlwA7.jpg
 
1. Unanunua nguo bila mpangilio. Kuna watu wana nguo kama duka. Please kuwa na nguo chache tu huwezi kushindana na fashion.
2. Unanunua viatu bila mpangilio. Viatu pia vinameza savings zetu. Nunua pea chache zenye ubora ili zidumu.
 
3. Unatoa ofa bar bila mpangilio. Nendaa bar kwa bajeti mahususi. Hakuna atakaye kusifia kwa kutoa ofa hovyo. Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake. Jifunze ubepari.
4. Unatumia hela nyingi kwenye simu ambazo sio productive. Unaweka vifurushi vya week vya sh. 7000 au 10000 ili uchati na marafiki FB au whatsapp, huo ni ujinga badilika.
 
5. Unakopa hela benki na unanunua vitu kama simu ya milioni na gari la ambazo sio productive. Unakosa hela hata ya mafuta, gari la nini kwanini usingewekeza sehemu ili kuwe na mradi wa kuzalisha ndio ununue gari?
6. Una marafiki wengi ambao ni mzigo kwako au hamuendani kivipato hivyo unajikuta unalazimika kutumia zaidi ya kipato chako ili uwa-impress. Meneja wa TRA na mwalimu wa sekondari unatarajia utoe ofa mpaka umfurahishe meneja wa TRA? Ubaki na sh ngapi katika salary yako? Zinduka.
 
7. Huna timetable ya kudumu ya maisha yako , unajikuta una buruzwa tu na marafiki zako na kwenda sehemu mbalimbali za matumizi. Kuwa na ratiba za maisha yako na zisimamie kikamilifu, usiburuzwe.
8. Una michepuko inayokutegemea wewe kwa kila kitu. Wanakuita ATM wewe unakenua tu huzinduki. Badilika.
 
Back
Top Bottom